Hivi kuna maelezo yeyote ya kitaalamu yaliyotolewa na mamlaka husika juu ya changamoto ya mtandao

Kenya wamerudisha Kwa asilimia 100%
Sasa hapo ndio utajua Technology haitaji bwebwe na maneno mengi sio kazi za kupeana Kwa connection..
Tuna waziri mzigo anatia hasara Sana
Hizo nyaya huko baharini zinamilikiwa na kampuni za kimataifa ikiwemo SeaCom nadhani ndio hii inayotusambazia sisi Afrika Mashariki. Hivyo hata likitokea tatizo wao ndio wana deal nalo. So, kama kenya imerudi kwa asilimia mia hata sifa sio za hao wakenya wenye cable zao wamemaliza matengenezo. And by the way tatizo lilizipata nchi 12 na Tanzania ndio iliathirika zaidi kuliko hizo zote.
 
Labda nikuulize hio link nyingine wanayotumia tunapata internet yenye speed hafifu kwa maelezo yao ni ipi? Ni satellite ama nyaya zingine?
walisema ni nyaya nyingine inatokea Madagascar, ambayo ni secondary link ya Tigo/Zantel,
Na imezidiwa kwa kuwa ISPs karibia wote wameungwa hapo kwa dharura
 
Ma Commercial Bank Yameathirika, Huduma Hazisongi Ipasavyo, Hata Kiuchumi Itatuathiri Hii
 
Huko kwa Biden hata umeme ukizimwa ukipiga simu shirika la umeme basi voice record inakwambia kama una hitilafu ya umeme county flani. Kuna matatizo ya kiufundi yametokea pahala fulani tunategemea by 6pm umeme utarudi kama kawaida.

Tanesco utasahau na ukipiga simu hakuna jipya hii nchi haina hata mfumo flani wa kuonekana kama unajali raia wake.
 
Unamtegemea Nape atoe maelezo ya kitaalamu? Are you serious?

Labda aulizwe ni kwa nini nchi karibia zote zimeshatatua (au zinaelekea kutatua) tatizo hili isipokuwa sisi?

Badala ya kuwekeza sana kwenye Science, Technology, Engineering and Math (STEM); ndiyo kwanza tumeanzisha tahasusi (combinations) za dini zaidi ya 10 kudadadeki!

 
Hili tatizo limechukuliwa poa lakini lina athari kubwa sana kuliko wanavyofikiri 🤒😎
 
Basi ingekuwa ni bure pka itengemae sasa wanachukuwa ela za bando za nini ni wezi
 
Kama serikali inakata umeme bila kujali shughuli za walipakodi nchini, usitegemee hao jama TCRA wanajali lolote zaidi ya maagizo kutoka juu.

Tuendelee na katika hii kandamizi inayounda mungu-mtu hadi akili zihamie vichwa vya juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…