Hivi kuna gharama za uhamisho kwa mtoto wa Shule ya Msingi?

Hivi kuna gharama za uhamisho kwa mtoto wa Shule ya Msingi?

crome20

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2010
Posts
1,193
Reaction score
810
Nimekwenda shule fulani hapa Dar kutaka kumuhamisha kijana wangu anayeingia STD 7 nikaambiwa gharama ni sh 10000/=, Is this real?

Cha ajabu risiti hatoi nilipo muhoji maelezo yake hayakunitosha. Kwa vile nilikuwa na assignment ya haraka sikuwa na MUDA wa kubishana nae.

Lakini Kama itakuwa sio kweli kesho namuibukia fasta. Elfu kumi sio mchezo.
 
Elfu kumi tu unafungulia uzi, wenzako sekondarí tunatoa had laki tano na risit hatujui tena sisi ndo tunabembeleza, tujifunze watz hakuna cha bure.

Kama unamtoa saint Kayumba unampelek Cambridge lipa hiyo hela, mbona ndogo sana huko unakompeleka c gharama tayari, utamnunulia unoform mpya tena ikiwezeka drafter, utamsafirisha. Hayo yote zaid ya afu kumi

So toa wala isikuume roho
 
Elfu kumi tu unafungulia uzi, wenzako sekondarí tunatoa had laki tano na risit hatujui tena sisi ndo tunabembeleza, tujifunze watz hakuna cha bure

Kama unamtoa saint Kayumba unampelek Cambridge lipa hiyo hela, mbona ndog sana huko unakompeleka c gharama tyr, utamnunulia unoform mpya tena ikiwezeka drafter, utamsafirisha
Hayo yote zaid ya afu kumi

So toa wala isikuume roho
Yani unamcheka Mwenzio alietoa elfu 10, wewe uliyetoa Laki 5 unajiona Mjanjaaaa!.
Kama sio Uzwazwa ni nini?
 
Nimekwenda shule fulani hapa Dar kutaka kumwamisha kijana wangu anayeingia STD 7 nikaambiwa gharama ni sh 10000/=, Is this real..
1672699343589.png
 
Elfu kumi tu unafungulia uzi, wenzako sekondarí tunatoa had laki tano na risit hatujui tena sisi ndo tunabembeleza, tujifunze watz hakuna cha bure...
Issue sio kiasi Cha pesa, Cha msingi Je ni halali ? Kama huwezi kufuatilia Mambo madogo., ujue Hata haki zako zingine hutakuwa na ujasiri wa kufuatilia.

Na hapa wabongo ndio tunafeli. kwani tozo ni hela nyingi? Mbona imeleta msuguano mkubwa ktk jamii
 
Issue ni Je? Hizo GHARAMA zipo kisheria? Ndio msingi wa hoja yangu. Kama hujui pita tu
Lakini la msingi lipa 10k hamisha mtoto, hizo nguvu zoote hadi faida elimu kisa 10k ....sasa kwenye ada itakuwaje
 
Nimekwenda shule fulani hapa Dar kutaka kumuhamisha kijana wangu anayeingia STD 7 nikaambiwa gharama ni sh 10000/=, Is this real?

Cha ajabu risiti hatoi nilipo muhoji maelezo yake hayakunitosha. Kwa vile nilikuwa na assignment ya haraka sikuwa na MUDA wa kubishana nae.

Lakini Kama itakuwa sio kweli kesho namuibukia fasta. Elfu kumi sio mchezo.
haipo kisheria itakua utaratibu tu wa shule Ila pia ukumbuke uhamisho siku hizi unafanyika Kwa njia ya mtandao. Mwalimu atahitaji kuwa na hela ya mawasiliano na shule anayotokea. Unataka shule ikugharamikie ? kingine cha kujua hela ya capitation ya mwanao inaenda kwenye shule aliyopangwa hivyo hapo unamuhamishia atakua burden Kwa shule na mwisho kupewa nafas ya kuhamia ni hisani mkuu anaweza kukataa pia
 
Hela ya capitation fafanua zaidi. Ni ipi hiyo na inahusikaje katika uhamisho
 
Hakuna gharama yoyote, labda kama ni private unaweza kukuta gharama kidogo ya mtihani wa kumpima kwenye shule anayoenda (nayo inategemea na utaratibu wa shule).
 
Hela ya capitation fafanua zaidi. Ni ipi hiyo na inahusikaje katika uhamisho
ni ruzuku ya kuendeshea shule, inatolewa Kwa kuangalia idadi ya wanafunzi, mwanafunzi anapohama ule mwaka wa Kwanza anakua anahesabiwa shule aliyotoka na hela yake inaenda huko
 
Hii nadhani ni Gov school. Issue yangu NI private school.
 
Mbona kakutajia pesa ndogo sana hiyo?????

Unajua gharama za bundles na nauli??????au unafikiri hilo kadi la mwanao linajipeleka lenyewe halmashauri?

TAFUTA HELA.
 
Back
Top Bottom