Hivi kukatika maji Dar ni shida iko au ni mradi wa mtu?

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,892
Reaction score
7,780
Ni kama mwezi umepita tangu wakazi wa dar wametangaziwa kwamba sasa mradi wa kuboresha maji umekamilika. Matarajio ya watu bila shaka hapatakua tena na mgao.

Lakini la kushangaza bado kuna mgao wa maji sehemu nyingi za jiji. Kila siku ya pili ninapoishi mimi maji asubuhi yanakatwa.

Kwa uzoefu wangu ninajua kuna watumishi wa maji ambao wao kuweka mgao wa maji ni mradi wao. Ndio maana miaka yote nimeishi hapa dar hadi nimekua mzee pamoja na miradi mingi hakuna kipindi ambapo maji yamepatikana wakati wote jijini.

Kila mradi ukija utasikia ni mkopo toka world bank au kwingine nje ya nchi. Siku hizi ni mikopo kutoka India na makandarasi toka India. Ajabu miradi haimaliziki na wala shida ya maji haimaliziki.

Pamoja na kile chanzo kikubwa cha maji cha kimbiji. Kimbiji tulielezwa ni ziwa kubwa la maji safi chini ya ardhi ambalo liligunduliwa kwa bahati wakati wa kutafuta mafuta ya petroli.

Ni aibu kwamba tunabakia na upungufu wa maji wakati tuna bahari ya maji safi chini ya ardhi hapo kimbiji. Vigogo serikalini inaonekana kwao la muhimu ni kuja hela za miradi na sio kuwapatia wananchi maji.

Watanzania tutaendelea kukosa maendeleo na kubakia watu wa shida tu kama vigogo wa nchi hii bado wanabakia na dhana ya kupata utajiri kutokana na miradi ya kutatua shida za wananchi. Yaani shida za umma wa watanzania.
 
Hao Dawasa huwa hawafanyi kazi mpaka wafokewe na kufukuzwa kazi. Kuna uzembe mkubwa , fukuza watu kazi.
 
Ni kama mwezi umepita tangu wakazi wa dar wametangaziwa kwamba sasa mradi wa kuboresha maji umekamilika. Matarajio ya watu bila shaka hapatakua tena na mgao.

Lakini la kushangaza bado kuna mgao wa maji sehemu nyingi za jiji. Kila siku ya pili ninapoishi mimi maji asubuhi yanakatwa.

Kwa uzoefu wangu ninajua kuna watumishi wa maji ambao wao kuweka mgao wa maji ni mradi wao. Ndio maana miaka yote nimeishi hapa dar hadi nimekua mzee pamoja na miradi mingi hakuna kipindi ambapo maji yamepatikana wakati wote jijini.

Kila mradi ukija utasikia ni mkopo toka world bank au kwingine nje ya nchi. Siku hizi ni mikopo kutoka India. Ajabu miradi haimaliziki na wala shida ya maji haimaliziki.

Pamoja na kile chanzo kikubwa cha maji cha kimbiji. Kimbiji tulielezwa ni ziwa kubwa la maji safi chini ya ardhi ambalo liligunduliwa kwa bahati wakati wa kutafuta mafuta ya petroli.

Ni aibu kwamba tunabakia na upungufu wa maji wakati tuna bahari ya maji safi chini ya ardhi hapo kimbiji. Vigogo serikalini inaonekana kwao la muhimu ni kuja hela za miradi na sio kuwapatia wananchi maji.

Watanzania tutaendelea kukosa maendeleo na kubakia watu wa shida tu kama vigogo wa nchi hii bado wanabakia na dhana ya kupata utajiri kutokana na miradi ya kutatua shida za wananchi. Yaani shida za umma wa watanzania.
Huku Wazo,Goba, Mbezi wameambiwa hata kama mtu ana deni la elfu moja la mwezi uliopita kata maji nilikuwa nagombana nao wanataka nilipe faini ya elfu ishirini wakati nalipa Baki ya 7000- la sivyo wanakata.
Nadhani hawana fedha za uendeshaji mitambo na dawa
 
Back
Top Bottom