Haya maisha haya acha tu....
Wakati wa utotoni, jirani yetu ambaye mtoto wake tulikuwa tunacheza nae mpira barabarani miaka ile ya 80s, maeneo ya Upanga maana kulikuwa kuwa kumetulia sana hata mpira mnacheza barabarani.
Sasa kuna kipindi ile familia nzima shule zilivyofungwa maana alikuwa anasoma Olympio, miaka ile na hata haikuwa ya gharama maana ilikuwa bado chini ya Halmashauri na tunafunga likizo pamoja na st kayumba...
Walienda kutembelea kwa mpigo nchi zifuatazo , Germany, France Belgium na UK, yaani hio ndio ilikuwa likizo yake, mpaka leo nakumbuka baada ya kuwa mtu mzima ndio najua yule mdingi kweli alikuwa sio wa kawaida.
Rafiki yetu akarudi na kutuletea tupipi na maisha yakaendelea huku tukicheza nae mpira wa kufuma na nylon.....
Wala hata hatukuliona ni jambo la ajabu,
Ni kwa sasa ndio nashangaa sana mpaka leo, kila nikikumbuKa