Hivi iliyofuzu AFCON 2024 Jana nchini Algeria ni Taifa Stars au Rais Samia?

Hivi iliyofuzu AFCON 2024 Jana nchini Algeria ni Taifa Stars au Rais Samia?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Na kama Jibu ni Taifa Stars sasa kwanini kila Kiongozi akizungumza baada ya Kufuzu AFCON Jana anatumia Sekunde 20 Kuipongeza, ila anatumia Dakika Saba (7) hadi Kumi (10) Kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan?

Leo GENTAMYCINE nawachana Live (Mubashara) nyie Viongozi wote wa Serikali wa Ngazi zozote kuwa Mnaboa kwa Kujipendekeza Kwenu kila mara Kumsifu Rais Samia na nina uhakika hata Yeye pia anaboreka nanyi na huenda hata Kimoyomoyo huwa anawaita Wapumbavu (Mapopoma) japo Machoni atajifanya anawapeni Tabasamu lake la Kizanzibari.

Nirudi Kwako Rais Samia Suluhu Hassan tafadhali nikuombe Zuia hii Viongozi wako Kujifanya Wanakusifia na Kukuabudu kwa kila Tukio Chanya kwani ndiyo hawa hawa Siku Ukistaafu na akija Rais Mwingine watakuhama, watakusema vibaya, watakuchafua na Kukudharau huku wakiwa Wanamsifia tena Kinafiki huyo Rais ambaye atakuja baada yako.

Nimalizie tu kwa nyie Viongozi Majuha na Wanafiki mnaopenda Kujipendekeza kwa Rais Samia Suluhu Hassan huku mkijifanya mnamsifia hadi Kumlamba Miguu yake kuwa iliyofuzu AFCON Jana ni Taifa Stars ya Watanzania na siyo Rais Samia Suluhu Hassan wenu sawa?

Taifa Stars ni ya Watanzania wote na siyo ya Rais Samia Suluhu Hassan peke yake. GENTAMYCINE naheshimu Mchango wake na Serikali yake lakini ni Upumbavu (Upopoma) usiovumilika Kulazimisha Akili (Fikra) zetu Watu wenye Upeo mkubwa duniani kuwa Mafanikio ya Timu kwa 99.9% yametokana na Yeye (Rais Samia) wakati kila Mtanzania kwa upande wake Kafanya alichokiweza na hatimaye AFCON ya mwakani (2024) nasi Tanzania tutakuwepo / tupo.

Kusema Ukweli Kwangu NI Tunu Kuu.
 
Rais ndiye msimamizi wa shughuli zote ndani ya nchi,team ya taifa ikifanya vibaya pia lawama zitaenda kwa serikali inayoongozwa na rais wa nchi,

Nawasilisha.
 
Mkuu hivi kulikua na ahadi ya kununua magoli?
 
Wanalinda vibarua vyao. Huu utaratibu wa kusifu na kuabudu ulianza awamu ya tano.

Hata haya mambo ya kuitana waheshimiwa yanatukuzwa sana huku kwetu. Ulaya hawafagilii. Huko majuu hata PhD holders ni nadra sana kulazimisha watu mtaani kutanguliza title ya Profesa au Dokta.

Bongo tunapenda sana kusifiwa.
 
Hakika Mama Samia Suluhu Hassan, The Mother of Modern Tanzania, atawatoa 'mafurofuro' nyie haters haki ya nani..........kila mnakozunguka, Mama Samia huyu hapa!!!
 
Chipukizi wa CCM watakuroga mkuu acha kuwapopoa.
Bahati nzuri Kwangu na Mbaya Kwao Moto Wangu GENTAMYCINE hapa JamiiForums wanaujua na waje kwa Nidhamu zote vinginevyo nitawavuruga Wote.

Kuna Vitu vinakera na havivumiliki hats kama Wengine ni Mashabiki ( si Wanachama ) wa CCM na tunavutiwa na Uwajibikaji wa Kusuasua wa Mwenyekiti Taifa.
 
Mkuu hivi kulikua na ahadi ya kununua magoli?
Ahadi ninayoijua ni Serikali kuipa tu DP World Bandari zote, Maziwa na Mito yote bila kusahau na Samaki zote za Tanzania na zile zilizoko Matumboni mwao Samaki wenye Mimba.
 
Wanalinda vibarua vyao. Huu utaratibu wa kusifu na kuabudu ulianza awamu ya tano.

Hata haya mambo ya kuitana waheshimiwa yanatukuzwa sana huku kwetu. Ulaya hawafagilii. Huko majuu hata PhD holders ni nadra sana kulazimisha watu mtaani kutanguliza title ya Profesa au Dokta.

Bongo tunapenda sana kusifiwa.
Obama na Clinton wana PhD,ila huwezi jua,ila Rais wenu na uDokta wa kupewa,akiwa anatambulishwa anaitwa Dkt Samia...Rubbish
 
Umeme ukikatika italaumiwa serikali na sio wafanyakazi wa Tanesco,umeme ukiwa stable itasifiwa serikali na wafanyakazi wa Tanesco pia coz serikali ndiye msimamizi na mpanga mikakati na kutoa fedha.
 
Back
Top Bottom