Hivi inakuwaje mama anamuonea wivu mtoto wake?

Umeanza vizuri sanaaa ila umemaliza vibaya sana,shubaamit mmoja wewe...[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Brother una akili nyingi mnooo!
Mungu akulinde uendelee kushusha nondo namna hii hii,yaani umeongea na kuonyesha ulivyo akili kubwa...
 
nimesoma comment za wadau, zipo za aina mbili wapo wanaopinga mkuu kuuleta huu uzi kuwa kayaweka mambo ya watu hadharani,.

na wengine wapo wanaosema mwanamke kakosea,

mimi sikubaliani na hayo mawazo kwanza nimejifunz kitu, na hili ni jukwaa la mapenz na mahusiano, vitu kama hivi ambavyo ndo vipo real ni vizuri kuvitumia kama case study, kikubwa hajatoa utambulisho halisi aidha wa namba jina au eneo alipo.

lakini pia mwenye makosa pia ni mwana ume, alichokifanya ni sawa na Mkurugenz wa shule kuja kutoa zawadi kwa mwanafunz halafu akaacha kutoa zawadi kwa mwalimu wake.

huyo mama asingelalamika kama mwamba hua anampa zawadi, mimi sijaoa lakini naona kwa wanawake ambao nimewahi date nao wanavyokua na hisia ukiwapa zawadi, anachukulia ume m appreciate sana!

Mwambie jamaa amtoe out mke wake tena huyo mwanae abaki nyumbani,, 😄wakimaliza ampitishe sehem akachague pamba za kutosha na sim kama hana smart foni 😄

kama hana uwezo, bas ampe hata japo kitenge akashone! nimefeel maumiv yake, 😄 na asijimwambafai kisa mwanaume amtake radhi... maisha mafupi haya tujifunze kuenjoy kwa furaha na amani!!
 
Itakuwa kawaza"mimi ninaelea huyu mtoto hajaona umuhimu wa ninachofanya hapa home?" Nayo ni point mkuu
 
Wachape makofi ya visogo hawa jamaa akili ziwarudi😂😂
 
Itakuwa kawaza"mimi ninaelea huyu mtoto hajaona umuhimu wa ninachofanya hapa home?" Nayo ni point mkuu
Kumbuka hii ilikuwa ahadi ya mtoto akifanya vizuri shule, mtoto amekomaa mpaka amefikia lengo la kufanya vizuri na ili kumuonyesha kwamba baba hadanganyi akamnunulia zawadi yake, sasa mama anaioneaje wivu zawadi ya namna hiyo?

Pili Kama mama anadai zawadi kwa kulea familia (kupika, kufua na kuangalia watoto wao) baba anayevuja jasho kuhakikisha kila kitu kipo sawa hapo home atapewa zawadi na nani?

Halafu watoto wakikua, wa kwanza kufaidika ni mama,na slogan ya "nani kama mama" inashika kasi kweli kweli,kama baba haukujiwekeza basi utakufa mapema sana,maana kila ulichofanya inakuwa ni wajibu wako,lakini malezi ya mama hayatazamwi kama wajibu Bali ni hisani isiyomfanowe!
 
Mama mzazi kabisaaa
Basi huyo baba Ajitathmini,mpaka kufikia mama analalamika kwamba hapewi zawadi sio kwamba anaona wivu mwanae akipewa zawadi hapana bali anamkubusha baba kwamba na yeye yupo,inabidi baba amkumbukepo mara moja moja kama anavyofanya kwa mwanae.
Nb:zawadi /hela inanogesha mapenzi
 
Kuna mama wa kizungu alikuwa anazaa watoto, baada ya muda mtoto anafariki katika mazingira yasiyoeleweka. Baada ya miaka kupita, ikagundulika kuwa anawaonea wivu watoto wakipendwa na baba yao, anataka upendo apewe au kuonesha yeye tu, na sio watoto.
 
Sawa,lakini kwanini alalamike mtoto wake akiwa anapewa zawadi? Kwanini hakulalamika siku kadhaa kabla? Halafu swala la malezi si ni la wote wawili?(baba na mama) inakuwaje mama anataka apongezwe kwa kununuliwa zawadi kwa ajili ya kufanya kitu ambacho baba pia anafanya?
Kama baba anatafuta chakula kwa ajili ya familia, na kununua mahitaji mengine yoooote,inakuwaje mama anataka kupongezwa na kupewa zawadi,baba atapewa na nani???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…