Pre GE2025 Hivi kile kijiwe cha kahawa cha wanawake alichokunywa Rais Samia kilienda wapi?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hivi ndivyo watanzania wanapenda kuona. nakumbuka mbunge wa jimbo langu alikuwa anapendwa kisa akija anaenda kunywa kahawa na watu na kupiga nao picha na kuwaachia laki wagawane.

Aliyefuata akajaribu kuanzisha mikopo ya riba nafuu, kujenga soko na miradi kibao. Akageuka kuwa adui wa wananchi hasa waliochukua mikopo wakagoma kurudisha wakakamatwa maana raia walikuwa wanaambizana tuchukue mikopo tu hailipwi.

Akawa adui ya wale ambao walikosa mikopo, mwisho akapigwa chini. Watanzania wao wanataka mtu awe mbunge akanywe nao kahawa au apande bodaboda kama mama salma siku moja basi utasikia yule mtu wa watu.
 
Nadhani wanafanya makusudi kwa sababu za kiusalama Ila Tu director awe makini na script
 
Hii ni kama yule muuza madafu, hawa watu inshort huwa wanapangwa, refer enzi za JPM alikuwa anakula mahindi njiani ,,,,unafikiri kalagabaho mchambia gunzi atoke tu huko aje achome mahindi amuuzie rais ale ? Hata vile vijiwe vya kahawa chato walikuwa ni watu wa system wanapangwa tu , wanaandaa tukio,,,,,
Hii inasaidia kuonekana kwamba raisi ni jamii na anashirikiana nao
 
Mtoa mada ameuliza kijiwe cha kahawa cha wanawake na bibi chaudele wewe unaleta tena habari za mwendazake πŸ€”πŸ€”
 
Shida kubwa ni kua hawana waandaaji wazuri wa maigizo yao ndio maana ni rahisi hata kwa mtoto wa chekechea kuwagundua
 
Wakili wangu hayupo nchini πŸ™ŒπŸΏπŸ™ŒπŸΏπŸ™ŒπŸΏπŸƒπŸΏπŸƒπŸΏπŸƒπŸΏπŸƒπŸΏ
Nakutegemea wewe kama wakili wangu lakiniπŸ™‚
 
Wangekiita tuu kijiwe cha uji cha kina mama....kuliko haya maigizo yasio na muongozaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…