Hivi kuna maisha baada ya kifo?

Hivi kuna maisha baada ya kifo?

Nzi ana roho? Plasmodium ana roho? Kama anayo inaenda wapi after death..kama hawana Wanaishi vipi bila roho
Broo; Kwani nzi na plasmodium wameumbwa kwa mfano na sura ya Mungu?
Nzi na Plasmodium ni viumbe hai i.e. Wana uhai lakini wakifa ndo bas tena. Ukiondoa binadamu, viumbe wote tumepewa ruksa sisi binadamu tuwatawale na kuwatumia kwa mustakabali wa maisha yetu (Mwanzo 1:26-28).
BTW: Wewe hangaikia yale yanayokuhusu ww binadamu achana na habari za hao viumbe wengine kama wana roho au la na wakifa wanaenda wapi. Mtakutana huko-huko kama nao huwa wanaenda huko tunakokwenda sisi. Hahahahaaaa.
 
Mimi nauliza hivi kuna uwezekano wa mtu au kiumbe kuishi baada ya kufa/kifo? Na kama ni ndio basi maana ya kufa ni ipi?
Hizo roho ni kiumbe hai? Au ni kitu gani? Kama ni ndio ni kiumbe kama sisi na wanyama na miti nk: basi utatusaidia kutuonesha hao viumbe roho, tunataka hata kwa macho ya mkaa tuione hiyo roho kama hatuwez kuwaona kwa macho ya nyama. Ila chamsingi tujiulize kuhusu hawa viumbe, kama mimi na wanyama hata wadudu wanaweza kuishi baada ya kufa? Na kama ndio sasa kufa maana yake nini?
Mkuu, hoja ya kuishi baada ya kufa imekaa kiimani zaidi.Kama huamini hivyo ni sawa Hakuna kuishi baada ya kifo. Lakini kama unaamini, basi jibu ni Ndio kuna maisha baada ya kifo.
Maana ya kufa ni pale Kitendo cha mwili kutengana na Roho iliyo ndani mwako. Ni pale mwili wako unapotwaa hali ya Umauti. Baada ya Umauti watu wenzako wanakufukia ardhini (wanakuzika) kwani huna tena maslahi/faida kwao. Mwili wako ni maiti na punde utaingia katika mchakato wa kuyarudia mavumbi(utaoza).
Roho sio kiumbe bali ni Nafsi hai au unaweza kusema roho ndiyo UZIMA.
 
Mkuu,Hakuna maisha baada ya Kifo wala kabla ya Kuzaliwa.Wewe utaendelea Kuwepo na Bibi na babu yako bado wapo ila hawapo HAI na hawana Maisha kama ambavyo unavyoyaishi hapa DUNIANI ila wapo Ila HAWAISHI
Wapo wapi sasa
 
ndugu maisha baada ya kifo yapo. kuna umilele baada ya haya maisha ya duniani binadamu huishi milele. maana binadamu ana roho ambayo haifi kinachokufa ni mwili.
umilele wa binadamu baada ya maisha hapa duniani hutegemea sana alivyoishi hapa duniani na kuna sehemu mbili tu ambazo mwanadamu anakwenda baada ya maisha hapa duniani. ni either uzima wa milele au moto wa milele.
Dah! Nimekwisha!
 
Mkuu, hoja ya kuishi baada ya kufa imekaa kiimani zaidi.Kama huamini hivyo ni sawa Hakuna kuishi baada ya kifo. Lakini kama unaamini, basi jibu ni Ndio kuna maisha baada ya kifo.
Maana ya kufa ni pale Kitendo cha mwili kutengana na Roho iliyo ndani mwako. Ni pale mwili wako unapotwaa hali ya Umauti. Baada ya Umauti watu wenzako wanakufukia ardhini (wanakuzika) kwani huna tena maslahi/faida kwao. Mwili wako ni maiti na punde utaingia katika mchakato wa kuyarudia mavumbi(utaoza).

Roho sio kiumbe bali ni Nafsi hai au unaweza kusema roho ndiyo UZIMA.
Unaweza kunionyesha roho iliyo hai na yenye uzima?

Mwili ndio uzima wenyewe, na hata wewe uko hai sababu ya mwili wako uko hai sio roho.

Ukifa huna uhai tena.

Sasa eleza na thibitisha hiyo roho ni nini na wapi uli iona ikiwa hai?
 
Kama roho haionekani ulijuaje ipo?

Unasema roho haionekani kwa macho yetu haya ya nyama, Sasa
uliiona wapi na kujua ipo?

Au unaunda dhana za kufikirika tu?

Imaginations just an illusion.
Mkuu, sio lazima uone kila kitu ili uamini kipo. Hivi (kwa utani lakini) unapoongea na simu unaamini kwamba huyo unayeongea naye ndiye kweli yeye?
Kwa habari za roho mm naamini ipo kutokana na matendo yake yanayoonekana. e.g. Umewahi kujiuliza hivi Wale watoto /wanafunzi wanaokimbia-kimbia na kupagawa wanaona au wanasikia nini hadi wafanye hivyo? Nina hakika Umewahi kusikia mara nyingi watu wakisema ''Aisee, Huyo jamaa ana roho mbaya sana kaa naye mabali" Je, kwa nini wasiseme ana moyo mbaya? Hiyo roho wanamaanisha waliionaje/nini? hata wakaithaminisha (grade) kuwa ni mbaya?
Wewe kama ni mtu wa imani Mkristo, soma Math 15:18-20 i.e. "kile" kilicho ndani ya mtu kinajidhihirisha kwa matendo tunayoyaona kwa macho yetu kama ushuhuda.
Mkuu, inawezekana kabisa ninaunda dhana za kufikirika (Imaginations) lakini mm ninaamini sio mtu wa kwanza kukubali kwamba kuna kitu kinaitwa Roho.
Je mm ni mjanja kuliko hao wengine? Kila mtu anaweza kuamini kile anachoona ni sahihi au ni cha ukweli kwake.
Asante.
 
Unaweza kunionyesha roho iliyo hai na yenye uzima?

Mwili ndio uzima wenyewe, na hata wewe uko hai sababu ya mwili wako uko hai sio roho.

Ukifa huna uhai tena.

Sasa eleza na thibitisha hiyo roho ni nini na wapi uli iona ikiwa hai?
Mkuu, Nikuonesheje?
 
Hii Kwa wasioamini dini(wazee wa logic and seenable things)
💥Kama umezaliwa hukuwa unajua utaish ,vip useme hamna maisha baada ya kifo ,we unatakiwa useme tu sijui maana ukisema hamna maisha manake ushajua na una elimu ingali hujakufa ukafika huko ukapata experience.
Na usijiaminishee unajua kila ktu Mana Kuna vtu vingi tu vimewashinda mfano mpak leo hamuwez hta kutibu vidonda vya tumbo kwa logic zenu kazi tu kutupa miji-antiacid,cancer imewashinda pia manake kumbe mna upungufu wa elimu .so atheist mkiulizwa kuhusu kifo mjibu hamjui.
💥Wenye Imani zetu(mnaotukebehi mkatuita wafia dini).
Tunaamini maisha yapo kwa kutumia mitume na vitabu ambavyo vimeshushwa kutupa muongozo.
Mfano waislamu sisi Tuamini hivi kuhusu kifo:
a)siku yako ya kufa watakuja malaika wengne watasimama kulia kwako na kushoto kwako haf Yule anaetoa roho atasimama sehemu ya kichwa ataamuru roho itoke na ikitoka wale malaika wengne wataichukua na kuivisha vazi flani (halijulikan namna yake) Kisha watapaa na roho kuelekea mbinguni.
b)kwa sisi waislamu mbigu zpo tabaka Saba ,so watapaa kuelekea tabaka la Saba kuipeleke hyo roho ambapo Kuna vtabu viwil Cha watu wema na waovu,na kila mbigu Ina malaika ambapo roho inapokuwa inapitishwa huulizana Ni Nani (baadhi ya malaika watakutaja kwa jina lako ulokuwa waitwa duniani)Mana lile vazi roho huvishwa huwa na harufu mbaya kwa muovu na nzuri kwa mwema.
C)Kama Ni mwema roho huenda mpak tabaka la Saba na huuandikwa kweny ktabu kinaitwa "iliyyin" ktabu ambacho huuandikwa watu wema tuu. Kama muovu huishia mbigu ya kwanza tu na hutupwa ardhini Mana Allah ameahid milango ya mbigu haitofunguliwa kwa watu waovu(mbigu kiimani Zina milango Ila haimanishi Kama hii ya nyumbani Yani Ni jina tu lakushabihisha,NB:vtu vyote ambavyo vpo baada ya kufa havifanan na hivi vyetu Ila Ni majina tu ili tuelewe Mana hakuna aliyewahi viona kwa macho). kwahyo muovu ataandkwa kweny ktabu Cha waovu kinachoitwa "sijjin".
c)uwe muovu au mwema wote roho zao ztarudishwa ardhini kweny miili yao baad ya kuzikwa Mana Allah katika suratul-twaha amesema "kutokana na hyo ardhi tmuekuumbeni(Yani adamu Mana ya ndo wa kwanza na asili yetu) na humo tutakurejesheni na tutakutoeni kwa Mara nyengne Tena (ufufuo)".
Roho zikirudishwa Kuna malaika watakuja kaburini kukuuliza maswali matatu tuu 1.Nani mola wako 2.Muhammad Ni Nani 3.umemjuaje Muhammad.
d)Kama Ni mwema,atajibu maswali yote na atakapoulizwa amemjuaje Muhammad atasema alisoma Quran.
Hvyo malaika watamuonyesha Moto aloambiwa na pepo aloahidiwa na Yale matendo mema alofanya duniani yatamjia Ni Kama kiumbe flani umbile la binadamu ,Yani kitaumbwa kiumbe kibinadamu lakini Ni matendo yake mema ili kumfariji yeye na upweke. Basi mtu mwema ataomba kiama kisimame mana ameona mambo yote na yey Ni katika walofaulu ili alipwe pepo yake.
d) Kama Ni muovu atashindwa kujibu maswali Mana atapatwa na uoga na haya maswali hujibu kwa ujanja Bali vle we ni muovu au mwema tu, akiulizwa kuhusu Muhammad atasema alikuwa anaskia watu wakisema Yani hamjui ,hvyo malaika watamuadhibu vikali , na Kuna adhabu mbalimbali Kama Kuna majoka ambayo Kama sumu yake itafika ardhini hakuna mmea utaota na Ni wakubwa wanatisha na matendo yake maovu yataubwa kuwa kiumbe kitakacho muadhibu ,na ataomba kiama kisisimame Mana atonyeshwa Moto na utafunguliwa milango yake hivyo joto lake na mrindimo wake utamfikia.
💥Haya maisha ya Kaburini yanaitwa maisha ya barzakh na Ni endelevu mpak siku ya hukumu.
NB: 1.maelezo Ni marefu nkipata mda ntaandika Uzi wa maisha ya milele kulingana na Imani yangu Mimi inshallah.
2.namsikitikia mtu anaye tarajia kufa haamini chochote manake anakufa Kama mnyama ambaye Hana akili ya kufikirii , hajipangii future yake anasubir future impangie.
 
Wewe hapo ni sehemu ya babu zako na bibi zako wanaishi kupitia wewe hili ndo lenye uhakika kisayansi kwa sasa. DNA yako ikipimwa babu na bibi zako wataonekana.

Kifupi mizimu. Waliokufa walikuwa wanaishi ndani ya waliohai.

Isaya 26:13-14
 
Habari wana JF,

Hivi kuna maisha baada ya kifo?
Au bado sijui maana ya kifo?
Yaani babu yangu liyemzaa bibi yangu bado anaishi baada ya kufa? Kwamba hawa waliokufa wanaishi ila waneshakufa?

Au naombeni maana ya kifo ili ning'amue huu mzozo.

(Kuna mtu kaniambia kuwa kuna maisha baada ya kufa)
Kuna maisha baada ya kifo.

Atoms za mwili wako zitaendelea kuishi katika funza, mimea, etc.
 
Tuwaulize waislamu maana mada zao na wanavopenda kujilipua na hadithi za huko wakifa waje kutupa mrejesho
 
Habari wana JF,

Hivi kuna maisha baada ya kifo?
Au bado sijui maana ya kifo?
Yaani babu yangu liyemzaa bibi yangu bado anaishi baada ya kufa? Kwamba hawa waliokufa wanaishi ila waneshakufa?

Au naombeni maana ya kifo ili ning'amue huu mzozo.

(Kuna mtu kaniambia kuwa kuna maisha baada ya kufa)
KUNA MAISHA BAADA YA KUFA KWA MUJIBU WA VITABU VITAKATIFU

Kwa mfano, tunaposoma Injili ya MATHAYO 17:3-7 katika Biblia; tunajifunza kwamba mahali hapa, Mungu alituthibitishia juu ya maisha baada ya kufa.

Musa alikuwa amekufa yapata miaka 1,700 na Eliya alikuwa ametoweka yapata miaka 1,000, lakini hapa wanaonekana wakiwa hai. .

Yesu Kristo alitoa mfano wa waliokuwa kama Tajiri yule akiongea kule Kuzimu na Ibrahimu akiomba maskini Lazaro arudi duniani kuwashudia nduguze wasiende kuteseka motoni kama Yeye ! Hapa tunafundisha kuna maisha baada ya kufariki dunia tukirejea maandiko kitabu Injili ya LUKA 16:19-31

Pia tunajifunza kwamba mwili unaweza kufa na kuoza kaburini, lakini NAFSI YA MTU HAIFI bali inaishi milele (ZABURI 16:10)

Tukumbuke Mungu ni Mungu akazidi walio hai kule mbinguni alipo Yeye
na wakatifu wake (LUKA 20:37-38).

Ni hakika kuna maisha baada ya kufa (Soma UFUNUO 6:9-11; WAFILIPI 1:21-23)
 
Back
Top Bottom