Hivi Kariakoo ni kweli kuna Fremu za 3M-5M au ni kutishana tu?

Hivi Kariakoo ni kweli kuna Fremu za 3M-5M au ni kutishana tu?

Pantomath

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2019
Posts
842
Reaction score
3,449
Mtaani tumezoea kodi ya fremu kuanzia 50k-200k, kutokana na eneo.

Kwa taarifa ninazopata ni kuwa fremu K.koo si chini ya 1M, oky hio sikatai kutokana na eneo lenyewe. Vipi hawa wanaosema ni 3M-5Millions.

Je, hii ni kweli? Mtu huyu ana mauzo ya namna gani?

Ikumbukwe hapa nazungumzia fremu za bidhaa ndogo ndogo kama simu, nguo n.k ambapo unakuta ukubwa wa chumba ni almost 8×10ft.

1624949477034.png
 
Enzi za JK Frame za mjini including Kariakoo zilikuwa hazikamatiki lakini kutokana na biashara nyingi kufa inawezekana bei ikawa imeshuka! Kwa mfano, mwaka 2019 National Housing walitangaza spaces za biashara zilizokuwa wazi across Dar es salaam. Kiukweli iliniuma sana manake kulikuwa na mamia ya unoccupied spaces. Picha niliyokuwa nimepata ni kwamba biashara nyingi zilikufa kwa sababu zamani haikuwa rahisi kuzipata.
 
Mtaani tumezoea kodi ya fremu kuanzia 50k-200k, kutokana na eneo..

Kwa taarifa ninazopata ni kua fremu k.koo si chini ya 1M, oky hio sikatai kutokana na eneo lenyewe,
Vipi hawa wanaosema ni 3M-5Millions,
Jee hii ni kweli? Mtu huyu anamauzo ya namna gani?
Ikumbukwe hapa nazungumzia fremu za bidhaa ndogo ndogo kama simu, nguo n.k ambapo unakuta ukubwa wa chumba ni almost 8×10ft.
Ukiwasikiliza wabongo hautajenga, hautaanzisha biashara, hautaoa yaani kila kitu kwako utaona kigumu tu tusubiri wenye ujuzi na Kkoo
 
Nina classmate wangu ambaye ni marafiki sanaa,

Baba yao alijenga mjengo wa kupangisha biashara k.koo,
Alishafariki, yule jamaa ile family yao/watoto kila katikati ya mwezi wana uhakika wa 5M..

No wonder aliacha shule, watu wakasema sana ikiwemo walimu anachezea maisha, ila njemba mpaka leo ni bata tuu na hakuna mazingira ya hizo laana kumpata.

Kuna wazee waliwekeza,
Wengine bahati mbaya walipambana ila mambo tuu hayakua upande wao BIG up kwao pia.

Achana na wale waliokua wamelala asaivi wanaong'ang'ania ukali kumbe stress za njaa na madeni, kwa kupenda kufoka mpaka koo limekauka,

Unakuta mzee muda wote anaongea kama kapaliwa na ukoko,
Kidogo tuu anatishia laana, Bahati nzuri hazishiki, wangemaliza watu bila sababu, Anaweza aage anaenda kutafuta kumbe anawaachia msala wa madeni,
 
Hakuna frame kkoo inayozidi 3m kwa sasa nyingi zinacheza 5-1.5m, napo inadepend na location au mtaaa mfano kwa Kariakoo mitaa kama ya Congo, Swahili, Mafia, Livingstone, Uhuru, Msimbazi na Gerezani bei zake zimechangamkaa sana, kuna mitaa Kariakoo frame zipo chini pia inategemea na mtaa.
 
Wakuu fremu bado ni ngumu kupata sehemu iliyochangamka asikudanganye mtu hasa Kwa DSM, Mbezi stand ya daladala Tu kupata Tu Banda la kukodi ni tena ndani humo kwenye vibanda ni 200k tena la kiboya Tu, Goba pale center mpaka 500k sembuse Kariakoo.... Kariakoo mtu kukwachia Tu fremu si chini ya 35mil wanaita kumvua kilemba ....
 
ulivyo malizia uko chini nimecheka sana

Ukali siku zote ni stress, unakuta mzee hataki kabisa kuguswa[emoji3][emoji3]
Ukali ni stress mzee hasa za njaa, hakuna cha nini wala nini....
Ndio maana kila siku hukosi kusikia baba amjeruhi/amuua mtoto kwa kuiba tsh 1200.

Mara nyingi wazee wanaosifika kwa vipogo ni wenye njaa.
 
Wakuu fremu bado ni ngumu kupata sehemu iliyochangamka asikudanganye mtu , hasa Kwa DSM , mbezi stand ya daladala Tu kupata Tu Banda la kukodi ni tena ndani humo kwenye vibanda ni 200k tena la kiboya Tu , goba pale center mpak 500k sembuse kariakoo.... Kariakoo mtu kukwachia Tu fremu si chini ya 35mil wanaita kumvua kilemba ....
Unamaanisha kuinunua kabisa?
 
Unamaanisha kuinunua kabisa?
Kuinunua tena 😀 jamaa anakuachia anaondoka na vitu vyake unabaki na frem tupu ndo hyo unampa mil 35 tena na Zaid kulingana na location .... Hapo unaanza kuelewana na mwenye frem sasa kuhusu Kodi na dalali hapo anahitaji chake , TRA nao ndani bila kusahau halmashauri , mlinzi n.k 🤪🤪🤣🤣
 
Kuinunua tena 😀 jamaa anakuachia anaondoka na vitu vyake unabaki na frem tupu ndo hyo unampa mil 35 tena na Zaid kulingana na location .... Hapo unaanza kuelewana na mwenye frem sasa kuhusu Kodi na dalali hapo anahitaji chake , TRA nao ndani bila kusahau halmashauri , mlinzi n.k 🤪🤪🤣🤣
Khaaaaaa.

Kuniachia kale kachumba nikupe 35M?

Halafu nianze tena kodi? Mimi kama nimekufuata ukanitajia hivyo naweza nikucheke mpk nianguke.
 
Hakuna frame kkoo inayozidi 3m kwa sasa nyingi zinacheza 5-1.5m, napo inadepend na location au mtaaa mfano kwa kariakoo mitaa kama ya congo, swahili, mafia, livingstone, uhuru, msimbazi na gerezani bei zake zmechangamkaa sana kuna mitaa kariakoo frame zipo chini pia inategemea na mtaaa
Biashara zipo mitandaoni siku hizi.
 
Back
Top Bottom