Hivi inakuwaje mwanadamu mwenye akili timamu anakaa ofisini kuwafanyia watu kazi kwa zaidi ya miaka mitano?

Hivi inakuwaje mwanadamu mwenye akili timamu anakaa ofisini kuwafanyia watu kazi kwa zaidi ya miaka mitano?

Habari za Leo wakuu,

Leo nilikua najaribu kuiuliza akili yangu swali lifutalo.

Hivi inakuwaje mwanadamu mwenye akili timamu anakaa ofisini kuwafanyia watu kazi kwa zaidi ya miaka mitano?

Yaani kwamba mwanadamu unafanya kazi za watu ambazo sio zako.

Yaani hapo ndio najiuliza, wakuu.

Wakuu hebu tujadili hii mada. Inakuwaje unaishi kwa kutumwa kwa miaka mitano?

Waajiriwa mlio maofisini hapa mtajibaraguza sana lakini hii mada inawahusu njooni mtolee maelezo huku.

Kwanini mnakaa kwenye ofisi za watu kwa zaidi ya miaka mitano.

Mkistaafu au kutumbuliwa ndio mnaanza kukumbuka shuka la kujiajiri na huku muda wenu wote, nguvu yenu yote na akili yenu yote mmemalizia kwenye ofisi za watu.
Sio kila kazi mtu anafanya ili kulipwa ujira...kazi nyingine zinafanywa kwa sababu ni utumishi. Hebu fikiria ikiwa kila Daktari,Mkunga,Nesi,Mfamasia angeacha kazi akajiajiri nani angetoa huduma ambayo kwa sehemu kubwa ipo katika kuajiriwa. Kuajiriwa sio kitu kibaya kulianza tangu dahari...mafirauni waliwaajiri waebrania bila ujira au kwa ujira wa chakula...bila hawa unaowadharau kwa kuajiriwa wewe hata huduma ya daktari usingeipata
 
Ivi unajifikiriaje kama huyo daktari anatakae kuhudumia maisha yako yote asingekuwepo coz ni ofisi pia?
 
Niko pamoja na mtoa mada, miaka 5 inatosha kuanza Majaribio ya kujiajiri. Vijana tusijitoe Akili, tusifanye Makosa kama ya Wazee wetu, Wengi wao wanakuja Kujiajiri baada ya kustaafu, mwisho wa siku wanakuja kufariki kabla ya walichokianzisha kufanikiwa. Hii ni kwa Faida ya Watoto na Vizazi vyetu. Hatuwezi kuwarithisha watoto wetu Ajira zetu.

Tuangalie wenzetu Mfano Wahindi, Watoto wao hatupishani nao kwenye Interview za Ajira kwa sababu Wazee wao waliwaandalia Watoto wao Mazingira mazuri ya Kujiajiri. Leo hii wapo wanasimamia Makampuni ya Wazazi wao. Hao wanasiasa tunaojilinganisha nao, wengi wao wana Mabiashara makubwa huko Mtaani. Ndo wanamiliki sekta ya Madini, Utalii, Kilimo, Wana Mahoteli, wanamiliki Mabus na Biashara nyenginezo. Wanasiasa wapo kwenye siasa kulinda Biashara zao. Mfano Shigongo, Tayari alikuwa amejiajiri kwa Miaka mingi. Lakini Leo ni Mwanasiasa.
 
Rais tu kaajiriwa na wananchi, sasa mtoa mada sijui unawazaje. Pia si kila mtu anaweza kusimamisha kitu chake na hata akiweza bado atahitaji nguvu kazi ya watu means ataajiri
Kama umeajiri watu basi angalia usiwaumize kwa sababu tu akili yako inakutuma hawa hawajiwezi ndio maana nimewaajiri
tunategemeana
 
Kuna mabloo kibao wanaishi hiyo life style mkuu
Ushwaini huo mzee! Yani napokea 4M halafu mke yupo mkoani huyo jamaa anafurahia uhuru wa manyani tu aidha mke mkorofi unaona bora awepo mbali tu
 
Hivi mtu uliyeajiriwa kwenye ofisi ya mtu unaweza wekaa miguu kwenye meza, unaweza kuamua kuchelewa kazini. Muda wote unaogopa boss wako
Hadi hapa nimejiridhisha kwamba u r too young to argue,huna experience yoyote na kujiajiri au kuajiriwa....if this is the case u'll take time ku achieve your goals once ukijiajiri na kwenda na attitude kama hii...hivi unajua kwamba ajira binafsi ndio ina shida zaidi hasa kwenye swala la muda na kujituma than ajira ya umma? ACHA UTOTO MWAMBIE SHEMEJI YAKO AKUTAFTIE KAZI YA KUFANYA MJINI USISHINDE HOME KULISHA BATA NA SUNGURA TU!
 
Habari za Leo wakuu,

Leo nilikua najaribu kuiuliza akili yangu swali lifutalo.

Hivi inakuwaje mwanadamu mwenye akili timamu anakaa ofisini kuwafanyia watu kazi kwa zaidi ya miaka mitano?

Yaani kwamba mwanadamu unafanya kazi za watu ambazo sio zako.

Yaani hapo ndio najiuliza, wakuu.

Wakuu hebu tujadili hii mada. Inakuwaje unaishi kwa kutumwa kwa miaka mitano?

Waajiriwa mlio maofisini hapa mtajibaraguza sana lakini hii mada inawahusu njooni mtolee maelezo huku.

Kwanini mnakaa kwenye ofisi za watu kwa zaidi ya miaka mitano.

Mkistaafu au kutumbuliwa ndio mnaanza kukumbuka shuka la kujiajiri na huku muda wenu wote, nguvu yenu yote na akili yenu yote mmemalizia kwenye ofisi za watu.
Shule zimefungwa tutasima mengi humu!!! Mkisha kula chai ya rangi na kiporo cha wali maharage payukeni tuuu ila muda ni mwalimu mzuri sana
 
Shule zimefungwa wakisha kula kiporo cha wali maharage hupayuka tuuu hapo anasuburi sembe dagaaa!!!
 
Kwanza kabisa, hakuna mtu anayefanya kazi zake.

Hata ukiwa na biashara yako, utafanya kazi za wateja wako.

Hivyo, na wewe pia umeajiriwa na hao wateja wako.

Tusiangalie mambo kwa tafsiri finyu ya juu juu tu.

Pia, watu wasingekaa ofisini kufanya kazi za watu wengine, hata wewe usingeweza kupost kitu hapa JF kujifaragua.

Kwa sababu JF inaendeshwa na watu wengi tu walioajiriwa wakakaa ofisini kufanya kazi za watu.
Anajifaragua tu JF.....
 
Mungu amesema paradiso kila mtu atakuwa na nyumba yake na atafanya kazi zake mwenyewe na kula matunda yake. Hatajenga mwingine akae, wala hata lima mwingine ale.

Inaonekana Mungu alituumba tuwe free kabisa.
Kwani hapa ilipo JF ndipo paradiso eeee? 🤣
 
Huyu watakua ni vijana waliotoka au bado wako shuleni bado anahisi kila kitu ni rahisi yaani akiona boom imeingia, akala chipsi yai, akanywa na pepsi, akaenda kufanya presentation akifanya na test akiwa anaongea na wenzake wanadanganyana anaona kila kitu rahisi uandishi wake unaonekana bado mchanga kwenye hustle za mtaa
🤣🤣
 
Hata mama nitilie anatumwa na walaji, mfuga kuku anatumwa na wateja wake, President, Mawaziri na wabunge wote wanatumwa na wananchi. Embu tueleze kazi unayofanya wewe hiyo ni ya namna gani, Au unafanyia mbinguni?
🤣
 
Hadi hapa nimejiridhisha kwamba u r too young to argue,huna experience yoyote na kujiajiri au kuajiriwa....if this is the case u'll take time ku achieve your goals once ukijiajiri na kwenda na attitude kama hii...hivi unajua kwamba ajira binafsi ndio ina shida zaidi hasa kwenye swala la muda na kujituma than ajira ya umma? ACHA UTOTO MWAMBIE SHEMEJI YAKO AKUTAFTIE KAZI YA KUFANYA MJINI USISHINDE HOME KULISHA BATA NA SUNGURA TU!
🤣
 
Habari za Leo wakuu,

Leo nilikua najaribu kuiuliza akili yangu swali lifutalo.

Hivi inakuwaje mwanadamu mwenye akili timamu anakaa ofisini kuwafanyia watu kazi kwa zaidi ya miaka mitano?

Yaani kwamba mwanadamu unafanya kazi za watu ambazo sio zako.

Yaani hapo ndio najiuliza, wakuu.

Wakuu hebu tujadili hii mada. Inakuwaje unaishi kwa kutumwa kwa miaka mitano?

Waajiriwa mlio maofisini hapa mtajibaraguza sana lakini hii mada inawahusu njooni mtolee maelezo huku.

Kwanini mnakaa kwenye ofisi za watu kwa zaidi ya miaka mitano.

Mkistaafu au kutumbuliwa ndio mnaanza kukumbuka shuka la kujiajiri na huku muda wenu wote, nguvu yenu yote na akili yenu yote mmemalizia kwenye ofisi za watu.
Ndo hapo sasa unakuta Rais anakaa kwenye ofisi miaka mitano badala akajiajiri
 
Naona kuna notion kwamba kuajiriwa ni jambo baya, hili jambo nalipinga. Kuajiriwa bila maslahi yanayoridhisha ndiyo jambo baya. Hata CEOs wa Apple, Google, Microsoft, Alibaba, Toyota and the list goes on and on nao pia ni waajiriwa na wanakunja pesa ndefu kuliko mkaanga viazi wa Tandahimba aliyejiajiri.

Aidha kujiajiri/ujasiliamali ni kuwa muajiriwa wa wateja wako. Wateja wako ndio mabosi wako. Utatenda vile watakavyo na kucheza mziki wao. Kifupi kukimbia kuajiriwa ni kuacha shughuli zote na kulala tu nyumbani.

Wewe unayepinga kuajiriwa siku ukianza ujasiliamali wako utahitaji hao hao waajiriwa. Kila mtu akiwa na mawazo kama yako sijui mtatoa wapi nguvu kazi.

Cha msingi ni kulipa watumishi maslahi stahiki.

Sure kukwepa ajira ni kuwekeza kwenye miradi inayokupa passive Income yaani umelala home mpunga unaingia we zako Dubai, Vegas na Bahamas mapumziko kila mwaka. Uwekezaji huo unaweza kuwa kwenye shares, Fixed Income securites i.e Bonds, Fixed deposits na Real Estate tofauti na hapo wote jasho linatutoka tu hamna cha bure. We bosi wako mteja na yule mwingine bosi wake big boss.
 
Back
Top Bottom