Siku ya jana hiki kitu kili-pop out kwenye akili yangu nikaona ni zooooooom kwa ukaribu zaidi kudhibitisha ukweli wa hiki kitu.
Nili-google picha za nyumba za makazi za wenzetu kwa kweli sikuona fensi ndefu zote fupifupi.
Nikajaribu ku-recall picha za movies, nikawasha Tv kuangalia taarifa ya habari za nje kwa kweli muonekana wa fensi niendelea kuuona kuwa ni ule ule. Hata kwa baadhi zilikua ndefu bado kulikua na uwazi ambao mtu aliepo nje anaweza kuona ndani fensi kunanini.
Sitaki kuamini kuwa maeneo yote yapo hivyo ila hii kitu inaweza kuwa na fashion au ni matakwa ya mamlaka.
Huku kwetu sasa, fundi anajenga mpaka tofali zitakapo ishia na wenye uwezo wanaongezea electric wire yani ni vurugu.
Kwenu sasa Wataalam wa nyumba na makazi bila kuwasahau Diasporas na wengine wote wenye kufahamu ukweli wa ilijambo.
View attachment 2184038