Hivi Kuna app ambayo mtu akiwa na namba Yako anaweza kujua jina lako

Hivi Kuna app ambayo mtu akiwa na namba Yako anaweza kujua jina lako

Godoro la kioo

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2025
Posts
456
Reaction score
1,003
Wakuu. Teknolojia inazidi kukua Kila kunapokucha

Kama ilivyo kwa Whatsapp mtu akiwa na namba Yako anaweza kuona picha Yako

Je Kuna app ambayo mtu akiwa na namba Yako inaweza kumletea jina lako au hata akaunti zako za mitandao ya kijamii

Nauliza hivyo kwa sababu Leo mchana Kuna mwanadada amenipigia sim na kuniambia maombi yangu ya kazi yamekubaliwa


Kilichonishangaza ni kwamba kanitaja kwa jina langu

Sasa najiuliza namba yangu kaitoa wapi na je. Kajuaje jina langu

Hisia zangu zinaniambia huyu mwanadada Inawezekana akawa aidha ni tapeli kwa sababu zifuatazo


1) Sijawahi kutuma maombi ya kazi sehem yoyote Ile

2)Sina mtu wa kuniunganisha kwenye hiyo ofisi aliyoitaja.


Hofu nyingine niliyonayo isije kuwa ni mtu wa kitengo hivyo ananivuta Ili nijae kwenye 18

Mara nyingi Huwa tunajiachia humu jukwaani na kuandika chochote tunachojisikia Sasa isije kuwa ni miongoni mwa memba wa humu na yupo kwa kazi maalumu


Swali jingine nalojiuliza Inawezekana kwamba baadhi ya wanachama ni watu wa vitengo maalumu?

Na je Inawezekana kwamba jf licha ya kutumia majina feki, VPn n,k ikawa siyo sehem salama Tena kama ambavyo Huwa tunafikiria

Anyway nisiwachoshe ila nilitaka kujua je. Kuna app ambayo mtu akiwa nayo basi inaweza kumsaidia kujua jina lako??
 
1. Kuangalia jina NMB App, CRDB, Yas etc inatosha kujua jina ulilosajilia.

2. TrueCaller App inasaidia kujua iyo namba “watu wengine wenye app ya TrueCaller” wameisevu vipi. Mfano: Ukiwa na TrueCaller App hafu kuna namba ngeni inakupigia unaweza kuta jina likajiandika “Dagaa Mbezi” inamaana kuna mtu iyo namba kaisevu ivo.

3. Kutumia WhatsApp kaa iyo namba iko, naweza kujua jina ulilojiandika.
 
Back
Top Bottom