Naona kuna notion kwamba kuajiriwa ni jambo baya, hili jambo nalipinga. Kuajiriwa bila maslahi yanayoridhisha ndiyo jambo baya. Hata CEOs wa Apple, Google, Microsoft, Alibaba, Toyota and the list goes on and on nao pia ni waajiriwa na wanakunja pesa ndefu kuliko mkaanga viazi wa Tandahimba aliyejiajiri.
Aidha kujiajiri/ujasiliamali ni kuwa muajiriwa wa wateja wako. Wateja wako ndio mabosi wako. Utatenda vile watakavyo na kucheza mziki wao. Kifupi kukimbia kuajiriwa ni kuacha shughuli zote na kulala tu nyumbani.
Wewe unayepinga kuajiriwa siku ukianza ujasiliamali wako utahitaji hao hao waajiriwa. Kila mtu akiwa na mawazo kama yako sijui mtatoa wapi nguvu kazi.
Cha msingi ni kulipa watumishi maslahi stahiki.