Kuna jamaa yang yet alinipa gar akaniambia tumia tu kweny mizunguko yako kwakua ilikua imepak tu,, ile gar nilitumia wik 3 tu nikamrudishia akashangaa chuma imepak nje ya get nikamkabidhi key
Nilijikuta naishi kwa gharama sana ala kipato cha kawaida ningeweza kuimudu ndiyo ila nisingeweza kusave pesa,, mm naamin kila kitu na wakat wake
Ha ha ha ha ha ha ha honest truth. Gari bila kipato ni sawa na mwanaume asiye na pesa kuishi na mwanamke mzuri anaetakwa na kila mwanaume.
Gari haitaki maigizo. Gharama inakuja katika sura nyingi.
Mafuta maana kila unapotembea unachoma mafuta.
Watu watakuomba hela na michango ya ajabu wakiamini wewe ni kibopa, mademu wenye njaa watakulegezea na ukiingia mkenge watakuletea bili zao ulipe na itakulazimu kujitutumua, familia nzima watakuona upo vema hawaisha kukuomba misaada.
Muda wowote gari inaweza pata pancha, mikwaruzo, wizi wa parts za gari, of which ni unforseen events so itakulazimu kuingia gharama.
Kila baada ya kipindi fulani gari itataka services kama oil, matairi na kadharika.
Matraffic humo barabarani mara nyingi wanamakosa ya kulazimisha ili uwatoe chochote kuanzia 5000. Na hapo itategemea unatumia gari ya size gani.
So matumizi ya gari = uwe vema kwenye kipato at least 40,000 per day na kazi ya at least 500,000.