The same thng ilinikuta mkuu, nilikuwa na biashara zangu nafanya nimefungua library ya movie pia nauza viatu, biashara ikawa nzuri hadi nikapanga chumba na sebure boonge la nyumba ndani ya geti. Mambo yakawa hovyo nikafunga biashara ya viatu kwny library napo nikapandishiwa kodi mara 3 yake na umeme juu. Ikabidi nifunge ofisi, ugumu wa maisha nikauza computer ili nijaribu zari kwngne, mwenye nyumba naye akanijia juu kisa kodi imepungua elfu 10 tu nikatimuliwa. Niliamua kumsafirisha wife na watoto kwao nikapanga kisirisiri kachumba kamoja kamatope na giza cha 10,000 mtaa wa pili nikawa nahama usiku usiku ili majirani wasinione. Mara ghafla nashtukia gari linakuja kasi na kupiga breki kali karibu yangu, "ndio hayahaya tunayoyatafuta, litakuwa jizi hili hebu lipakie kwenye difenda" afande mmoja aliropoka kwa sauti akimwamrisha mwenzake, huyo mwenzake akaja kasi na kunizoa.. Wee niligoma nikamwambia mi nahama hivi ni vitu vyangu, wakataka niwapeleke nnapotoa vitu nikawapeleka walipo ridhika wakaondoka.