Hivi inakuaje mama mzazi ni mdogo kuliko mume wa binti yake

Hivi inakuaje mama mzazi ni mdogo kuliko mume wa binti yake

Nimekutana nayo jana hii nilipomsindikiza jamaa kumsalimia mama wa mwanamke aliyezaa naye. Jamaa lina miaka 56 halafu binti aliyemzalisha ana miaka 24 na mama wa binti ana miaka 49, Mtoto wao sasa ana miaka mitatu.

Changamoto niliyoikuta ni kwenye salamu, binti hakumpa jamaa shikamoo lakini Mama akampa jamaa shikamoo
Chai
 
Siku hizi ukioa utajikuta umeoa mtoto wa age mate, class mate wako. Kali zaidi ni kuoa mke ambaye mama yake pia ni mdogo kiumri kwako. Sasa kama binti kakupenda utaanzaje kumkataa awe mke wako?
 
Tamaa za mabinti wanajikuta wanawavulia nguo wanaume umri wa babu zao na baba zao
Ni haki zao za kikatiba na kibinadamu.

Msiwanyanyapae watu kwa kutumia haki zao.

Mradi wao wamekubaliana inatosha.
 
Kuna jamaa mama mkwe wake alimuambia binti yake kuwa bwana ake ni saizi yake, binti akajisikia vibaya kuolewa na mwanaume saizi ya mama yake
 
Yupo jamaa mwingine alikwenda kujitambulisha ukweni. Akakuta wakwe zake amewazidi umri wote mama na baba. Baba akamuuliza binti yake umempendea nini mzee huyu, mbona unaolewa na mtu mzee? Binti aliwajibu wazazi nimempenda acheni anioe!
 
Siku hizi kupata mke ambaye wazazi wake ni wazee ni shughuli pevu. Inabidi uoe waliopo ambao mama zao pia wana umri mdogo kuliko wewe.
 
Changamoto za kuoa wanawake ambao mama zao umewazidi umri ni mama mkwe kukosa heshima, anakuona ni saizi yake baada ya kuzoeana. Wengine ni wahuni hutaka kuonja mpiko wa mume wa binti yake. Kama kichwa hakiko sawa unaweza ukapita na mia kwa mama mkwe mwenye shobo na miparato mingi. Heshima huwa zero na huona hakuna shida na wao watafunwe sambamba na mabinti zao.
 
Inasikitisha sana!

Kwahiyo na wewe msindikizaji ulisalimia shikamoo au ulisalimiwa?
Niliiepuka hiyo kwa kuambiwa karibu kaka yangu. Japo mimi ni mzee ila nina kamwili fulani hivi kauongo. Ukizingatia siku hizi tunanyoa nywele zote kuficha Mvi na kipara
 
Nimekutana nayo jana hii nilipomsindikiza jamaa kumsalimia mama wa mwanamke aliyezaa naye. Jamaa lina miaka 56 halafu binti aliyemzalisha ana miaka 24 na mama wa binti ana miaka 49, Mtoto wao sasa ana miaka mitatu.

Changamoto niliyoikuta ni kwenye salamu, binti hakumpa jamaa shikamoo lakini Mama akampa jamaa shikamoo
Eeh Shikamoo ya nini wakati wanakula tundra wote!
 
Siku hizi ukioa utajikuta umeoa mtoto wa age mate, class mate wako. Kali zaidi ni kuoa mke ambaye mama yake pia ni mdogo kiumri kwako. Sasa kama binti kakupenda utaanzaje kumkataa awe mke wako?
Kama Daudi wa kwenye Biblia Alioa kabinti ili apate joto,sisi ni nani tuwakatae Mkuu!
 
Kama Daudi wa kwenye Biblia Alioa kabinti ili apate joto,sisi ni nani tuwakatae Mkuu!
kuna jamii za wafugaji vijijini ni fasheni mzee kuoa binti ikiwa mke wake amezeeka na mikikimikiki ya kuchakatwa hawezi tena, mzee huoa kigori amsaidie bi mkubwa majukumu hayo pamoja na kumpa joto mzee. Binti hakatai ndio mila zao zilivyo
 
Iyo inawezekana kabisa. Kibaolojia tumetofautiana. Mimi nina class mate wangu wa shule ya msingi alizaa akiwa form 3. Sasa hivi binti yake ni mkubwa kabisa naweza hata kumuoa.
 
Back
Top Bottom