Sina haja ya kutembelea Gamboshi, tunaye mtu huko Gamboshi ni kwao yuko hapa anakwambia hizo habari za kwamba Gamboshi kuna uchawi ni hadithi za watu tu.
Yani kama wewe umeanza kuisikia Gamboshi ukubwani kwenye stories za vijiweni, yeye huko ndiko familia yake walipotokea.
Tatizo, ukishaanza na imani ya uchawi, ukiona story yoyote ambayo huna uhakika nayo, huielewi, haijathibitishwa, unaikubali kama uchawi.
Nimekuuliza, ukiona kitu ambacho unafikiri kipo nje ya kanuni za physics, utajuaje huu ni uchawi, na si kanuni za physics ambazo wewe huzielewi tu?Au hadaa za watu tu? Hujajibu maswali haya kabisa.
Haya ni maswali ya msingi sana, ukiacha kuyajibu unanionesha kwamba unabishana kishabiki, unatetea upande wako, huna nia ya kuchunguza mambo kwa kina na kupata ukweli.
Ama hivyo, ama huyaelewi maswali haya na umuhimu wake, jambo ambalo linanipa shaka sana kama mazungumzo na wewe yatakuwa na tija yoyote.
Unajuaje huu ni uchawi ulio nje ya kanuni za physics, na huu si uchawi, ni mambo yaliyo ndani ya kanuni za physics tu, kwa kanuni z aphysics ambazo sijazielewa bado? Hujajibu swali hili.
Unajuaje huu ni uchawi, na huu ni mchezo wa hadaa za walimwengu tu katika jitihada za kupambana na hali zao na kupigana pesa? Hujajibu swali hili.
Unaongelea data, huwezi kwenda kukusanya data bila ya kujua scope, bila kujua kipi kiko nje ya kanuni za physics na kipi kinaweza kuwa ndani lakini wewe hujazijua tu hizo kanuni.
Unakusanya vipi data wakati hujui hata mipaka ya kukusanya data iko wapi?
Unayaelewa haya maswali? Au unajibu kibishi tu kwa kutetea upande wako?
Nyani Ngabu