Pre GE2025 Hivi kile kijiwe cha kahawa cha wanawake alichokunywa Rais Samia kilienda wapi?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Nimefika hapa Soko la Wamachinga parking Nzega nikataka kujionea kijiwe cha Kahawa cha wanawake ambacho Rais Samia alionekana akinywa kahawa maana nimezunguka mikoa mingi sijawahi kuona kijiwe cha wanawake, nikataka angalau nikawaunge mkono Wanawake hao ila sijafanikiwa kukiona.

Nimeuliza wenyeji hapa nao wanashangaa uwepo wa kijiwe hicho cha kahawa cha wanawake, nikasogea hadi vijiwe vilivyo vya wanaume nikawauliza iwapo wanajua wauza kahawa wenzao ambao ni wanawake walipo wakanishangaa wakasema hakuna na hawajawahi kuwaona.


Samia akiwa Soko la Wamachinga parking, Nzega, Tabora​

Pia soma:Mmeshawahi kuona kijiwe cha wanywa kahawa wanawake?
 
Unachokitafuta utakipata. Nadhani ungeanza na wale waliokuwa wanamuuzia mwendazake mapapai, samaki na mahindi ya kuchoma kabla ya hiki kijiwe cha kahawa cha juzi kwa Madam.

Mwendazake aliwahi kujongea vijiwe vya kahawa pia.

Sidhani kama ni halisi, ni vya kutengeneza tu kwa ajili ya mahusiano ya Rais na jamii.
 
Ila uwezekano wa wanawake kupata muda wa kukaa kijiweni kunywa kahawa mbona naona kama ni mdogo sana ?
 

πŸ˜€
Mtanikumbuka
 
Wakili wangu hayupo nchini πŸ™ŒπŸΏπŸ™ŒπŸΏπŸ™ŒπŸΏπŸƒπŸΏπŸƒπŸΏπŸƒπŸΏπŸƒπŸΏ
 
Naona MTU wa kitengo hapo nyuma anahakiki huyo mwenye shati la kijani πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
Mwenye shati la kijani ni kiongozi wa Kijiji wa nyuma yake anasaa mikononi ni wakitengo. Mbele ya mwalimu pia ni wa kitengo
 
Ile ilikuwa script
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…