Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Utahama na mita yako endapo tu utapata ruhusa kutoka ofisi ya TANESCO.
Tofauti na hapo huruhusiwi kuhama na mita bila makubaliano ya TANESCO.
Mita ni mali ya TANESCO na ikiharibika unapewa nyingine bure.
Inawezekana, andika barua TANESCO.
Kwa kawaida ile mita ya umeme ni mali ya Tanesco hivyo hata kwenye kuiamisha kwenda kwingine au ukibomoa nyumba na ukataka kujenga tena, lazima kuwajulisha jamaa
Kwa uelewa wangu kama icho kibanda umejenga hapo hapo pembeni ya ulipopanga inawezekana unaandika barua inapewa gharama inahamia jengo jipya,kama eneo tofauti na hapo aiwezekani lipia mita nyingine
Acha shoboSwali langu ni je inawezekana ukahama na mita yako ya umeme? Mfano ulipanga chumba cha biashara sehemu na hiyo sehemu hakukuwa na umeme ukafanya michakato TANESCO ukavuta umeme.
Baada ya muda ukajenga chumba chako cha biashara na unataka kuhama hapo ulipopangisha. Je, inawezekana ukawaomba tanesco wakaifungue ile mita na kuja kufungiwa kwenye sehemu yako?
Hapana mkuu ni sehemu nyingine kabisa sio hapo
Shobo gani tena jamaa yanguAcha shobo
Mita haihamishiki kwa sababu za kiusalama wa mapato, pia mteja hajalipia wala kununua mita ile ni mali ya TANESCO hivyo ukihama unaiacha pale pale kwa kuwa sio mali ya mteja.Kuhusu gharama zimepungua sana kutoa hapo awaliNi upumbavu mtupu,,, wanajua tunakozitoa pesa! Sheria za kijinga hizi,,, mkuu, ingependeza serikali ikaruhusu upinzani kama vile Mitandao ya simu kunakuwa na ushindani. Sasa hawa jamaa viburi, wanafanya wanavyotaka kwa kujua hakuna mpinzani.
mama samia aliangalie kwa undani swala hili, na bei ya kuwekewa umeme ishuke.
TANESCO , kaka njoo huku utoe maelezo! Kwanini kuhamisha mita haiwezekani?
Na bei za kuunganishiwa ni very expensive!!!!
Mita haihamishiki kwa sababu za kiusalama wa mapato, pia mteja hajalipia wala kununua mita ile ni mali ya TANESCO hivyo ukihama unaiacha pale pale kwa kuwa sio mali ya mteja.Kuhusu gharama zimepungua sana kutoa hapo awali
Kama upo ndani ya mita 30 ni Tsh 321000 kwa mijini na vijijini ni Tsh 27000 tuKwa singo fesi mijini, na umeme wa nyaya 3 viwandani bei ikoje kwa sasa mkuu? Hali ni mbaya, hela hamna mtuhurumie jamani.
Nikihama naruhusiwa kuhama na nguzo na nyaya za service line nilizolipia?
Sasa mbona mnazipa usajili wa majina ya mteja?ELIMIKA NA TANESCO
MWONGOZO KUHUSU KUHAMISHA MITA KUTOKA ENEO MOJA KWENDA ENEO JINGINE
Je mteja anaweza kuhamisha mita kutoka eneo moja kwenda eneo lingine?
Jibu la TANESCO
[emoji3578]Mita ni kifaa kinachotumika kupima matumizi ya mteja kadiri ya matumizi yake.
[emoji3578] Mteja halipii wala kununua mita bali analipia gharama halisi ya kufungiwa umeme (Service line connection fee).
[emoji3578]Mita inaendelea kuwa mali ya TANESCO wakati wote mteja anaotumia umeme.
[emoji3578]Mita ya umeme ikiharibika au kupata hitilafu yeyote ambayo haitokani na uzembe au matumizi mabaya ya mteja, TANESCO inabadilisha mita hiyo kwa gharama zake kwa kuwa ni kifaa chake.
[emoji3578] Wajibu wa mteja wa TANESCO unaanzia baada ya mita kuingia ndani ndio maana mteja au fundi (mkandarasi) haruhusiwi kufanya matengenezo yoyote kwenye mita ya TANESCO, wala kuifungua.
[emoji3578] Mita ya umeme ikishafungwa haiwezi kuhamishwa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine isipokuwa ndani ya ploti / kiwanja husika na inafanywa na TANESCO kupitia maombi kwa maandishi ya mteja.
[emoji3578] Unapoona hitilafu yeyote kwenye mita au kifaa chochote cha umeme kuanzia kwenye mita kwenda nje toa taarifa TANESCO mara moja na sisi tutaifanyia kazi bila gharama yeyote.
Toa taarifa kupitia [emoji116]
[emoji3578] TANESCO APP
[emoji3578]Facebook/twitter/tanesco yetu
[emoji3578]Instagram:tanesco_official page
[emoji3578]Tovuti: www.tanesco.co.tz
[emoji3578] Barua pepe: Customer.service@tanesco.co.tz
[emoji3578] Huduma kwa wateja
0768 985 100/ 022 219 4400
TANESCO Tunayaangaza Maisha yako
Kama upo ndani ya mita 30 ni Tsh 321000 kwa mijini na vijijini ni Tsh 27000 tu
Zipo, kwa sababu watafanya survey na utapewa gharama japo zitakuwa ndogo...Endapo umeandika barua, na mwisho wa siku wakakuhamishia mita yao kwenda sehemu nyingine, je! Watakutoza upya au kuna gharama nyingine?
Sasa mbona mnazipa usajili wa majina ya mteja?
Kwa nini asihame nayo kwa kutoa taarifa kwenu..muifungue mmpatiea.. anapoenda tanesco waifunge.
Ama lah ile mita number iendelee kuwa configured na device mpya.
Kuna watu wanahitaji kumentain kumbukumbu zao.
Mkuu kinachoniumiza zaidi ni, bei ya kuvutiwa umeme iko juu sana, na pia ukihitaji kuhamishiwa mita kutoka sehemu husika kwenda sehemu nyingine kwa umbali hata wa kilometer 1 haiwezekani why!!!! kwa sisi ambao uwezo wetu mdogo inakuwa ngumu. Mtu umegharamika kufuatilia wakufungie mita na ukalipia gharama za kuvutiwa mwisho wa siku unahitaji kuhamishiwa eti haiwezekani, ina maana utakapohamia ulipie upya gharama/ada ya kuvutiwa umeme. Inauma inauma sana.
Tutaendelea kutoa elimu eneo hiliSasa mbona mnazipa usajili wa majina ya mteja?
Kwa nini asihame nayo kwa kutoa taarifa kwenu..muifungue mmpatiea.. anapoenda tanesco waifunge.
Ama lah ile mita number iendelee kuwa configured na device mpya.
Kuna watu wanahitaji kumentain kumbukumbu zao.
Anahitaji jibu la 3 phase vijijini na mijiniKama upo ndani ya mita 30 ni Tsh 321000 kwa mijini na vijijini ni Tsh 27000 tu
Zipo, kwa sababu watafanya survey na utapewa gharama japo zitakuwa ndogo...
Mathalani utapohamia, kuna kitu kama waya wa kutoka kwenye nguzo hadi bracket kama hilo jengo halina umeme kabisa