Hivi kuna maelezo yeyote ya kitaalamu yaliyotolewa na mamlaka husika juu ya changamoto ya mtandao

Hivi kuna maelezo yeyote ya kitaalamu yaliyotolewa na mamlaka husika juu ya changamoto ya mtandao

Kenya wamerudisha Kwa asilimia 100%
Sasa hapo ndio utajua Technology haitaji bwebwe na maneno mengi sio kazi za kupeana Kwa connection..
Tuna waziri mzigo anatia hasara Sana
Hizo nyaya huko baharini zinamilikiwa na kampuni za kimataifa ikiwemo SeaCom nadhani ndio hii inayotusambazia sisi Afrika Mashariki. Hivyo hata likitokea tatizo wao ndio wana deal nalo. So, kama kenya imerudi kwa asilimia mia hata sifa sio za hao wakenya wenye cable zao wamemaliza matengenezo. And by the way tatizo lilizipata nchi 12 na Tanzania ndio iliathirika zaidi kuliko hizo zote.
 
Labda nikuulize hio link nyingine wanayotumia tunapata internet yenye speed hafifu kwa maelezo yao ni ipi? Ni satellite ama nyaya zingine?
walisema ni nyaya nyingine inatokea Madagascar, ambayo ni secondary link ya Tigo/Zantel,
Na imezidiwa kwa kuwa ISPs karibia wote wameungwa hapo kwa dharura
 
Ma Commercial Bank Yameathirika, Huduma Hazisongi Ipasavyo, Hata Kiuchumi Itatuathiri Hii
 
Mkuu,

Nakuelewa sana maumivu yako. Pole sana.

Ni jambo moja kuwa na tatizo kama hili, ni jambo tofauti kuwa na tatizo halafu hakuna hata updates.

Miezi michache iliyopita kuna meli iligonga nguzo ya daraja mjini Baltimore, Maryland USA. Daraja likaanguka. NIkawa naangalia wale viongozi kuanzia meya mpaka gavana wanavyoitisha press conferences kuwajulisha watu nini kimetokea, maendeleo, njia mbadala za kutumia, na hata pale ambapo walikuwa hawana majibu walikuwa wanasema kwa sasa ni mapema mno hatuna majibu, tunafanyia kazi, tutawajulisha tena maendeleo baada ya muda fulani.

Nilivyowaona wanafanya vile nikafikiria sana Tanzania na kusema tunaweza kujifunza mengi kwenye Disaster Management kutoka kwao.

Huku kwetu Nape akisha tweet ki vague tweet tu ndiyo imetoka hiyo.
Huko kwa Biden hata umeme ukizimwa ukipiga simu shirika la umeme basi voice record inakwambia kama una hitilafu ya umeme county flani. Kuna matatizo ya kiufundi yametokea pahala fulani tunategemea by 6pm umeme utarudi kama kawaida.

Tanesco utasahau na ukipiga simu hakuna jipya hii nchi haina hata mfumo flani wa kuonekana kama unajali raia wake.
 
Unamtegemea Nape atoe maelezo ya kitaalamu? Are you serious?

Labda aulizwe ni kwa nini nchi karibia zote zimeshatatua (au zinaelekea kutatua) tatizo hili isipokuwa sisi?

Badala ya kuwekeza sana kwenye Science, Technology, Engineering and Math (STEM); ndiyo kwanza tumeanzisha tahasusi (combinations) za dini zaidi ya 10 kudadadeki!

IMG-20240514-WA0052.jpg
 
Hili tatizo limechukuliwa poa lakini lina athari kubwa sana kuliko wanavyofikiri 🤒😎
 
Ni takribani siku kadhaa sasa tangu internet nchini imekuwa na changamoto.

Hadi sasa tunachofahamishwa ni kwamba kuna nyaya huko baharini zimeleta hitilafu, hilo ndilo kila mmoja nchini utasikia akisema, sasa najiuliza na huu mtandao ulivyo chini ina maana kuna nyaya zilibaki ndizo zinaleta mtandao huu hafifu? Au tumekodi satellite kama backup kwa muda.

Hao wataalamu wa IT huko TCRA na mamlaka husika hawana uwezo kufanya press conference na vyombo vya habari kuelezea wananchi kwa kina au kutoa elimu mwanzo mwisho kuhusu jambo lililotokea na mfumo mzima wa huo mkonga unavyofanya kazi, je umeleta hasara ipi? Je kuna ulazima wa kuwa na back up kwa wakati ujao? Ilishawahi kutokea mara ngapi? Mitandao ya simu itafidia gharama za watumiaji walioathirika na hili tatizo? Kuna mengi ya kuelezea tena kwa maelezo ya kitaalamu ili wananchi waelewe. Au na hao IT na wao ni weupe vichwani kutoa maelezo, au pengine wateja au wananchi hawapaswi kuwa na uelewa wa kinachoendelea? Kingine serikali iangalie mawaziri wenye uelewa mkubwa kuhusiana na wizara husika.

Hili suala limeathiri shughuli za wengi, kuna vijana wana hizi online TVs, kuna vijana wana trade stocks n.k kwa kifupi internet imesaidia wananchi wengi kujiajiri kuna watu internet ndio maisha yao, lakini kwa jinsi mamlaka zinavyochukulia hili suala ni kama jambo la kawaida tu. Suala la mtandao ni issue serious. Kushirikiana na wananchi kunaweza pelekea utatuzi wa tatizo hili kwa siku zijazo.

Ukimuuliza mtu mbona mtandao upo chini utasikia kuna nyaya huko baharini zina hitilafu. Hizo nyaya zenyewe hajui hata zinafanana vipi. Ukimuuliza hitilafu imesababishwa na nini hapo jibu hana.

Wanasiasa na mamlaka husika nyie mmeajiriwa na wananchi lazima kuhakikisha wananchi wanapata updates kwa kila kinachoendelea kwa maelezo ya kitaalamu yasiyoleta shaka, vijana sasa wamesoma wana uelewa mkubwa kuhusu ulimwengu huu wa kidijitali.

Katika kituko cha karne ni pale kuna shida ya internet halafu mamlaka husika zinakwenda kutoa taarifa mtandaoni kupitia mitandao ya kijamii, sasa hao wananchi wanapata vipi taarifa?


Hii nchi tuna safari ndefu.
Kama serikali inakata umeme bila kujali shughuli za walipakodi nchini, usitegemee hao jama TCRA wanajali lolote zaidi ya maagizo kutoka juu.

Tuendelee na katika hii kandamizi inayounda mungu-mtu hadi akili zihamie vichwa vya juu
 
Back
Top Bottom