Hivi kuna Mganga anayeweza kumuua Mchawi?

Hivi kuna Mganga anayeweza kumuua Mchawi?

WatesiWETU

Senior Member
Joined
Jan 2, 2022
Posts
106
Reaction score
248
Habarini wana JamiiForums,

Nimejaribu kujiuliza maswali, Kuhusu Uchawi na Uganga, sasa nikaja kugundua kwamba Hakuna Mganga asiye Mchawi na ingawa siyo wachawi wote ni waganga.

Sasa kinacho nifanya nije kwenu nikujua wataalaamu wa haya maswala kama wanaweza nipa Jibu ya swali langu, Kwamba Inawezekana kweli kukawepo Mganga ambaye anaweza kuwauwa wachawi? Maana mganga ni mchawi mwezao na kinachozidi tu ni kuwa mganga ana kipawa cha kutafuta dawa za tiba za miti shamba ila mchawi hawezi, sasa najiuliza ikiwa mganga ni watiba je anawezaje kuuwa Mchawi ikiwa nayeye ni mchawi je ana uwezo gani wazida zaidi ya miti shamba ya kutibu uchawi ulio fanywa na wachawi wenzake?

Kwanini nimewaza hivi ni jinsi ambayo unaweza kwenda kwa mganga aka kwambia ulichofanyiwa ila kamwe hata kwambia ni nani kafanya ikiwaaliye fanya ni mchawi ila kama aliye fanya siyo mchawi anakutajia jina la yule aliye kuendea kwa mganga kukuloga.

Sasa Basi kwa wale wajuzi wa mambo Naombeni mniambie kuna mganga yeyote hapa Tanzania mwenye uwezo wa kuuwa mchawi?

Asanteni.
 
Swali lako ni SAwa na kusema hivi jambazi anaweza muua police. Police na majambazi wanafahamiana vizuri. Police anawajua wezi, vibaka na majambazi wote wa mtaa, au mji mzima.
Hivyo hivyo vibaka majambazi wanawajua na wanawatambua askari wote kwa majina na sura hata wakivaa kiraia. Mchawi na mganga ni ndugu boss wao ni mmoja. Wote wanauwana ni timing tu mchawi akimuua mganga anapanda cheo, mganga akimuua mganga mwenzake anachukua nguvu zake. Wachawi wanawaua waganga wanaozuia mtu wamtakae kumroga kama kawekewa kinga na mganga.
Kiujumla kwenye ulimwengu huo wa giza wanaishi kwa kuwindana kugombea umiliki wa anga kama ilivyo fisi na simba KILA mmoja anamla mwenzake akizidiwa nguvu. Maadamu wanakula nyama hawana tofauti na wanyama pori walao nyama. Wanyama walao nyasi ndio waliostaarabika.
 
Yesu aliwahi kujibu hili mayahudi walipomzushia kwamba anatoa pepo kwa kutumia nguvu za beelzebul........akasema kwamba shetani hawezi kumtoa shetani mwenzie. Sasa hao wote, waganga, wachawi, walozi, wanga, wafanya matambiko, waliosimikwa uchifu mkuu wanafanya au wanashiriki nguvu za giza, kwa hiyo wote ni 'manzi ga nyanza' wote wanasubiri hukumu yao pamoja na mkuu wao ibilisi siku ya kiama......​
 
Habarini wana JamiiForums,

Nimejaribu kujiuliza maswali, Kuhusu Uchawi na Uganga, sasa nikaja kugundua kwamba Hakuna Mganga asiye Mchawi na ingawa siyo wachawi wote ni waganga.

Sasa kinacho nifanya nije kwenu nikujua wataalaamu wa haya maswala kama wanaweza nipa Jibu ya swali langu, Kwamba Inawezekana kweli kukawepo Mganga ambaye anaweza kuwauwa wachawi? Maana mganga ni mchawi mwezao na kinachozidi tu ni kuwa mganga ana kipawa cha kutafuta dawa za tiba za miti shamba ila mchawi hawezi, sasa najiuliza ikiwa mganga ni watiba je anawezaje kuuwa Mchawi ikiwa nayeye ni mchawi je ana uwezo gani wazida zaidi ya miti shamba ya kutibu uchawi ulio fanywa na wachawi wenzake?

Kwanini nimewaza hivi ni jinsi ambayo unaweza kwenda kwa mganga aka kwambia ulichofanyiwa ila kamwe hata kwambia ni nani kafanya ikiwaaliye fanya ni mchawi ila kama aliye fanya siyo mchawi anakutajia jina la yule aliye kuendea kwa mganga kukuloga.

Sasa Basi kwa wale wajuzi wa mambo Naombeni mniambie kuna mganga yeyote hapa Tanzania mwenye uwezo wa kuuwa mchawi?

Asanteni.
Waganga wote makanjanja tu

Sasa tazama wale wa puuzi wa ile kesi ya mauaji like moshi ..waganga baadae ya kila Pesa ya mteja wakatekeleza mauaji
 
Mganga na mchawi wote wana maarifa sawa, wanaenda shule moja, mwalimu wao mmoja, kozi moja, darasa moja, mitihani yao ni sawa, tofauti ni kwamba mganga amechagua kuondoa nadhara wakati mchawi amechagua kuleta madhara
 
Daktari

Daktari anaweza kutengeneza ugonjwa na kutibu ugonjwa.Anajua jinsi malaria inavyotengenezwa na namna ya kuindoa.Ukikuta daktari sio muadilifu anaweza ku inject virus au kutengeneza ugonjwa basi hapo tunasema daktari anafanya uharibifu kwa lugha nyingine kawa mchawi..

Na yule anayeambukiza gono na magonjwa mwngine huko mtaani basi huyo ndo mchawi.

Kifupi mganga anaweza kuwa tabibu na mchawi ila mchawi yeye kaamua kuwa muharibifu tu moja kwa moja
 
Naombeni mwenye taarifa ya Bibi wa Ngenda, Lindi anipe nataka kufika uko..

Naambiwa hakuwa na number zamani ila nahisi huenda ashakuwa nayo na pia kama hana mwenye taarifa ya kufika uko anisaidie nafakaje..

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mganga na mchawi wote wana maarifa sawa, wanaenda shule moja, mwalimu wao mmoja, kozi moja, darasa moja, mitihani yao ni sawa, tofauti ni kwamba mganga amechagua kuondoa nadhara wakati mchawi amechagua kuleta madhara
Aisee....
 
Aliye fanikiwa ku wauwa wachawi.. ajitokeze anisaidie Number za mtaalamu.. maana kuna watu wanacheza na familia yangu kimazingara.. Maombi yamewashindwa hawa mbwa dawa ni kuwaangamiza tu.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom