Hivi kile kitendo cha Daktari kumfumua Mgonjwa nyuzi kina tofauti gani na pale Madaktari wanapoamua kugoma?

Hivi kile kitendo cha Daktari kumfumua Mgonjwa nyuzi kina tofauti gani na pale Madaktari wanapoamua kugoma?

May Day

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
6,311
Reaction score
9,027
Kwanza nami nalaani alichokifanya yule Bw Dokta.

Baada ya lile tukio nimesikia matamko mbalimbali ya kulaani ambapo miongoni wao ni Madaktari wenzake....na nadhani hata bado kuna mchakato wa kumuadhibu kwa kukiuka maadili.

Baadae nikakumbuka ya kuwa kuna wakati Madaktari huamua kugoma, na hapo nchi jirani walitoka kugoma muda si mrefu.

Sasa nimejiuliza kama Madaktari wameungana na kulaani hili, ni nini huwakuta na kukubaliana wengi wao kama sio wote kugoma wakijua kabisa kuna Wagonjwa wanapata matatizo zaidi au hata kupoteza maisha?.

Kwa kuwa sijamsikia Daktari yeyote akijaribu kukaa upande wa Dokta yule, hivyo tusitarajie kusikia wameitisha mgomo?.
 
migomo ya watumishi wa umma liishia awamu ya nne huko.

kuanzia awamu ya 4 na hii ya 5,goma ukimaliza,ukatafute na kazi ya kufanya.
 
Huyo atakuwa ni Tabibu mtu aliyesoma Udaktari hawezi kumfumua mgonjwa
 
Usichanganye Madesa...! Kuna Jambo hapo limevuka mipaka ya Ubinadamu...! Ndo maana Wote wameungana Kulaani Kitendo Kiovu.
 
Hii inanikumbusha a pound of flesh kule Venice na Yule Merchant.... (A Merchant of Venice)

Huyo Daktari ni kweli alikuwa na haki ya kuondoa nyuzi zake sababu jamaa hajalipia..., Ila sidhani kama alikuwa na haki ya kumpatia jamaa maumivu mara mbili ya kushonwa na kunyofolewa....

Hivyo basi Dokta achukue nyuzi zake na alipwe muda wake alioupoteza na jamaa amkabidhi maumivu Dokta aliyomsababishia...

Anyway na huyu jamaa hakujua kwamba anahitaji kulipa ? Au amesahau tupo njiani kuelekea Kwenye Ubepari ? (Aende Marekani aone jinsi watu wasio na Bima Dokta anawaangalia tu na kuwapita)
 
Pesa ya tozo kazi yake nini sasa kama mgonjwa anafumuliwa nyuzi......si walisema zimepelekwa kujenga vituo vya afya na huyu mgonjwa aliyeng'ofolewa nyuzi ni miongoni mwa wachangiaji wa tozo, au kuna maana nyingine ya solidarity fund.....
 
Aibu sana kwa huyo jamaa.....

Sidhani kama amekishika kiapo cha "DO NOT DO HARM"......

Tabibu gani "nnya" kiasi hicho?!!! Khaaa 😲😲😲

SHAME TO HIM

#YetzerHaTov
#SiempreJMT
#NchiKwanza
#KaziIendelee
 
Kwanza nami nalaani alichokifanya yule Bw Dokta.

Baada ya lile tukio nimesikia matamko mbalimbali ya kulaani ambapo miongoni wao ni Madaktari wenzake....na nadhani hata bado kuna mchakato wa kumuadhibu kwa kukiuka maadili.

Baadae nikakumbuka ya kuwa kuna wakati Madaktari huamua kugoma, na hapo nchi jirani walitoka kugoma muda si mrefu.

Sasa nimejiuliza kama Madaktari wameungana na kulaani hili, ni nini huwakuta na kukubaliana wengi wao kama sio wote kugoma wakijua kabisa kuna Wagonjwa wanapata matatizo zaidi au hata kupoteza maisha?.

Kwa kuwa sijamsikia Daktari yeyote akijaribu kukaa upande wa Dokta yule, hivyo tusitarajie kusikia wameitisha mgomo?.
Tofauti ni kubwa sana. Yote si matendo ya kiungwana, ila kitendo cha mganga huyu ni unyama.
 
Back
Top Bottom