Hivi kumbe unaweza toka na gari na hauna hata shillingi mia mfukoni

Hivi kumbe unaweza toka na gari na hauna hata shillingi mia mfukoni

Samcezar

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
13,095
Reaction score
22,731
Dah nimeanza kujifunza kitu. Kuna muda mtu unamuona anapita na kausafiri kake especially hivi vibaby walker, ukasema ameyapatia na ile hali hapo hiyo route anapokwenda akikosa anachokifuata basi anaweza asiweze kuamsha gari sababu ya kukosa fuel ya kumrejesha home.

Kuna mshikaji hapa analalamika yupo empty set gari taa ya tank ya mafuta ina blink na yeye mfukoni mia hana. Aiseee haya maisha yetu haya.

Mshawahi pitia situation kama hii wakulungwa. Najua wengi imetukuta hebu tushare experience mlifanya mbinu gani. Given kuwa hapo wazee wako wa busara nao wote juu ya mawe so kuwamake call wakutumie inakuwa ni wazo tasa.
 
Anaishi maisha ya hatari sana huyo jamaa, ukiweka gari barabarani hakikisha una angalau 50,000 ya kuongea na traffic, wale jamaa hawaelewi lugha nyingine.
Hahahaha sijawahi kuwapa labda waombe tena kwa adabu, juzi mmoja nilimpa buku mbili Wilaya ya Ikungi huko
 
Aisee mimi hiyo mara nyingi sana sana nikiwa naenda kazini ila najitahidi niwe na angalau 5000 ya emergency
 
Anaishi maisha ya hatari sana huyo jamaa, ukiweka gari barabarani hakikisha una angalau 50,000 ya kuongea na traffic, wale jamaa hawaelewi lugha nyingine.
Imagine hapo ndio umevuka zebra na raia walikuwa wanapita.... Dah....
 
Walau 10k mfukoni, that's for emergency. Kungurumisha gari barabarani bila hata mia mfukoni ni hatari sana, hata kama gari ipo full tank.
Ndio mimi nikawa nawaza jamaa anavyonambia dah nikaona hii haijakaa sawa. Ingawa nimempanga kuwa awe makini....
 
Kuna jamaa yang yet alinipa gar akaniambia tumia tu kweny mizunguko yako kwakua ilikua imepak tu,, ile gar nilitumia wik 3 tu nikamrudishia akashangaa chuma imepak nje ya get nikamkabidhi key.

Nilijikuta naishi kwa gharama sana ala kipato cha kawaida ningeweza kuimudu ndiyo ila nisingeweza kusave pesa,, mm naamin kila kitu na wakat wake.
 
Hiyo laki tano inakaa muda mrefu sana kwenye gari kaka inakata mwezi wa tano huu...
kama bank vile nikikwamaga naichomoa then narudisha
Bit laki tano nyingi sana. Hata mbili ni fair enough.....
 
Ni hatari sana.

Imenitokea wiki iliyopita natoka udsm, sasa kama unaenda kimara lazima uje upite mawasiliano hapa, sasa kuna hilux iko mbele yangu ikakatisha kwenye barrier zile za barabara ya fly over na ile ya kawaida, na mimi nkataka kuiga, tairi za mbezi zimepita gari ikakaa, tia 4wd, chuma ikagoma, mfukoni empty set.

Aisee nlipagawa traffic wako pale mawasiliano. Bahati nzuri boda na jamaa mmoja anapita wakanipa msaada kupush ikarudi nyuma then nkawaomba sina kitu wakanielewa though maneno ya dharau nlipewa.

Usitembee mjini na kausafiri bila pesa mzee, ni hatari kwa afya.
 
Kuna jamaa yang yet alinipa gar akaniambia tumia tu kweny mizunguko yako kwakua ilikua imepak tu,, ile gar nilitumia wik 3 tu nikamrudishia akashangaa chuma imepak nje ya get nikamkabidhi key
Nilijikuta naishi kwa gharama sana ala kipato cha kawaida ningeweza kuimudu ndiyo ila nisingeweza kusave pesa,, mm naamin kila kitu na wakat wake
Ha ha ha ha ha ha ha honest truth. Gari bila kipato ni sawa na mwanaume asiye na pesa kuishi na mwanamke mzuri anaetakwa na kila mwanaume.

Gari haitaki maigizo. Gharama inakuja katika sura nyingi.

Mafuta maana kila unapotembea unachoma mafuta.

Watu watakuomba hela na michango ya ajabu wakiamini wewe ni kibopa, mademu wenye njaa watakulegezea na ukiingia mkenge watakuletea bili zao ulipe na itakulazimu kujitutumua, familia nzima watakuona upo vema hawaisha kukuomba misaada.

Muda wowote gari inaweza pata pancha, mikwaruzo, wizi wa parts za gari, of which ni unforseen events so itakulazimu kuingia gharama.

Kila baada ya kipindi fulani gari itataka services kama oil, matairi na kadharika.

Matraffic humo barabarani mara nyingi wanamakosa ya kulazimisha ili uwatoe chochote kuanzia 5000. Na hapo itategemea unatumia gari ya size gani.

So matumizi ya gari = uwe vema kwenye kipato at least 40,000 per day na kazi ya at least 500,000.
 
Back
Top Bottom