Hivi inawezekanaje mtu mmoja kama Rostam kuweza kuwapita akili na ku-outsmart viongozi

Hivi inawezekanaje mtu mmoja kama Rostam kuweza kuwapita akili na ku-outsmart viongozi wetu wakubwa, wanasiasa, wakurugenzi, mameneja wa mashirika makubwa ya umma na hata vyombo vya ulinzi na usalama? Swali hili linaacha mshangao mkubwa.

Je, ni kwa sababu yeye ni genius, au kuna udhaifu mkubwa kwenye mifumo yetu?

Tumeona mara nyingi kwa sasa Polepole akimlenga Rostam kama chanzo cha ufisadi wa muda mrefu nchini. Ameeleza kwa undani jinsi jina lake linavyohusishwa na vigogo wakubwa serikalini, na kwa namna ya kushangaza, historia hii inarudi nyuma tangu mwaka 2005 hadi leo. Rostam ni tycoon, mtu mwenye nguvu kubwa kwenye anga za uchumi na siasa, na ukiunganisha nukta za maelezo ya Polepole, unaweza kuona kuna ukweli kwa kiwango kikubwa.

Lakini maswali amaboyo najiuliza:

Huyu mtu anapata wapi muda wa kufanya “deals” zote hizi kubwa zinazohusisha mabilioni ya fedha? Amewezaje mara kwa mara kuwapiga chenga marais na mawaziri wetu? Na zile pesa zote nyingi ambazo amekuwa akizipata kwa miaka yote hii zinakwenda wapi? Je, ni kweli anapiga hela hizi kwa faida binafsi tu, au kuna mtandao mkubwa zaidi unaofaidika nyuma yake je huu mtandao unatoka nchi gani hasa?

Cha kushangaza zaidi, kuhusu maisha yake binafsi hatuna taarifa nyingi. Hata familia yake haijulikani waziwazi, hujawahi kusikia habari za mke au watoto wake. Ni kana kwamba maisha yake binafsi yamefunikwa kwa makusudi ili kuendelea kumfanya aonekane ni mtu “untouchable”.

Na pia, kwa nini kila awamu jina ni lilelile? Kwa nini mara zote ni Rostam? Wapo mabilionea wengine wakubwa kama Mo Dewji, Bakheresa na wengine ambao hawajawahi kutajwa mara kwa mara kwenye skendo kubwa za kisiasa na kiuchumi. Kwa nini ni yeye peke yake anayejitokeza kila mara?

Mwisho wa yote, swali langu kubwa lipo kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama:

Hivi mnashindwa vipi kudhibiti mtu mmoja anayeonekana kila mara kuwavuruga viongozi wetu wakuu? Inakuwaje mtu mmoja anachafua taswira ya viongozi, hadi hata pale ambapo kiongozi mpya akiingia madarakani kwa matumaini na mapenzi ya wananchi, baada ya muda mfupi taswira yake inaharibika kwa sababu ya kushirikiana au kuhusishwa na huyu bwana?

Wananchi wa kawaida, ambao hatuna ushabiki wa kisiasa, tunabaki na maswali mazito. Vyombo vya ulinzi na usalama mnafanya kazi kwa maslahi ya nani? Ni kwa ajili ya wananchi na taifa kwa ujumla, au kwa maslahi ya mtu mmoja na mtandao wake? Kwa sasa, badala ya kuwa kimbilio la usalama na amani, vyombo hivi vimeanza kuonekana kama sehemu ya kuongeza taharuki.

Hii inaleta hofu kubwa kwa mustakabali wa nchi na vizazi vijavyo.
Ogopa mtu anayeikashifu judicial system yetu, halafu wanakaa kimya tu bila kumjibu. Si Waziri, si Mwanasheria wa serikali, si Jaji mkuu, wote kimya.
 
Nadhani mahakama ilitoa tamko aombe radhi.
 
KATAA WAHUNI, OKOA TANGANYIKA.✍️📌
 
Nadhani mahakama ilitoa tamko aombe radhi.
Mmh! Ilichukua muda gani kuomba radhi? Ningekuwa mimi kapuku nimeisema mahakama hivyo ningeambiwa niombe radhi? Kwanza ku dare kuzungumza hivyo dhidi ya mahakama, angestahili kuchukuliwa hatua za kisheria. No wonder mama aliyekutwa na kilo ngapi sikumbuki za nyama ya swala aliishia kufungwa miaka mingi, ingawaje alitolewa baada ya kelele nyingi lakini mdogo wake Rostam hata baada ya kukutwa na nyara za serikali kibao na bunduki za kuwindia zaidi ya dozen aliishia kupigwa faini.
 
Sio kwamba ana wa outsmart ila anatumia “money” ku influence mipango yake

Ukiwa mgumu wanapitia kwa mke, mtoto wako. Sasa ukionekana wewe kichwa ngumu sana, bora uwapishe tu. Na ukisha ingia kwenye huo mtego huwezi toka maana umesha chafuka. Sasa unaelekezwa kwa remote.
 
Hivi inawezekanaje mtu mmoja kama Rostam kuweza kuwapita akili na ku-outsmart viongozi wetu wakubwa, wanasiasa, wakurugenzi, mameneja wa mashirika makubwa ya umma na hata vyombo vya ulinzi na usalama? Swali hili linaacha mshangao mkubwa.

Je, ni kwa sababu yeye ni genius, au kuna udhaifu mkubwa kwenye mifumo yetu?

Tumeona mara nyingi kwa sasa Polepole akimlenga Rostam kama chanzo cha ufisadi wa muda mrefu nchini. Ameeleza kwa undani jinsi jina lake linavyohusishwa na vigogo wakubwa serikalini, na kwa namna ya kushangaza, historia hii inarudi nyuma tangu mwaka 2005 hadi leo. Rostam ni tycoon, mtu mwenye nguvu kubwa kwenye anga za uchumi na siasa, na ukiunganisha nukta za maelezo ya Polepole, unaweza kuona kuna ukweli kwa kiwango kikubwa.

Lakini maswali amaboyo najiuliza:

Huyu mtu anapata wapi muda wa kufanya “deals” zote hizi kubwa zinazohusisha mabilioni ya fedha? Amewezaje mara kwa mara kuwapiga chenga marais na mawaziri wetu? Na zile pesa zote nyingi ambazo amekuwa akizipata kwa miaka yote hii zinakwenda wapi? Je, ni kweli anapiga hela hizi kwa faida binafsi tu, au kuna mtandao mkubwa zaidi unaofaidika nyuma yake je huu mtandao unatoka nchi gani hasa?

Cha kushangaza zaidi, kuhusu maisha yake binafsi hatuna taarifa nyingi. Hata familia yake haijulikani waziwazi, hujawahi kusikia habari za mke au watoto wake. Ni kana kwamba maisha yake binafsi yamefunikwa kwa makusudi ili kuendelea kumfanya aonekane ni mtu “untouchable”.

Na pia, kwa nini kila awamu jina ni lilelile? Kwa nini mara zote ni Rostam? Wapo mabilionea wengine wakubwa kama Mo Dewji, Bakheresa na wengine ambao hawajawahi kutajwa mara kwa mara kwenye skendo kubwa za kisiasa na kiuchumi. Kwa nini ni yeye peke yake anayejitokeza kila mara?

Mwisho wa yote, swali langu kubwa lipo kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama:

Hivi mnashindwa vipi kudhibiti mtu mmoja anayeonekana kila mara kuwavuruga viongozi wetu wakuu? Inakuwaje mtu mmoja anachafua taswira ya viongozi, hadi hata pale ambapo kiongozi mpya akiingia madarakani kwa matumaini na mapenzi ya wananchi, baada ya muda mfupi taswira yake inaharibika kwa sababu ya kushirikiana au kuhusishwa na huyu bwana?

Wananchi wa kawaida, ambao hatuna ushabiki wa kisiasa, tunabaki na maswali mazito. Vyombo vya ulinzi na usalama mnafanya kazi kwa maslahi ya nani? Ni kwa ajili ya wananchi na taifa kwa ujumla, au kwa maslahi ya mtu mmoja na mtandao wake? Kwa sasa, badala ya kuwa kimbilio la usalama na amani, vyombo hivi vimeanza kuonekana kama sehemu ya kuongeza taharuki.

Hii inaleta hofu kubwa kwa mustakabali wa nchi na vizazi vijavyo.
Nikisikia hivyo naumia,baada ya kukumbuka mwalimu Nyerere alivyomshikilia yule mgiriki,baada yakuserikali yote kaitia mfukoni!? Enzi hizo😂😂😂,kwa kweli Mwalimu alikua jasiri sana 😂😭😭😭
 
Kwa sababu ndiko wanapowekeza hela
Wanamuamini kuwa hawadhulumu
Wewe nikupe Elfu kumi tu mkopo unabadili na njia

Ndio maana hamuaminiani na kumpa huyu jamaa awake kwenye miradi yake
Nimewaza tu maana mnajua tena sisi ni kuongea tu Yaani kamdomo 😂😂😂
 
Jibu ni moja tu KATIBA MBOVU,pamoja na uvundo mwingi uliopo kwenye katiba lakini siku katiba ikisema rais ashtakiwe basi nidhamu itakuwepo pia kusiwe na mhimili uliojichimbia chini kuliko mingine maana hapo kila mhimili utakuwa unaheshimu na kuuogopa mwingine,tofauti na sasa unaona kabisa mihimili miwili iliyobaki ni kama upumbavu unacheza maigizo ya futuhi
 
Yaani bunge na mahakama ni kama sehemu au ofisi za serikali kuu..
Binafsi nilipokuwa mdogo nilipata shida sana kwenye civics nilipoambiwa hiyo ni mihimili inayojitegemea hadi leo nikiangalia nchi yetu naona si kweli.
 
Hivi inawezekanaje mtu mmoja kama Rostam kuweza kuwapita akili na ku-outsmart viongozi wetu wakubwa, wanasiasa, wakurugenzi, mameneja wa mashirika makubwa ya umma na hata vyombo vya ulinzi na usalama? Swali hili linaacha mshangao mkubwa.

Je, ni kwa sababu yeye ni genius, au kuna udhaifu mkubwa kwenye mifumo yetu?

Tumeona mara nyingi kwa sasa Polepole akimlenga Rostam kama chanzo cha ufisadi wa muda mrefu nchini. Ameeleza kwa undani jinsi jina lake linavyohusishwa na vigogo wakubwa serikalini, na kwa namna ya kushangaza, historia hii inarudi nyuma tangu mwaka 2005 hadi leo. Rostam ni tycoon, mtu mwenye nguvu kubwa kwenye anga za uchumi na siasa, na ukiunganisha nukta za maelezo ya Polepole, unaweza kuona kuna ukweli kwa kiwango kikubwa.

Lakini maswali amaboyo najiuliza:

Huyu mtu anapata wapi muda wa kufanya “deals” zote hizi kubwa zinazohusisha mabilioni ya fedha? Amewezaje mara kwa mara kuwapiga chenga marais na mawaziri wetu? Na zile pesa zote nyingi ambazo amekuwa akizipata kwa miaka yote hii zinakwenda wapi? Je, ni kweli anapiga hela hizi kwa faida binafsi tu, au kuna mtandao mkubwa zaidi unaofaidika nyuma yake je huu mtandao unatoka nchi gani hasa?

Cha kushangaza zaidi, kuhusu maisha yake binafsi hatuna taarifa nyingi. Hata familia yake haijulikani waziwazi, hujawahi kusikia habari za mke au watoto wake. Ni kana kwamba maisha yake binafsi yamefunikwa kwa makusudi ili kuendelea kumfanya aonekane ni mtu “untouchable”.

Na pia, kwa nini kila awamu jina ni lilelile? Kwa nini mara zote ni Rostam? Wapo mabilionea wengine wakubwa kama Mo Dewji, Bakheresa na wengine ambao hawajawahi kutajwa mara kwa mara kwenye skendo kubwa za kisiasa na kiuchumi. Kwa nini ni yeye peke yake anayejitokeza kila mara?

Mwisho wa yote, swali langu kubwa lipo kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama:

Hivi mnashindwa vipi kudhibiti mtu mmoja anayeonekana kila mara kuwavuruga viongozi wetu wakuu? Inakuwaje mtu mmoja anachafua taswira ya viongozi, hadi hata pale ambapo kiongozi mpya akiingia madarakani kwa matumaini na mapenzi ya wananchi, baada ya muda mfupi taswira yake inaharibika kwa sababu ya kushirikiana au kuhusishwa na huyu bwana?

Wananchi wa kawaida, ambao hatuna ushabiki wa kisiasa, tunabaki na maswali mazito. Vyombo vya ulinzi na usalama mnafanya kazi kwa maslahi ya nani? Ni kwa ajili ya wananchi na taifa kwa ujumla, au kwa maslahi ya mtu mmoja na mtandao wake? Kwa sasa, badala ya kuwa kimbilio la usalama na amani, vyombo hivi vimeanza kuonekana kama sehemu ya kuongeza taharuki.

Hii inaleta hofu kubwa kwa mustakabali wa nchi na vizazi vijavyo.

WEWE HUMJUI ROSTAM. ROSTAM ANA PESA SANA . ROSTA ANA PESA NJIWA HARUKI. ANA NGUVU KULIKO RAIS AU MKUU WA MAJESHI. HUJUI TU NYAMAZA.
 
Alitembea na usemi maarufu wa Vito Corleone wa kwenye hadithi ya kimafia ya The Godfather aliousema nanukuu.." I'm gonna make him an offer he can't refuse"... yeah .. alitumia udhaifu wa vibopa wa ccm ya tamaa na ulafi wa pesa kama fursa ya kujipenyeza hadi kwenye "meza kuu"..
 
Access to resources and capital.... tafuta hela, wanasiasa watakuabudu tu.

Hiyo ni principle ya dunia nzima.
 
Hivi inawezekanaje mtu mmoja kama Rostam kuweza kuwapita akili na ku-outsmart viongozi wetu wakubwa, wanasiasa, wakurugenzi, mameneja wa mashirika makubwa ya umma na hata vyombo vya ulinzi na usalama? Swali hili linaacha mshangao mkubwa.

Je, ni kwa sababu yeye ni genius, au kuna udhaifu mkubwa kwenye mifumo yetu?

Tumeona mara nyingi kwa sasa Polepole akimlenga Rostam kama chanzo cha ufisadi wa muda mrefu nchini. Ameeleza kwa undani jinsi jina lake linavyohusishwa na vigogo wakubwa serikalini, na kwa namna ya kushangaza, historia hii inarudi nyuma tangu mwaka 2005 hadi leo. Rostam ni tycoon, mtu mwenye nguvu kubwa kwenye anga za uchumi na siasa, na ukiunganisha nukta za maelezo ya Polepole, unaweza kuona kuna ukweli kwa kiwango kikubwa.

Lakini maswali amaboyo najiuliza:

Huyu mtu anapata wapi muda wa kufanya “deals” zote hizi kubwa zinazohusisha mabilioni ya fedha? Amewezaje mara kwa mara kuwapiga chenga marais na mawaziri wetu? Na zile pesa zote nyingi ambazo amekuwa akizipata kwa miaka yote hii zinakwenda wapi? Je, ni kweli anapiga hela hizi kwa faida binafsi tu, au kuna mtandao mkubwa zaidi unaofaidika nyuma yake je huu mtandao unatoka nchi gani hasa?

Cha kushangaza zaidi, kuhusu maisha yake binafsi hatuna taarifa nyingi. Hata familia yake haijulikani waziwazi, hujawahi kusikia habari za mke au watoto wake. Ni kana kwamba maisha yake binafsi yamefunikwa kwa makusudi ili kuendelea kumfanya aonekane ni mtu “untouchable”.

Na pia, kwa nini kila awamu jina ni lilelile? Kwa nini mara zote ni Rostam? Wapo mabilionea wengine wakubwa kama Mo Dewji, Bakheresa na wengine ambao hawajawahi kutajwa mara kwa mara kwenye skendo kubwa za kisiasa na kiuchumi. Kwa nini ni yeye peke yake anayejitokeza kila mara?

Mwisho wa yote, swali langu kubwa lipo kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama:

Hivi mnashindwa vipi kudhibiti mtu mmoja anayeonekana kila mara kuwavuruga viongozi wetu wakuu? Inakuwaje mtu mmoja anachafua taswira ya viongozi, hadi hata pale ambapo kiongozi mpya akiingia madarakani kwa matumaini na mapenzi ya wananchi, baada ya muda mfupi taswira yake inaharibika kwa sababu ya kushirikiana au kuhusishwa na huyu bwana?

Wananchi wa kawaida, ambao hatuna ushabiki wa kisiasa, tunabaki na maswali mazito. Vyombo vya ulinzi na usalama mnafanya kazi kwa maslahi ya nani? Ni kwa ajili ya wananchi na taifa kwa ujumla, au kwa maslahi ya mtu mmoja na mtandao wake? Kwa sasa, badala ya kuwa kimbilio la usalama na amani, vyombo hivi vimeanza kuonekana kama sehemu ya kuongeza taharuki.

Hii inaleta hofu kubwa kwa mustakabali wa nchi na vizazi vijavyo.
Ni taasisi hiyo.
 
Back
Top Bottom