Hivi jua huwa likizama linatua wapi?

[emoji16][emoji16][emoji16]ndo mana lisipo waka siku hiyo linakuwa limechafuka si eti

Yaani, watu hawajui tu sayansi ilivyo mamiiii ila sayansi ina siri kubwa sana mwaya.

Tuko pamoja mamitto. Lol.
 
Aisee uko darasa la ngapi?hii ni jografia ya darasa la tano mkuu.
Kuna mwingine juzi kauliza eti kama dunia inazunguka mbona hatumwagiki?sijui walimu wa siku hizi hawana zana za kufundishia!!...au wanafunzi wenyewe ndiyo wale 500 wa mh Mnyeti![emoji135]
 
Mkuu nimesema dunia kujizungusha kwenye muhimili wake ndo tunapata usiku na mchana.
Dunia ina mizunguko miwili.Wa Kwanza Dunia kujizungusha kwenye mhimili wake.Na wa pili kulizunguka jua.

Usiku na mchana ni matokeo ya dunia kujizungusha kwenye mhimili wake.Jua liko palepale
 

ivo ndo ulivo funzwa huko skuli za private kuwasaidia watu? elimu yako yenye mapana ndo inavo kufundisha kumsaidia mtu au kujibu shinda-basi bora iyo elmu ya kata mara mia kuliko iyo yako isio na usaidifu
 
Jua halitui ila2 linapigiwa misele na dunia lenyewe limetulia
 
Habari wakuu,


Tunajua usiku na mchana hupatikana kwa dunia kujizungusha kwenye muhimili wake.

Katika kitu cha kujiuliza ni wapi jua linapotua, je lenyewe halisimami?

Najua mtabeza.


Ila toeni maoni yenu.
Imamu alituambia linazama kwenye matope
 
Mm huwa nawashangaa sanaa humu JF mtu ameuliza swali hata kama ni la kipumbavu ww kama una uelewa mjibu sio kumkejeli sio watu wote tumesoma labda mm nilivyo maliza darasa la saba sikuendele mbele nilienda kusomea mapishi sasa mambo ta jua nitayajua wapi. Hata wenzetu waliosoma kama yeye ni Dr wa maneno huwa ni meno tuu ukimletea tatizo la sikio hawezi kukutibu. Tuwe tunasaidiana kuongezana maarifa elimu sio darasani peke yake.
 
Hiyo ni dhana iloletwa na mlevi tu
 
Litatuaje wakati limesimikwa sehemu moja milele na milele? Sisi na shida zetu tunaishia tu kulizunguka ili angalau kupata uzima .Kumbuka jua ni maisha.
 
sishangai sana sababu siku hizi hata watoto wa darasa la pili wanamiliki simu janja na wana acc. Jf
 
Jua huwa halitui, huo ni msemo kulingana na mwonekano tu. Pia huwa tunatumia msemo "jua limezama" haimaanishi limezama baharini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…