Hivi inawezekana ukahama na mita yako ya umeme?

Utahama na mita yako endapo tu utapata ruhusa kutoka ofisi ya TANESCO.

Tofauti na hapo huruhusiwi kuhama na mita bila makubaliano ya TANESCO.

Mita ni mali ya TANESCO na ikiharibika unapewa nyingine bure.

Sasa, kama ni mali ya tanesco/bure ile pesa ya kuwekewa umeme tsh 321,000 ni ya nini?
 
Inawezekana, andika barua TANESCO.

Kwa kawaida ile mita ya umeme ni mali ya Tanesco hivyo hata kwenye kuiamisha kwenda kwingine au ukibomoa nyumba na ukataka kujenga tena, lazima kuwajulisha jamaa

Endapo umeandika barua, na mwisho wa siku wakakuhamishia mita yao kwenda sehemu nyingine, je! Watakutoza upya au kuna gharama nyingine?
 
Kwa uelewa wangu kama icho kibanda umejenga hapo hapo pembeni ya ulipopanga inawezekana unaandika barua inapewa gharama inahamia jengo jipya,kama eneo tofauti na hapo aiwezekani lipia mita nyingine

Ni upumbavu mtupu,,, wanajua tunakozitoa pesa! Sheria za kijinga hizi,,, mkuu, ingependeza serikali ikaruhusu upinzani kama vile Mitandao ya simu kunakuwa na ushindani. Sasa hawa jamaa viburi, wanafanya wanavyotaka kwa kujua hakuna mpinzani.
mama samia aliangalie kwa undani swala hili, na bei ya kuwekewa umeme ishuke.

TANESCO , kaka njoo huku utoe maelezo! Kwanini kuhamisha mita haiwezekani?
Na bei za kuunganishiwa ni very expensive!!!!
 
Acha shobo
 
Mita haihamishiki kwa sababu za kiusalama wa mapato, pia mteja hajalipia wala kununua mita ile ni mali ya TANESCO hivyo ukihama unaiacha pale pale kwa kuwa sio mali ya mteja.Kuhusu gharama zimepungua sana kutoa hapo awali
 
Kwa singo fesi mijini, na umeme wa nyaya 3 viwandani bei ikoje kwa sasa mkuu? Hali ni mbaya, hela hamna mtuhurumie jamani.
 
Inawezekana kabisa,,
Hiyo mita ni mpya au ya zamani??[emoji2959]
 
Kwa singo fesi mijini, na umeme wa nyaya 3 viwandani bei ikoje kwa sasa mkuu? Hali ni mbaya, hela hamna mtuhurumie jamani.
Kama upo ndani ya mita 30 ni Tsh 321000 kwa mijini na vijijini ni Tsh 27000 tu
 
Sasa mbona mnazipa usajili wa majina ya mteja?

Kwa nini asihame nayo kwa kutoa taarifa kwenu..muifungue mmpatiea.. anapoenda tanesco waifunge.

Ama lah ile mita number iendelee kuwa configured na device mpya.

Kuna watu wanahitaji kumentain kumbukumbu zao.
 
Kama upo ndani ya mita 30 ni Tsh 321000 kwa mijini na vijijini ni Tsh 27000 tu

Bei ni ile ile haijapungua kitu,nilifikiri itakua chini ya lakitatu

Kama ninataka kufungua kamradi mjini mnachaji bei gani kunivutia umeme wa 3fase?
 
Endapo umeandika barua, na mwisho wa siku wakakuhamishia mita yao kwenda sehemu nyingine, je! Watakutoza upya au kuna gharama nyingine?
Zipo, kwa sababu watafanya survey na utapewa gharama japo zitakuwa ndogo...

Mathalani utapohamia, kuna kitu kama waya wa kutoka kwenye nguzo hadi bracket kama hilo jengo halina umeme kabisa
 
Mkuu kinachoniumiza zaidi ni, bei ya kuvutiwa umeme iko juu sana, na pia ukihitaji kuhamishiwa mita kutoka sehemu husika kwenda sehemu nyingine kwa umbali hata wa kilometer 1 haiwezekani why!!!! kwa sisi ambao uwezo wetu mdogo inakuwa ngumu. Mtu umegharamika kufuatilia wakufungie mita na ukalipia gharama za kuvutiwa mwisho wa siku unahitaji kuhamishiwa eti haiwezekani, ina maana utakapohamia ulipie upya gharama/ada ya kuvutiwa umeme. Inauma inauma sana.
 
Ndiyo lazima ulipe upya! Sababu hapa ni za kitaalam zaidi kuliko kibiashara! Ungekuwa mtaalam wa Electrical technology ungejua kwa nini huo ugumu upo.
 
Tutaendelea kutoa elimu eneo hili
 
Zipo, kwa sababu watafanya survey na utapewa gharama japo zitakuwa ndogo...

Mathalani utapohamia, kuna kitu kama waya wa kutoka kwenye nguzo hadi bracket kama hilo jengo halina umeme kabisa

Okay, kingine naomba kujua chief. Napotaka kuunganishiwa umeme wa 3phase au single phase, je! Mbali na ada hiyo nitakayowapa ya kuvutiwa umeme, je! kuna baazi ya vifaa nitatakiwa kuvinunua kwa hela yangu ili wanivutie umeme?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…