Binadamu ana roho, na ukitaka kujua kama duniani watu huwa wanaoperate kiroho na kimwili, basi waulize wachawi, au kina mshana kama wapo humu watakuambia. roho ni real na mwili ndio huu unaouona. Kunga ulimwengu wa roho kabisa ambao waliokufa huwa wanaenda huko, ungalipo hai chukua hatua.
kwenu ninyi ambao hamjaokoka, hivyo hivyo ulivyo Mungu atakupokea na atabeba mizigo yako yote, sali sala hii pamoja na mimi:
Eee Mungu wangu, mbele zako mimi ni mwenye dhambi, ninaamini ulimtoa Yesu Kristo alikufa kama kafara kwa ajili ya ukombozi wangu, naomba unisamehe, uniokoe kuanzia leo, mimi niwe mali yako, futa jina langu katika Kitabu cha hukumu, andika jina langu katika Kitabu cha Uzima cha Mwana Kondoo Yesu Kristo, Katika Jina la Yesu! Amen.
hivihivi kimchaezo mchezo umeshaokoka, acha dhambi, kimbia dhambi na jiunge na wale waliookoka ili mmwabudu Mungu pamoja. Ubarikiwe.