Hivi inakuaje mtu kufanya hivi?

Hivi inakuaje mtu kufanya hivi?

Leo nilikuwa nimetoka ofisini Sasa kwa bahati mbaya kifurushi changu Cha mwezi kikawa kimeniishia

Na Kibaya zaidi ninapokwenda siwezi kwenda bila kuwa na muda wa maongezi

Nikaona ni vema nichukue vocha kwanza kabla Sijaanza safari yangu ya kwenda huko ninakotaka kwenda.
Eneo letu la kazi pembezoni Kuna sehemu ni grocery lakini pia Wana m.pesa na huwa wanauza na voucher pia

Sasa nikafika pale nikawakuta vijana baadhi wanapata vinywaji vyao pale nikawasalimia Kisha Nikaagiza voucher

Wakati najiandaa kutoa hela Kuna kijana mmoja miongoni mwa wale waliokuwa wamekaa pale Wanakunywa

Akaniambia kwa kujiamini we brother ninunulie pombe."

Nikamuuliza Mimi?

Akajibu ndio wewe hapo."

kwa sauti ya kukaza"

Sasa nikamtazama nikagundua Kwanza amelewa tayari japo sio sana

lakini pili muda anaokunywa pombe ni muda wa kazi hakustahili kuwa pale muda ule kwa kijana anayejitafuta

Badala yake alipaswa awe kazini au kutafuta kazi ili kuitafuta hatima yake ya jioni anaporudi nyumbani

Nikajisemea moyoni kwamba angeniomba hela ya kula alikuwa sahihi lakini pombe na kwa hali hii aliyo nayo sipaswi kumpa

Basi nikamjibu kwamba Sina hela aisee Niko vibaya boss wangu,..

Cha ajabu na cha kushangaza akadakia kwa sauti kubwa akaniambia afu we bigi nilikuwa nakuheshimu kumbe ni k...u...m...kabisa eti?""

Unavaa smart hela hata ya pombe moja huna matako wewe"una nini wewe huna hata Mia hapo?

Aiseeh. Nilijikuta nimelipukwa na hasira za ghafla

pembeni Kuna brother mmoja alikuwa ameshika chupa ya soda huku akimshangaa yule jamaa

Nilitamani niichukue Ile chupa nimnyooshe kisawa sawa yule jamaa lakini nikaona si busara kwani jamaa amelewa itaonekana nilipigana na mlevi

Na watu wote mle ndani walikuwa wameduwaa kwa mshangao

Na istoshe namfahamu fahamu kwani anashinda eneo la jirani na ofisini kwangu

Nilichokifanya nikawaza haraka haraka nikaona huyu acha nimalizane nae kwa akili siwezi kumwacha hivi hivi huyu boya

Nikamuuliza kwa upole kwamba Je! unataka nikuonyeshe nilicho nacho?

Akajibu kwa jazba na kujiamini ndio nionyeshe tuone una nini wewe?""

Nikachomoa wallet nikatoa shilingi laki moja nikamuuliza umeniita k. Si ndio?

Unaweza kunionyesha hata robo au theluthi ya kiasi hiki au hata alfu mbili ya kisungura hicho unachokunywa ?

Akabaki ametoa jicho tuu huku akitazama hela nilizokuwa nimezishika kwa macho ya uroho

nikamwangalia nikaona huyu boya kalowa tayari

Nikamuuliza tena kwa upole nikasema Sasa ndugu yangu unaniitaje Mimi k...u..m...a. wakati huna hata alfu mbili mfukoni halafu mtoto wa kiume?

Nikakuta kazubaa na Anaanza kujilegeza Kama mtoto wa kike ambaye yupo tayari kutoa tunda

Nikamtazama nikakaa kwenye kiti Kisha nikamwambia.

Sasa nilikuwa na haraka lakini naona leo acha tupige story kwani hatufahamiani vizuri au sio?
Akaitikia fresh big Mani kwa sauti ya puani.

Nikamuuliza hiyo pombe bei gani kwani mpaka tunafikia hatua ya kutukanana boss wangu?

akadakia buku mbili tuu big Mani"

Nikamwabia tena kwa upole unaonekana Kama una hamu Sana na pombe mwanangu au sio?

Akajibu Sana brother" nikaona hazijamkaa sawa bado huyu.

Nika mwambia yule brother mwenye Ile ofisi naomba umpe huyu jamaa visungura kumi halafu na mimi hapa nipe maji ya bariidi tuendelee kupiga story na jamaa yangu hapa

Yule mhudumu akamuuliza yule jamaa huku akimkazia macho eti eti nikupe visungura kumi uta maliza ?

Jamaa likajibu lete hizo namaliza mwenyewe na hakuna mtu kugongea nilijua tu ataninunulia nikimchokonoa huyu big mani huku likicheka cheka

Nikamwitikia au sio mi mwenyewe nilijua unatania tu haukuwa siriasi huku nikimkenulia meno kinoko

Basi Akaletewa pombe zake bwana na mimi Nikamwambia jitahidi umalize ukishindwa utazilipia mwenyewe lakini huku nikiwa nimemkazia sura kidogo

Likaitikia mbona Cha mtoto hiziii. basi nikasema sawa

Akapiga ya kwanza kufika ya tano nikakuta jamaa anaanza kulegea hata story nnazompigisha anashindwa kujibu

Haukupita mda Sana yule mhudumu akatoka nje

Ile anarudi hajakaa hata dakika mbili akaja mtendaji ananiambia nimesikia habari yako bwana killing machine

Naomba Kama mtendaji wako na tunaheshimiana msamehe kijana huyus asije akaumaliza mwendo kesho serikali ikatudai mtu wao

Nikamwambia yule mtendaji amuulize amekubali kushindwa/katosha?

Jamaa akaitikia kwa kunyanyua kichwa mzee akasema basi mwache

Skuongea kitu wakuu zaidi ya kuwaambia vijana wengine waendelee kunywa zilizobaki

Nikamtuma na kijana mmoja akanunue maziwa mabichi lita moja wamnyweshe ndugu yangu iwapo hali yake itaendelea kuwa mbaya zaidi Kisha nikaishia zangu

Sasa mpaka Sasa najiuliza huyu jamaa kwanini alifanya vile kwangu?

Je watu Kama hawa huwa wanajiamini nini kufanya hivyo?

Ningeomba Kama Kuna wataalam wa mambo kama haya watufafanulie kidogo

kwamba kwanini mtu anamchukia/au kumzoea mtu ambaye hajawai hata kupiga nae hata story?

Na kingine ni kwamba..

Kiukweli kahela kangu kameniuma Ila hata moyo wangu naona umejawa na tabasamu mwanana humu ndani kwangu..,,

Niwatakie jioni njema wakuu zangu 🙏🙏🙏
Asante mkuu kwa simulizi. Ila nami nimetia mkono kwenye andiko lako kurekebisha kidogo
 
Bora wewe umefika huko, Mimi hizo R mahali zisipostahili zimenishinda kuendelea kusoma. Mtu hela anaandika hera, kutafuta anaandika kutafta🤣🤣🙌
Kumbe naweza kufanya kazi kwenye mazingira magumu kukushinda, kuna mwamba kamaliza kabisa.
 
Back
Top Bottom