Hii Kwa wasioamini dini(wazee wa logic and seenable things)
💥Kama umezaliwa hukuwa unajua utaish ,vip useme hamna maisha baada ya kifo ,we unatakiwa useme tu sijui maana ukisema hamna maisha manake ushajua na una elimu ingali hujakufa ukafika huko ukapata experience.
Na usijiaminishee unajua kila ktu Mana Kuna vtu vingi tu vimewashinda mfano mpak leo hamuwez hta kutibu vidonda vya tumbo kwa logic zenu kazi tu kutupa miji-antiacid,cancer imewashinda pia manake kumbe mna upungufu wa elimu .so atheist mkiulizwa kuhusu kifo mjibu hamjui.
💥Wenye Imani zetu(mnaotukebehi mkatuita wafia dini).
Tunaamini maisha yapo kwa kutumia mitume na vitabu ambavyo vimeshushwa kutupa muongozo.
Mfano waislamu sisi Tuamini hivi kuhusu kifo:
a)siku yako ya kufa watakuja malaika wengne watasimama kulia kwako na kushoto kwako haf Yule anaetoa roho atasimama sehemu ya kichwa ataamuru roho itoke na ikitoka wale malaika wengne wataichukua na kuivisha vazi flani (halijulikan namna yake) Kisha watapaa na roho kuelekea mbinguni.
b)kwa sisi waislamu mbigu zpo tabaka Saba ,so watapaa kuelekea tabaka la Saba kuipeleke hyo roho ambapo Kuna vtabu viwil Cha watu wema na waovu,na kila mbigu Ina malaika ambapo roho inapokuwa inapitishwa huulizana Ni Nani (baadhi ya malaika watakutaja kwa jina lako ulokuwa waitwa duniani)Mana lile vazi roho huvishwa huwa na harufu mbaya kwa muovu na nzuri kwa mwema.
C)Kama Ni mwema roho huenda mpak tabaka la Saba na huuandikwa kweny ktabu kinaitwa "iliyyin" ktabu ambacho huuandikwa watu wema tuu. Kama muovu huishia mbigu ya kwanza tu na hutupwa ardhini Mana Allah ameahid milango ya mbigu haitofunguliwa kwa watu waovu(mbigu kiimani Zina milango Ila haimanishi Kama hii ya nyumbani Yani Ni jina tu lakushabihisha,NB:vtu vyote ambavyo vpo baada ya kufa havifanan na hivi vyetu Ila Ni majina tu ili tuelewe Mana hakuna aliyewahi viona kwa macho). kwahyo muovu ataandkwa kweny ktabu Cha waovu kinachoitwa "sijjin".
c)uwe muovu au mwema wote roho zao ztarudishwa ardhini kweny miili yao baad ya kuzikwa Mana Allah katika suratul-twaha amesema "kutokana na hyo ardhi tmuekuumbeni(Yani adamu Mana ya ndo wa kwanza na asili yetu) na humo tutakurejesheni na tutakutoeni kwa Mara nyengne Tena (ufufuo)".
Roho zikirudishwa Kuna malaika watakuja kaburini kukuuliza maswali matatu tuu 1.Nani mola wako 2.Muhammad Ni Nani 3.umemjuaje Muhammad.
d)Kama Ni mwema,atajibu maswali yote na atakapoulizwa amemjuaje Muhammad atasema alisoma Quran.
Hvyo malaika watamuonyesha Moto aloambiwa na pepo aloahidiwa na Yale matendo mema alofanya duniani yatamjia Ni Kama kiumbe flani umbile la binadamu ,Yani kitaumbwa kiumbe kibinadamu lakini Ni matendo yake mema ili kumfariji yeye na upweke. Basi mtu mwema ataomba kiama kisimame mana ameona mambo yote na yey Ni katika walofaulu ili alipwe pepo yake.
d) Kama Ni muovu atashindwa kujibu maswali Mana atapatwa na uoga na haya maswali hujibu kwa ujanja Bali vle we ni muovu au mwema tu, akiulizwa kuhusu Muhammad atasema alikuwa anaskia watu wakisema Yani hamjui ,hvyo malaika watamuadhibu vikali , na Kuna adhabu mbalimbali Kama Kuna majoka ambayo Kama sumu yake itafika ardhini hakuna mmea utaota na Ni wakubwa wanatisha na matendo yake maovu yataubwa kuwa kiumbe kitakacho muadhibu ,na ataomba kiama kisisimame Mana atonyeshwa Moto na utafunguliwa milango yake hivyo joto lake na mrindimo wake utamfikia.
💥Haya maisha ya Kaburini yanaitwa maisha ya barzakh na Ni endelevu mpak siku ya hukumu.
NB: 1.maelezo Ni marefu nkipata mda ntaandika Uzi wa maisha ya milele kulingana na Imani yangu Mimi inshallah.
2.namsikitikia mtu anaye tarajia kufa haamini chochote manake anakufa Kama mnyama ambaye Hana akili ya kufikirii , hajipangii future yake anasubir future impangie.