Hii comment hawezi kuijibuHuyo mjinga mmoja amekuambia anataka watoto?
Anao uwezo wa kuwalea na yuko tayari kubeba hayo majukumu?
Kuna watu walio tayari kumsaidia kuwalea ikiwa hana huo uwezo kwa sasa??
Ulimpima afya yake ukagundua hana tatizo la kupata watoto?
Mmethibitisha hana mtoto au watoto huko nje ambao hamuwajui?
Daaah Mimi mwenyewe wamenishinda hawa watoto wanafyatua Sio poa,halafu wala Sio shida zao!Hivi unaweza shindana na watoto wa 2000 kwa kufyetua watoto?🤣🤣🤣🤣utafeli
Akaa 😅Mwanaume inatakiwa upate mtoto wa kwanza ukiwa below 25 uwe na kipato usiwe na kipato utajua mwenyewe 😀
Mdogo wangu wa kike Yuko na watoto watatu, mimi kaka yake hata Sina mchumba 🤔
Halafu mkuu inategemea umekulia mazingira Gani.
Mdogo wangu baada ya kukua kidogo kaolewa chap kazaa, wakati kaka yake Niko mtaani sijui hili Wala lile kuhusu wanawake.
Kwahiyo mazingira yanaamua.
unabetia maisha yako kizembe sana watoto ni gharamaMwanaume inatakiwa upate mtoto wa kwanza ukiwa below 25 uwe na kipato usiwe na kipato utajua mwenyewe 😀
Kuzaa sio sifa sana hasa Kwa kipindi kama huwezi hudumia na kuwaandalia maisha mazuri usiongeze mzigo Kwa wenzioYaani mdogo wako anakutangulia kuzaa aisee ni dharau sana
Wazee kuna mjinga mmoja hapa mtaani mdogo wake ana watoto wa 3, yeye hana hata mmoja aisee halafu kampita mdogo wake kwa miaka 5
Huu ni ujinga
Huyo bro ni Mimi, vipi tuzae we dada upo tayariYaani mdogo wako anakutangulia kuzaa aisee ni dharau sana
Wazee kuna mjinga mmoja hapa mtaani mdogo wake ana watoto wa 3, yeye hana hata mmoja aisee halafu kampita mdogo wake kwa miaka 5
Huu ni ujinga
Wewe utakuwa ni mwalinu WA taaluma ahsante Kwa ujumbe boraMpunguze maelekezo kwenye maisha ya watu jamani !! Mambo ya kuzaa , kuolewa na kuoa ni choice za mtu binafsi.
Na nyie mnaozaa na kuoa kwa mkumbo mnashindwa kulea yale yale unakutana na mtoto asubuhi anaenda shule shati ina kifungo kimoja unajiuliza ina maana huyu mzazi weekend nzima hakupata nafasi ya kukagua hata shati ya mtoto ? Mtoto asubuhi mapema mafuta kapaka upande mmoja , nywele zina mchanga wa jana, shingo ina uchafu maana yake mtoto anajiosha kila siku, kitoto kimepauka utasema usiku mmemchimbisha mashimo mtoto.
Au kiatu kimechanika sole ya kiatu yote anaiburuza na ni jumatatu.
Hapa mtakimbilia kusema hali hazifanani tunawajua 😂 jamani ukizaa watoto kumbuka kuwaangalia every inches wale hawakukuandikia barua ya maombi uwazae zilikua ni furaha zako na mihemko, simamia watoto
kuna hali kweli mtoto hata umwangalie vipi atakuchomoka tu wenye watoto hili tunalijua hakuna bingwa wa malezi.
Ila wazazi mmezidi watoto wanatembea ni wachafu , na hawana mahitaji na wazazi wengi msioangalia watoto ndo mnakomaaga watu waolewe na wazae bila kujisikiliza wao "Zaa kila mtoto anakuja na sahani yake" ndo hayo week ijayo vitoto vinafungua shule minywele hiyo , makucha marefu maana yake umemleta mtoto duniani ili umtese.
Wadogo zangu ambao hamjaoa au kuolewa au kuzaa mtu asikupangie chochote kuhusu unavyotakiwa au lini uingie kwenye ndoa au uzae sema na moyo wako kijana /binti angalia hali yako.
Na vyote vikikushinda acha kama huviwezi sio dhambi na sio lazima kuoa au kuolewa au kupata watoto.
Wazazi osheni watoto ni wachafu ni aibu