Hivi kuna maisha baada ya kifo?

Okoka leo, maisha baada ya kifo yapo, ya mateso au ya kupumzika kusubiri siku ya mwisho. Yesu Kristo mwenyewe alithibitisha hili kwa kutoa mfano wa LAZARO na TAJIRI. jambo linalothibitisha kwamba, kumbe baada ya mwili huu kufa, roho ina maisha mengine huko, kitakachodetermine wapi unaenda ni kama ulimpa Yesu Kristo maisha yako hapa duniani, yeye ndiye njia kweli na uzima, hupati uzima wa milele bila kupitia yeye, yeye pekee ndiye aliyemwaga Damu ya ukombozi kwa ajili ya ondoleo la dhambi ili mtu atakayesafishwa astahili kuingia uzima wa milele, mitume wengine wote hata waseme maneno gani hawajamwaga Damu, hawajatoa kafara, wanakuletea maneno matupu, ila Yesu Kristo alikufa kwa ajili yako, amekupa mbele yako mlango wa uzima uchague kuingia au ubaki mautini. soma jinsi Biblia ilivyosema hapa chini:

LUKA 16:19 - 31 INASEMA:
Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa. Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi, naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.

Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.

Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.

Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.

Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu, kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso. Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.

Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu. Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.
 
Nipe namba ya simu ya huyo aliyekwambia kuna maisha baada ya
kufa. Ninataka kuongea nae nikupe majibu mazuri.
 
ndugu usijidanganye, sio hekaya, baada ya kifo kuna maisha, mazuri au mabaya kutegemeana na jinsi ulivyoishi hapa duniani. kibaya zaidi hatujui lini tutaondoka ili tujiandae, huwa inakuja ghafla ndio maana tunatakiwa kukesha tukiwa tumejiandaa kwasababu hatujui siku wala saa.
 
You had no life before life but you want to have life after life in imaginary places..!!

You cannot wish for a house of gold in heaven while you have never touched gold right here on earth.

If you fail to live on earth the fantasy of heaven is an illusion.

Hakuna maisha baada ya kufa.

Ukifa unakwenda kuwa chakula cha bacteria una decompose na kuwa underground soil...
 
Unaweza kuthibitisha hayo maisha baada ya kifo yapo na si mawazo yako ya kufikirika tu?
 
Mkuu,Hyo ni mafundisho ya DINI.Swali JE Maisha ni nini?Umilele ni nini?Je unapokuwa katika Moto wa Milele una uhai au unakuwa umekufa?Na Huko kwenye Uzima wa Milele unakuwa unafanya nini?

So Unamaanisha kwamba Hapa Kwnye Dunia Tupo Shule then kuna mtihani tukifaulu tunawekwa kundi jingine na tukifeli kundi jingine?Kwamba Baada ya maisha hapa Duniani tutapewa matokeo ya Maisha yetu?Nafikiri aliyeuliza swali hakuwa anahitaji mafundisho ya DINI yy alitaka kujua JE mtu akifa akazikwa kuna maisha?Je ni ukishakufa hakuna Maisha kama unavyoyafahamu au tunavyoishi.Ila sio kwamba Unaacha kuwepo.Mwanadamu yupo,alikuwepo na atakuwepo.Swala la JINSI na namna ya UWEPO kabla na baada ya Maisha ya duniani bado ni swala ambalo linahitaji utulivu kulielewa ILA BAADA YA KIFO KUISHI KUNAISHA
 
Mtu asemaye kuna maisha baada ya kifo, hana tofauti na mtu asiyeelewa maana ya neno kufa.

Kwa dhana ya viumbe hai,
Kufa maana yake ni mwisho wa kiumbe hicho kuishi (mwisho wa maisha)

"Nafikiri mwili wa kiumbe hai ni sawa na kompyuta,
Kompyuta itaacha kufanya kazi pindi ambapo moja ya kifaa chake kitaharibika.

Hakuna mbingu wala maisha baada ya kuharibika kwa kompyuta hiyo.

Habari za mbingu na kuzimu ni hadithi za watu wanaoogopa giza. "
 
Roho ni kitu gani?

Unaweza thibitisha uwepo wa hiyo roho kama si hadithi za dini na imani tu!?
 
Absolutely true
 
unafikir hiyo life ambayo hukuwa nayo kabla ya life. uliitaka? au unafikir imekuja coincidence tu!.
 
Either ni mafundisho au lah ila kujibu swali la maisha ni nini? lazma uelewe wewe ni nani?. ( note.sijauliza jina lako wala personality yeyote kwako)

na kujua umilele ni nini nikuulize swali lingine kifo ni nini.
majibu ya maswali yako yako kwny majibu ya haya niliokuuliza
 
Roho ni kitu gani?

Unaweza thibitisha uwepo wa hiyo roho kama si hadithi za dini na imani tu!?
wewe ni nani. note Smotor linaweza kuwa jina lako na ukifa ukawekwa kwny sanduku tutasema ule ni mwili wako je wewe uko wapi hapo?.
 
umezungumza sawia kabisa mwili sasa huyo mtu yuko wapi kama mwili wake unaenda kushambuliwa na bakteria huko ardhini.
na hata ukifa leo tutasema mwili wa marehemu ila bado ww hatutakutaja hapo uko wapi?
 
.... Mwili ni sawa na computer.. je wewe ni mwili?
 
Wewe umekufa au upo hai na kama upo hai dhibitisha,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…