Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,899
- 10,415
Kwanza kabisa, hakuna mtu anayefanya kazi zake.
Hata ukiwa na biashara yako, utafanya kazi za wateja wako.
Hivyo, na wewe pia umeajiriwa na hao wateja wako.
Tusiangalie mambo kwa tafsiri finyu ya juu juu tu.
Pia, watu wasingekaa ofisini kufanya kazi za watu wengine, hata wewe usingeweza kupost kitu hapa JF kujifaragua.
Kwa sababu JF inaendeshwa na watu wengi tu walioajiriwa wakakaa ofisini kufanya kazi za watu.
🤣 🤣 🤣 🤣 akijibu nitagiLabda nikuulize swali, hussein pamba kali kajiajiri unahisi yeye ni bora na nafuu kuliko Kasimu Majaliwa ambaye kaajiriwa?
Waajiriwa leo mtajieleza sana.🤣 🤣 🤣 🤣 akijibu nitagi
Kwa sisi tuliojiajiri, wewe umekosea kwani watu hutegemeana kwenye haya maisha, haina maana kuajiriwa ni kubaya labda uwe mwalimu wa chekechea, lakini kuna waajiriwa wanakunja pesa ambayo wewe kajiajiri kwenye mpunga miaka kumi bado huwezi kumfikia, tujifunze kuheshimiana na kuvumiliana maisha bila kutegemeana hayajawa maisha labda useme ajira isiyo na maslahi haifai tena ajira za dunia ya tatu au nchi maskini ndio changamoto lakini walikoendelea huko ajira ni bingo tu
Sasa kwanini hao walioajiriwa wakifukuzwa kazi au kustaafu wanaanza kuhaha kujiajiri tena, zile hela walizopata kule kwenye kuajiria hazitoshi au hizi za kuja kujiajiri ndio zitatosha.
Ww unafanya shuhuli gani?Habari za Leo wakuu,
Leo nilikua najaribu kuiuliza akili yangu swali lifutalo.
Hivi inakuwaje mwanadamu mwenye akili timamu anakaa ofisini kuwafanyia watu kazi kwa zaidi ya miaka mitano?
Yaani kwamba mwanadamu unafanya kazi za watu ambazo sio zako.
Yaani hapo ndio najiuliza, wakuu.
Wakuu hebu tujadili hii mada. Inakuwaje unaishi kwa kutumwa kwa miaka mitano?
Ww unafanya shuhuli gani?