FYATU
JF-Expert Member
- Dec 7, 2011
- 5,567
- 4,683
Wahenga Wenzangu wanaweza kukumbuka vizuri taarifa mbalimbali tulizokuwa tukizisikia kumuhusu Idd Amin Dada.Kuna baadhi ambazo nani nilifanikiwa kuzisikia kama vile kusomba Walemavu ombaomba wote pale Kampala na kwenda kuwamwaga ziwa Victoria ili jiji libaki safi,kuwepo kwa vichwa vya Watu aliohitilafiana nao na kuwaua na kuviweka kwenye friji ikulu,pia tuliambiwa kwamba alimuua Mwanae wa kiume baada ya Mtoto huyo kuonesha dalili za kutamani mdaraka ya Baba yake.Yapo mengi na sidhani kama nilifanikiwa kuyasikia yote.Na kwa muda wote huu sijawahi kukutana na taarifa rasmi ya kukanushwa hayo.Sasa je ni kweli aliyatenda hayo yote?Je yeye mwenyewe alijua kinachoendelea na kupuuzia tu akiwa ukimbizini Saudi Arabia? Au Je hakukuwa na Watu waliotamani kukanusha walau kwa yale aliyosingiziwa?Hakika maswali ni mengi kuliko majibu.