Hivi inawezekana ukahama na mita yako ya umeme?

Hapana haujazilipia hizo bali ulilipua ada ya kuunganishiwa umeme. Hii inadhirishwa na kiasi ulicholipia mfano 27000 kwa vijijini au 177000 kwa mijini

177,000/=
Kama upo ndani ya mita 30 ni Tsh 321000 kwa mijini na vijijini ni Tsh 27000 tu

Hapa umesema 321,000/=

Sijui tuelewe lipi mkuu, mnatuchanganya kwakweli.
 
Naomba mnifahamishe gharama za kufungiwa mita ya Luku ktk kibanda changu cha biashara
 
Mita haihamishiki kwa sababu za kiusalama wa mapato, pia mteja hajalipia wala kununua mita ile ni mali ya TANESCO hivyo ukihama unaiacha pale pale kwa kuwa sio mali ya mteja.Kuhusu gharama zimepungua sana kutoa hapo awali
Kwa hii sheria yenu naona kama zimepitwa na wakati
Kwa sasa ni wakati wa kiruhusu mita mtu aweze kuhama nayo maana nyumba moja utakuta ina wapangaji 20 na kila mtu ana mita binafsi kulingana na matumizi yake sasa unapofika muda wa kuhama anaiacha na harudi TANESCO kuripoti mita inabaki kwa mwenye nyumba tuu ilhal mngeruhusu kuhama nayo mngekuwa pia mnaongeza mapato kwani iendako itakuwa bado inatumika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…