Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 12,675
- 25,924
Okoka leo, maisha baada ya kifo yapo, ya mateso au ya kupumzika kusubiri siku ya mwisho. Yesu Kristo mwenyewe alithibitisha hili kwa kutoa mfano wa LAZARO na TAJIRI. jambo linalothibitisha kwamba, kumbe baada ya mwili huu kufa, roho ina maisha mengine huko, kitakachodetermine wapi unaenda ni kama ulimpa Yesu Kristo maisha yako hapa duniani, yeye ndiye njia kweli na uzima, hupati uzima wa milele bila kupitia yeye, yeye pekee ndiye aliyemwaga Damu ya ukombozi kwa ajili ya ondoleo la dhambi ili mtu atakayesafishwa astahili kuingia uzima wa milele, mitume wengine wote hata waseme maneno gani hawajamwaga Damu, hawajatoa kafara, wanakuletea maneno matupu, ila Yesu Kristo alikufa kwa ajili yako, amekupa mbele yako mlango wa uzima uchague kuingia au ubaki mautini. soma jinsi Biblia ilivyosema hapa chini:Habari wana JF,
Hivi kuna maisha baada ya kifo?
Au bado sijui maana ya kifo?
Yaani babu yangu liyemzaa bibi yangu bado anaishi baada ya kufa? Kwamba hawa waliokufa wanaishi ila waneshakufa?
Au naombeni maana ya kifo ili ning'amue huu mzozo.
(Kuna mtu kaniambia kuwa kuna maisha baada ya kufa)
LUKA 16:19 - 31 INASEMA:
Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa. Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi, naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.
Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.
Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.
Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.
Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu, kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso. Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.
Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu. Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.