Hivi kile kizazi cha watumwa waliokuwa wanachukuliwa na waarabu kutoka Tanganyika kiliishia katika taifa/mataifa yapi?

Hivi kile kizazi cha watumwa waliokuwa wanachukuliwa na waarabu kutoka Tanganyika kiliishia katika taifa/mataifa yapi?

Leo tunaona 13% ya population ya Marekani ikiwa ni ya watu weusi wengi wao kwa asilimia maradufu ni kizazi cha watumwa waliochukuliwa kutoka west africa.

Hivi wale waliokuwa wanatekwa wakina abushiri walipelekwa wapi na mark yao leo iko wapi.

Au walichukuliwa kwa uchache na kusambazwa maeneo tofauti ya waarabu?

Au walifutwa kama vile walivyofutwa wa pale argentina?
Waliouzwa UARABUNI walihasiwa...pia walitumika kama kifaa cha burudani kwa kuingiliwa kinyume cha maumbile na waarab......walahi walikuwa wanabashiwa...
 
Leo tunaona 13% ya population ya Marekani ikiwa ni ya watu weusi wengi wao kwa asilimia maradufu ni kizazi cha watumwa waliochukuliwa kutoka west africa.

Hivi wale waliokuwa wanatekwa wakina abushiri walipelekwa wapi na mark yao leo iko wapi.

Au walichukuliwa kwa uchache na kusambazwa maeneo tofauti ya waarabu?

Au walifutwa kama vile walivyofutwa wa pale argentina?
Unataka ukawatafute?
 
Nafikiri waliwauza kwa wazungu wengi wao.

Na kidogo wakapelekwa uarabuni

Nimekaa nchi za kiarabu nyingi na nimewaona watu weusi na hata Viongozi wakubwa na hata kwenye majeshi wamo wengi tena wenye vyeo vikubwa sana mpaka marubani nimewaona

Nimefanya nao kazi
Ila nilikuja kushangaa nilipokutana na Mpalestina mweusi
Utajuaje hawa ni weusi waliokuja miaka ya karibuni, mfano miaka ya 1950s, mpaka sasa, au waliokuja tangu enzi za utumwa?

Katika ma Prince wa Saudi Arabia, kuna Prince Bandar. Mama yake ni Muethiopia, anaonekana mweusi yuko tofauti na ma Prince wengine.

Nilikuwa nafikiri labda huyu Prince Bandar ni sehemu ya masalia ya watumwa, kumbe huyu mama yake alikuwa mfanyakazi wa ndani jumba la Mfalme, katoka Ethiopia, Prince akaruka naye akazaa mtoto, ndiyo huyo Prince Bandar.
 
Uarabuni wapo watu weusi wengi tu, na kuna jimbo moja kule Iran ni la watu weusi na wanafahamika kabisa uzao wao ulitokea East Africa. Ni sawa sio wengi kama US lakini wapo , kwa sababu waarabu walikua wakiifanya hio biashara ya utumwa kwa kuwauzia wazungu, hivyo walioenda uarabuni hawakua wengi kama walioenda America ya kaskazini na kusini.
Mkuu,

Iran si Uarabuni lakini. WaIran si Waarabu.
 
Waliobahatika kwenda Uarabuni walikuwa wanahasiwa , kwa hiyo kulikuwa hamna kuzaliana ni kupiga kazi tu

====

East Africa's forgotten slave trade​

Over several centuries countless East Africans were sold as slaves by Muslim Arabs to the Middle East and other places via the Sahara desert and Indian Ocean. Experts say it is time for this to be discussed more openly.

Back then, Arab Muslims in North and East Africa sold captured Africans to the Middle East. There, they worked as field workers, teachers or harem guards, which is why the castration of male slaves was common practice.

====

The Caliphate in Baghdad at the beginning of the 10th Century had 7,000 black eunuchs and 4,000 white eunuchs in his palace." The Arab slave trade typically dealt in the sale of castrated male slaves. Black boys at the age of eight to twelve had their p..... and scr...... completely amputated.

Reportedly, about two out of three boys died, but those who survived drew high prices. However, according to Islamic law and Muslim jurists castration of slaves was deemed unlawful.

Watumwa ktk harakati za kuwatetea mabwana zenu.

Hii vita ya watetezi wa bwana mwarabu na bwana beberu wa uzunguni, ngumu kuisha maana Kila mtu anamtetea bwana wake

Kiufupi tu ni hivi, huyo mwarabu na hao wazungu wote ni mashetani ambao walifanya biashara haramu dhidi ya utu wa MTU mweusi.

Kibaya zaidi mwarabu ndie kawaharibu makondoo wake kiakili yamekuwa mazuzu, majinga hayaoni ukweli.

Yapo makondoo hata huko Zanzibar ambako Kuna ushahidi wa ukatili wa mwarabu ambako ndiko lilikuwa chimbo na soko la mawinga wa kuuza/kununua watu mchana kweupe, ushahidi upo lkn hayo majitu yamerogwa akili yanadai kuwa bwana wao mwarabu hakuuza watu weusi Bali kasingiziwa tu kwa chuki za mzungu.

Kitu kibaya ambacho bwana mwarabu alikitenda kumzidi bwana mzungu, ni kuwarithisha makondoo wake dini ya kitapeli ambayo inautukuza uzazi wa uarabu kulingana na stories za kipuuzi za hiyo dini ya bwana muarabu(uislamu), dini ambayo makondoo(wafia dini weusi) wanaitetea kuliko hata kuutetea uhalisia wao na jamii za weusi wenzao.

Watu weupe wote ni washenzi kwa hili mutambue ukweli, hakuna mwenye unafuu.
 
Afadhali hata wamarekani tunawaona waafrika huko ila hawa waarabu sijui waliwapeleka wapi waafrika, maana hatuwaoni katika mataifa yao, tuone hata machotara tu
Watu weusi wapo nchi zote za kiarabu ila sio sana kuoneshwa, mfano India kuna wale wahindi weusi wa south. Hawa sio sana kuwaona kama wale wahindi wa north, pia India kuna weusi kama sisi wa Tanzania. Hawa mpaka ufatilie mwenyewe ndio utajua ila wao kuwaonesha hawafanyi hivyo kabisa.

Mexico,Peru,Guantamala,Venezuela au Caribbean wale wote wanatokea Afrika. Jamaica,Japan na Australia pia wapo hata Egypt na Yemen wapo weusi wengi sana tu lakini media huchagua watakacho wao.

Ni sawa na history ya Tanzania utaijua ile ya shule lakini ipo ya wenyeji ipo tofauti na ya shule.
 
Nafikiri waliwauza kwa wazungu wengi wao.

Na kidogo wakapelekwa uarabuni

Nimekaa nchi za kiarabu nyingi na nimewaona watu weusi na hata Viongozi wakubwa na hata kwenye majeshi wamo wengi tena wenye vyeo vikubwa sana mpaka marubani nimewaona

Nimefanya nao kazi
Ila nilikuja kushangaa nilipokutana na Mpalestina mweusi
Watu weusi kupitia muziki, siasa na michezo mingine tunawaona.
Ila mnawavyowapamba waarabu utafikiri hakuna Zanzibar revolution
Ulifanya kazi Uarabuni halafu unajiita Black Sniper kwanini usingetumia jina la kiaarabu? Hiyo ni ishara tosha waarabu siyo watu wema.
Mnagoogle picha halafu mnaweka. Ni bora nikaishi kwa wazungu kuliko kwa waarabu.
 
Watu weusi wapo nchi zote za kiarabu ila sio sana kuoneshwa, mfano India kuna wale wahindi weusi wa south. Hawa sio sana kuwaona kama wale wahindi wa north, pia India kuna weusi kama sisi wa Tanzania. Hawa mpaka ufatilie mwenyewe ndio utajua ila wao kuwaonesha hawafanyi hivyo kabisa.

Mexico,Peru,Guantamala,Venezuela au Caribbean wale wote wanatokea Afrika. Jamaica,Japan na Australia pia wapo hata Egypt na Yemen wapo weusi wengi sana tu lakini media huchagua watakacho wao.

Ni sawa na history ya Tanzania utaijua ile ya shule lakini ipo ya wenyeji ipo tofauti na ya shule.
Mbona nchi za wazungu weusi wako huru sana? Tunawaona kwenye mpira, muziki na shughuli zingine.
Barack Obama, 50 Cent, lil wayne, movies km zote nk. Ufaransa ndiyo wapo wengi sana.
Waarabu kutoka Syria walikuwa wanakufa majini wakienda nchi za ulaya
 
Waarabu walikuwa ni wauza bidhaa na wazungu walikuwa ninwanunua bidhaa kwa ajili ya Cheap labour
Utawadanganya ambao wanatumia kiaarabu cha maarabu kumuomba mungu wa kiarabu.
Waarabu na wazungu walifanya biashara za watumwa. Zanzibar revolution ilihusu nini? Waarabu wangekuwa wema wangekuwepo mpk leo Zanzibar
 
Utajuaje hawa ni weusi waliokuja miaka ya karibuni, mfano miaka ya 1950s, mpaka sasa, au waliokuja tangu enzi za utumwa?

Katika ma Prince wa Saudi Arabia, kuna Prince Bandar. Mama yake ni Muethiopia, anaonekana mweusi yuko tofauti na ma Prince wengine.

Nilikuwa nafikiri labda huyu Prince Bandar ni sehemu ya masalia ya watumwa, kumbe huyu mama yake alikuwa mfanyakazi wa ndani jumba la Mfalme, katoka Ethiopia, Prince akaruka naye akazaa mtoto, ndiyo huyo Prince Bandar.
Ni kweli kila binadamu ana historia yake na wale wa asili ya utumwa wanajulikana pia
Kwa kuwa nimekaa sana ME kwenye nchi hizo kuna moja kwa mfano Kuwait hii nchi ni ndogo sana na wakati huo kulikuwa na population ya watu million moja tu wakiwemo expatriates 250 000
Sasa kulikuwa na Crown prince Sheikh Saad Al Salim Al Sabah huyu alikuwa ni mweusi na baba mwarabu ila baba yake alioa kijakazi wao (mtumwa) na mwisho mwanae huyu Saad akaja kuwa mfalme au Amir kama wanavyoitwa Q8
Na niwajua weusi wengi ambao wanasema wao asili yao ni Africa na ni zao la utumwa
Kwa hiyo wapo wengi ila kesi kama hiyo ya Bandar zinatokea pia ila sio nyingi
Nimewaona mpaka stateless weusi
Hawa baada ya Kuwait na Saudia au iraq kupatikana mafuta hawa walikuwa wanaishi au wakiwa watumwa desert wakichunga ngamia na mbuzi
Waarabu walipopata mafuta wakaanza kubaguana na kusema nyie sio wa kabila hili au sio wa nchi hii
Wakiwemo weusi pia
Nilikuwa nataniana nao na kuwaambia mimi ni mwafrika OG sasa nyie mnahesabika kama nani? Wanasema sisi ndugu zako
 
Watu weusi kupitia muziki, siasa na michezo mingine tunawaona.
Ila mnawavyowapamba waarabu utafikiri hakuna Zanzibar revolution
Ulifanya kazi Uarabuni halafu unajiita Black Sniper kwanini usingetumia jina la kiaarabu? Hiyo ni ishara tosha waarabu siyo watu wema.
Mnagoogle picha halafu mnaweka. Ni bora nikaishi kwa wazungu kuliko kwa waarabu.
Hapa tunaongelea vitu ninavyojua wala sina mda wa ku google kwa sababu ni shuhuda na nimeishi kote Uarabuni na Ulaya na Africa pia
Pia hata wewe unaweza kuwa John au Peter lakini haikufanyi uwe mzungu bali mwafrika tu
Hapa tunajadili tu wala hakuna udini wala ukabila
Na kiukweli sielewi kabisa una maana gani kwa kuandika haya
Siwatetei waarabu wala waafrika bali nimeandika ninachojua
Nimejaza passports 4 kwa mihuri ya nchi kibao kwa hiyo ninajua ninachoandika
 
Kuna uzi ulianzishwa jana tu leo mwengine.

Kifupi mkuu sehemu pekee watu weusi waliofanikiwa ni Uarabuni, ndio sehemu pekee utakuta scientist wakubwa, Maprofessor na madokta vyuoni, maEngineer na watu wengine wenye heshima.

Afro Arabs sio masikini ama waganga njaa kama weusi wengine wanaopatikana mataifa mbalimbali Duniani.

Hii comment yangu nilipost jana nacopy na ku paste hapa.

1. Mtu mweusi Tajiri Duniani huwa wanapokezana Baina ya Dangote na Al Amoud Bilionea Wa Saudia, Hakuna Mweusi yoyote Ulaya ama Usa anaegusa kwa Al Amoud
View attachment 3195316

2. Kuna Viongozi Kibao wenye Asili ya Africa ama ambao wame changanya kama Marehemu Qabous wa Oman pamoja na Baba yake, Mfalme wa Zamani wa Kuwait etc hii picha ya Lineage ya Sabah Familia ya viongozi wa Kuwait
View attachment 3195329
View attachment 3195330

3. Ukiangalia makampuni makubwa Makubwa ya Saudia na Arabuni kwa Ujumla utawakuta hao Black Arabs wakiwa na positions kubwa kubwa kama MA CEO, MA Engineer wakubwa, Madaktari etc kifupi kazi zinazohitaji akili.

-Ahmad Hawsawi CEO wa Siemens Saudia
View attachment 3195331

-Abdulelah AlHawsawi
Founder wa Saudi Patient safety centre kama Colaborate centre ya Who (Zipo 5 tu dunia nzima) na ni member wa WHO kwenye same field, pia anakuwa hadi Chairman vikao vingi vya WHO
View attachment 3195336

-Ingia website yoyote inayolist research papers na wanasayansi eka ukoo wowote wa watu weusi Wa Saudia kama huo wa Hawsawi angalia Contribution zao

Hakuna popote Pale Duniani utapata Viongozi wazuri weusi tofauti na Nchi za kiarabu, hakuna popote Duniani utapata watu weusi wasomi tofauti na Nchi za kiarabu hakuna popote pale Duniani utapata watu weusi Wenye Hela tofauti NA nchi za kiarabu huo ni ukweli mchungu ambao wengi hawataki kukubali.
Al Amoud ni Muethiopia, mzaliwa Ethiopia, kasoma Ethiopia na Mhamara kwa asili.
Huyu mtu ni muafrika halisi ila kapata uraia wa Saudia by Tajinisi.
Sio zao la watumwa na Wala hakuna mtumwa katika vizazi vyake vya nyuma.
Huo uarabu mnaomfungamanisha kautolea wapi?
 
Ni kweli kila binadamu ana historia yake na wale wa asili ya utumwa wanajulikana pia
Kwa kuwa nimekaa sana ME kwenye nchi hizo kuna moja kwa mfano Kuwait hii nchi ni ndogo sana na wakati huo kulikuwa na population ya watu million moja tu wakiwemo expatriates 250 000
Sasa kulikuwa na Crown prince Sheikh Saad Al Salim Al Sabah huyu alikuwa ni mweusi na baba mwarabu ila baba yake alioa kijakazi wao (mtumwa) na mwisho mwanae huyu Saad akaja kuwa mfalme au Amir kama wanavyoitwa Q8
Na niwajua weusi wengi ambao wanasema wao asili yao ni Africa na ni zao la utumwa
Kwa hiyo wapo wengi ila kesi kama hiyo ya Bandar zinatokea pia ila sio nyingi
Nimewaona mpaka stateless weusi
Hawa baada ya Kuwait na Saudia au iraq kupatikana mafuta hawa walikuwa wanaishi au wakiwa watumwa desert wakichunga ngamia na mbuzi
Waarabu walipopata mafuta wakaanza kubaguana na kusema nyie sio wa kabila hili au sio wa nchi hii
Wakiwemo weusi pia
Nilikuwa nataniana nao na kuwaambia mimi ni mwafrika OG sasa nyie mnahesabika kama nani? Wanasema sisi ndugu zako
Dah, noma sana.

Hao stateless kuna documentary moja nilikuwa naangalia wanaelezea hivyo hivyo ulivyosema.

Niliwaonea huruma sana.
 
Al Amoud ni Muethiopia, mzaliwa Ethiopia, kasoma Ethiopia na Mhamara kwa asili.
Huyu mtu ni muafrika halisi ila kapata uraia wa Saudia by Tajinisi.
Sio zao la watumwa na Wala hakuna mtumwa katika vizazi vyake vya nyuma.
Huo uarabu mnaomfungamanisha kautolea wapi?
Logic hapa ni Kwamba Usa kuna 13% watu weusi na Middle East hakuna, kitu ambacho sio sahihi, hata Usa hao 13% sio wote ni zao la Watumwa. Mfano Obama mzazi wake nae alitoka Kenya, lakini utaona anatumiwa humu kwenye mbadala.

Saudia kuna koo za watu weusi kama Al Dosary, Hawsawi, bishi na Jizani, Takriban asilimia 10 ya wasaudia ni watu weusi.

Wengi nimewataja humo Ni Hawsawi ambao asili yao ni Nigeria kabila la Hausa.
 
Ila nchi za kiarabu ndo zinaongoza kwa kuwatesa watu weusi. Watu weusi wengi wanafanywa kama watumwa kwenye nyumba za kiarabu na pia nchi za kiarabu ndo zinaongoza kutoa hukumu ya vifo kwa watu weusi sasa si bora Marekani wanawafunga peke yake.
Hukumu Za kifo for what? Una stats yoyote ku backup? Na weusi Wa nchi Za kiarabu si wafanyakazi wa ndani, tofautisha mtu anaetoka huku kufanya kazi za ndani Middle East na mtu mweusi aliezaliwa Middle East.
 
Mix mwarabu na mu-Ethiopia, ndio investor mkubwa zaidi Ethiopia.
Aisee huu uongo wako, bado unaushikilia?
Lete ushahidi kuwa kachanganya.

Hivi unajua asilimia 13 ni watu wangapi kati ya watu 300,000,000.

Marekani
Tumeshuhudia Raisi akiwa mweusi Barack Obama
Waziri wa mambo ya nje Condoleeza
Rice
Defence secretary General Austin
Greatest surgeon
Na wengineo.

Hao waarabu ni wabaguzi na wakatili kupita maelezo
 
Aisee huu uongo wako, bado unaushikilia?
Lete ushahidi kuwa kachanganya.
Boss Al Amoud ni Mixer myemen na Mu Ethiopia, unafikiri hao Forbes na wengineo wanaemuweka kwenye list ya Black billionaire ni wajinga? Simple ukicheki wikipedia biography yake unaiona na ana Uraia pacha nchi zote mbili Saudi na Ethiopia
Hivi unajua asilimia 13 ni watu wangapi kati ya watu 300,000,000.
Asilimia 13 ni watu takribani milioni 39

Jela za wamarekani kuna watu kama 2M, kati ya hao 37% ni watu weusi,

Asilimia 16 ya watu weusi wamewahi kwenda jela.
Marekani
Tumeshuhudia Raisi akiwa mweusi Barack Obama
Waziri wa mambo ya nje Condoleeza
Rice
Defence secretary General Austin
Greatest surgeon
Na wengineo.

Hao waarabu ni wabaguzi na wakatili kupita maelezo
Again umeitaja watu sijui wanne ama watano, haiondoi fact kwamba population iliobakia hawana maisha mazuri, pia umekataa Al Amoud sio mu Africa then unaenda kutaja chotara kwenye hoja yako huoni ni double standard? Ama definition ya mtu mweusi kwako ni yule unaemtaka wewe tu?

Hii report inaelezea vizuri under representation ya watu weusi kwenye Ajira na sekta binafsi kwa Ujumla

Back
Top Bottom