Mganga na mchawi wote wanatoa nguvu zao toka chanzo kimoja. Hawawezi kuhitilafiana maana wanajenga ufalme mmoja wa nguvu za giza.
Yesu aligusia hili na kusema Shetani hawezi kumtoa shetani mwenzake....kama ingelikuwa ni hivyo, Ibilisi angesimamishaje himaya yake? Hii ni baada ya baadhi ya wayahudi kumtuhumu kuwa anatoa pepo kwa njia ya Beelzebub mkuu wa pepo....yaani walimaanisha Yesu anatoa pepo kwa kutumia nguvu za giza.
Inahitajika nguvu kubwa zaidi independent ya ile ya Ibilisi ili kuweza kumshinda shetani na mawakala wake kama waganga au wachawi. Nguvu hiyo ni ya Mungu pekee.
Si kweli kwamba mganga na mchawi wanatoa nguvu zao toka chanzo kimoja. Waafrika tumeaminishwa na wazungu kuwa Uganga ni kitu kibaya na kinatoka kwa shetani. Kwanza ni vema kujua tofauti ya uganga na uchawi. Hivi ni vitu viwili tofauti.
Mchawi yupo kwa ajili ya kuangamiza, kuharibu, kutia mikosi, na hata kuvuruga mambo mema. Kwanini? Uchawi ni roho ya uharibifu toka kwa shetani.
Uganga ni nini? Ni uponyaji, urejeshaji, ujengaji, uuwishaji, utabibu, na urekebishaji. Ndo maana kwa kiswahili asilia daktari anaitwa mganga. Ndo maana tuna Mganga Mkuu wa serikali, Mkoa na kadhalika. Neno Daktari si kiswahili.
Uganga ni utaalamu ambao uhitaji mafunzo ya muda mrefu, ambayo uhusisha utaalamu wa kibaiolojia na kikemia, kwa kutumia mimea kuweza kutibu wanyama, binadamu na hata mimea yenyewe. Utaalamu huu uambatana na kujua saikolojia ya mwili wa binadamu, wanyama na mimea yenyewe.
Nitajikita katika Uganga asilia wa utabibu, ambao upo kila sehemu duniani. Uganga asilia uhitaji mafunzo ya muda mrefu, na umejikita zaid ktk matumizi ya mimea. Mtu aweza jifunza unganga kupitia kwa mtu akimuonesha aina tofauti za mimea na namna inavyoweza kutibu magonjwa mbalimbali.
Mara nyingi uganga huu uambatana na nguvu za kinyota, uwezo wa kisaikolojia, ramli, nguvu za asili za ukoo au miujiza. Uganga haupo kuuwa wala kuangamiza. Bali utokea tu pale kuna ulazima wa kufanya hivyo, na mara nyingi utoa onyo mara kadhaa kabla ya kuangamiza au kuuwa. Na hii itafanyika kama kuna jambo au tukio lililoumiza zaidi.
Tofauti ya Uchawi na Uganga, mchawi hawezi tibu, bali ni kuangamiza. Na mchawi asilimia kubwa nguvu zake ni za giza. Hakuna upatano baina ya mganga na mchawi. Ndo maana wachawi wengi hujitahidi waangamize mganga au kuuwa. Waganga kutokana na nguvu kadhaa za kiroho, kiukoo, uweza kuzuia nguvu za kichawi. Kuzuia huku hakuwafanyi wao kuwa wachawi la hasha!
Uganga unatofautiana, kwakua swali ni iwapo mganga anaweza muuwa mchawi nitajibu kwa mlengo huo. Mganga mwenye nguvu, anauwezo huo. Ila hafanyi tu kuuwa kama mchawi anavyo fanya. Mganga atauwa mchawi kama mchawi kafanya jambo baya la kuumiza na kuleta masononeko kwenye jamii au familia.
Na mara nyingi mganga atatoa onyo ili muhusika au mchawi ajisalimishe na kutubu. Inaposhindikana ndo hapo mganga atauwa mchawi. Na wakati mwingine kama mganga ajafurahishwa basi uamua kumuuwa mchawi bila kuonya iwapo huyu mchawi atajiona yeye ni yeye.
Tukumbuke swala la kuuwa, hata madakitari wetu wanauwezo wa kuuwa mtu wanapoona kunahitajika. Hivyo nguvu za uuaji zinatofautiana.
Mchawi uchukua muda mpaka kumuuwa mtu. Uanza kumroga na kuleta mikosi kwa huyo mtu. Ushindana na roho au nyota ya huyo mtu hadi kummaliza. Niliambiwa mchawi uondoa roho ya mtu wakati wa jua na si usiku. Usiku anautumia kulegeza nguvu za kiroho alizo nazo mhusika.
Ni mara chache inatokea akikuua usiku, ila roho yako itaondoka wakati wa jua.
Katika maisha yangu, nilishuhudia mganga mmoja, ambae waliuwa mwanae. Huyu mganga aliumia na kutamka. waliofanya hivyo wote watakufa. Na kweli hawa wachawi walikuwa kumi walioshirikiana kuuwa. Mmoja baada ya mwingine walianza kuumwa. Nakumbuka kuna mchawi mmoja hakuwahi kufahamika ni mchawi. Yeye alikuwa na dawa ya kuoga akiroga uchawi utaonekana kwa mtu mwingine si yeye. Hivyo walipokuja waganga kutambua wachawi yeye hakutambulika. Bali uchawi wake aliuweka kwa mchawi mwingine alie tambulika.
Lakini kwa huyu mganga alinasa, aliumwa na kuanza kwenda kwa wanganga kutafuta dawa, kila alipofika kwa mganga fulani aliambiwa umechezea sehemu mbaya, utakufa. Hatuna dawa ya kukutibu. Hospitali na kwa waganga ilishindikana. Nikimtembelea huyu mchawi, alitia huruma. Aliongea kwa shida huku machoni akiwa na aibu kubwa. Tulijuana nae kwa miaka kadhaa na alikuwa mtu mwema kwangu. Ndo maana niliona nikamjulie hali.
Lakini siku Mganga huyu anafanya yake ili waliomroga mwanae wafe nilikuwepo. Tulienda nae wote eneo la kaburi. Wala hakutumia uchawi. Sipendi kusema hapa namna alivyofanya wachawi wote kumi wakafa. Ila niseme Mganga mwenye ujuzi wa hali ya juu, ambae yupo kwa tiba tu na kinga anauwezo wa kuondoa uhai wa mchawi kama kuna jambo la kuumiza limetokea na hatumii uchawi!
Waganga wengi wananguvu za kiroho, wanalindwa wasipate athari za kichawi kwa nguvu ambazo wao wamekingwa nazo. Ila mchawi akikuta mganga ambae si imara na huyu mganga anazuia mchawi huyo asifanye mambo yake basi mchawi anauwezo wa kumroga au kumuuwa mganga.
Mganga mara nyingi uletewa jonzi au maono, ndo maana anajua mambo kadhaa. Ila mchawi hana jonzi au maono anaporoga. Yeye inambidi ajibadilishe, awe kwenye mfumo wa roho chafu, au awe katika maumbile mengine ili akaroge.
Ni mara chache mganga anaweza akaingia ktk ulimwengu wa roho akapotea usimuone. Hii hutokea pale tu kuna jambo maalum mganga inabidi afanye. Na hii uwezeshwa na nguvu za kiroho alizonazo.
Waganga wana mengi mazuri shida fani imeingiliwa na matapeli. Waganga wengi wazuri hawahitaji fedha. Na wanajua mambo mengi, dawa nyingi. Na hawa mchawi hawezi kuwagusa. Wanaweza kukupa kinga ya mchawi asifikirie kukudhuru, au akitaka kukudhuru hakuoni. Hawa waganga hawapendi kuuwa kabisa.
Mganga na mchawi ni vitu viwili tofauti. hata majini hayapendi wachawi. Yaani ni uadui mkubwa. Ni kwanini Majini ni adui wa uchawi? Ni somo refu linahitaji muda.
Na katika uganga, upo wa majini, yaani umetokana na majini. Upo uganga umetokana na mizimu katika koo. Upo uganga unaotokana na mashetani, niseme huu mara nyingi si mzuri unakonekisheni na nguvu za kichawi.
Uchawi nao unatofautiana, kuna wanga, hawa mara nyingi hawana madhara, wanacheza tu, wakija kwako usiku ni kukubeatua kukusumbua yaani vituko vya kila aina. Lakini Mchawi halisi huyu anaroga, anauwa, anaharibu na kuangamiza. Huyu ni hatari sana kuliko mwanga wa kawaida ambae mara nyingi ni kucheza na kukusumbua tu. Hawezi kukuua.