Swali langu ni je inawezekana ukahama na mita yako ya umeme? Mfano ulipanga chumba cha biashara sehemu na hiyo sehemu hakukuwa na umeme ukafanya michakato TANESCO ukavuta umeme.
Baada ya muda ukajenga chumba chako cha biashara na unataka kuhama hapo ulipopangisha. Je, inawezekana ukawaomba tanesco wakaifungue ile mita na kuja kufungiwa kwenye sehemu yako?
ELIMIKA NA TANESCO
MWONGOZO KUHUSU KUHAMISHA MITA KUTOKA ENEO MOJA KWENDA ENEO JINGINE
Je mteja anaweza kuhamisha mita kutoka eneo moja kwenda eneo lingine?
Jibu la TANESCO
[emoji3578]Mita ni kifaa kinachotumika kupima matumizi ya mteja kadiri ya matumizi yake.
[emoji3578] Mteja halipii wala kununua mita bali analipia gharama halisi ya kufungiwa umeme (Service line connection fee).
[emoji3578]Mita inaendelea kuwa mali ya TANESCO wakati wote mteja anaotumia umeme.
[emoji3578]Mita ya umeme ikiharibika au kupata hitilafu yeyote ambayo haitokani na uzembe au matumizi mabaya ya mteja, TANESCO inabadilisha mita hiyo kwa gharama zake kwa kuwa ni kifaa chake.
[emoji3578] Wajibu wa mteja wa TANESCO unaanzia baada ya mita kuingia ndani ndio maana mteja au fundi (mkandarasi) haruhusiwi kufanya matengenezo yoyote kwenye mita ya TANESCO, wala kuifungua.
[emoji3578] Mita ya umeme ikishafungwa haiwezi kuhamishwa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine isipokuwa ndani ya ploti / kiwanja husika na inafanywa na TANESCO kupitia maombi kwa maandishi ya mteja.
[emoji3578] Unapoona hitilafu yeyote kwenye mita au kifaa chochote cha umeme kuanzia kwenye mita kwenda nje toa taarifa TANESCO mara moja na sisi tutaifanyia kazi bila gharama yeyote.
Toa taarifa kupitia [emoji116]
[emoji3578] TANESCO APP
[emoji3578]Facebook/twitter/tanesco yetu
[emoji3578]Instagram:tanesco_official page
[emoji3578]Tovuti:
www.tanesco.co.tz
[emoji3578] Barua pepe:
Customer.service@tanesco.co.tz
[emoji3578] Huduma kwa wateja
0768 985 100/ 022 219 4400
TANESCO Tunayaangaza Maisha yako