Hivi kila kilichoandikwa au kusemwa kuhusu Idd Amin kilikuwa cha kweli?

Hivi kila kilichoandikwa au kusemwa kuhusu Idd Amin kilikuwa cha kweli?


 
Wahenga Wenzangu wanaweza kukumbuka vizuri taarifa mbalimbali tulizokuwa tukizisikia kumuhusu Idd Amin Dada.Kuna baadhi ambazo nani nilifanikiwa kuzisikia kama vile kusomba Walemavu ombaomba wote pale Kampala na kwenda kuwamwaga ziwa Victoria ili jiji libaki safi,kuwepo kwa vichwa vya Watu aliohitilafiana nao na kuwaua na kuviweka kwenye friji ikulu,pia tuliambiwa kwamba alimuua Mwanae wa kiume baada ya Mtoto huyo kuonesha dalili za kutamani mdaraka ya Baba yake.Yapo mengi na sidhani kama nilifanikiwa kuyasikia yote.Na kwa muda wote huu sijawahi kukutana na taarifa rasmi ya kukanushwa hayo.Sasa je ni kweli aliyatenda hayo yote?Je yeye mwenyewe alijua kinachoendelea na kupuuzia tu akiwa ukimbizini Saudi Arabia? Au Je hakukuwa na Watu waliotamani kukanusha walau kwa yale aliyosingiziwa?Hakika maswali ni mengi kuliko majibu.
Ukitaka kumfukuza ama kumuua mbwa mchagulie kwanza majina yote mabaya, kisha nenda kafanye kweli.
 
Tuseme yote yalikuwa ya uongo je, Nduli alitaka sehemu ya TZ? Je, alisapoti utekaji ndege ya Air France iliyokuwa imebeba waisrael kwenda Paris na badala yake ikaenda Libya na kisha Uganda? Kama alifanya yeyote kati ya hayo alistahili kichapo. Alikuwa dictator na mpenda sifa na tunajua hulka za watu wa aina hiyo. Alistahili kila kitu kilichompata.
Point yangu ni kuwa Idd Amin kweli alivuka mpaka kwenye maeneo mengi lakini je ni yote yanayosemwa alifanya?Tukiweka mbali yale ambayo ni ya kuinekana wazi kama la Ndege kushikiliwa Entebe,kuivamia Kagera n.k kama hayo ya kula moto wa Binaadamu tana ukweli au ni Watu walijiongeza?.
 
Ukitaka kumfukuza ama kumuua mbwa mchagulie kwanza majina yote mabaya, kisha nenda kafanye kweli.
Ila pia tujiulize kwani taarifa zote kama hizo kumuhusu Amin zilitoka Tanzania au zilizotoka kwa Waganda wenyewe?
 
Ni uhakika Iddi Amin alikuwa mwendawazimu
 
Hii

Hii nilikutana nayo kwenye documentary moja, aliulizwa na Mwanahabari akacheka sana na kukiri kuwa ni kweli anataka aje Dar aonane na Mwalimu wazichape.
Mkuu dictator yeyote huwa na mabaya yake na mazuri yake mengi tu. Lakini kamwe mazuri yake huwa hayaandikwi.
Rejesha madai ya kumuondoa Gadafi madarakani waliona mabaya machache tu kama sio moja la kukaa madarakani muda mrefu lakini kwa sasa wanalia
 
Back
Top Bottom