Hivi kuna Mganga anayeweza kumuua Mchawi?

Bro nimeku inbox.. tafadhali pitia ombi langu uko dm kwako..
 
Hizo ni falme za giza. Ni sawa na fisi na simba ni suala la timing tu
 
Karibu katika chuo chetu cha ushirikina tandika.
Utajua maswqli yote ulonayo.

Wanadamu mu watu wa ajabu sana yani maandiko mnayo ila hamjui chochote mbona sisi watu wa kushoto tunajua yenu na yetuu?
 
Mbona kama mu weupe sana.
Anaetaka kujua haya mambo kwa kina anitafute inbox hapa sitoweza kuandika yote vingnevyo niandike makala maalumu na siku nkiwa na muda
 
Bro nimeku inbox.. tafadhali pitia ombi langu uko dm kwako..
Mbona unaemwambia umesha mtext ka mweupe sana katika haya mambo?
Ya Mungu hajua na yashetani hajui sasa yuko upande upi
 
Hakuna uchawi wala haujawai kuwepo....
Mkuu mbona kama u mweupe sanaa yan ya Mungu hujui pia ya shetani?
Maandiko yanaeleza bayana habari zabuchawi na ushirikina na baadhi ya watu waloufanya sasa we hata hilo hujui
 
Nitafute kwa wakati wako nkupe tofauti zao pia nkupe kufanana kwao
 
Perfect mkuu.
Ukimwengu wa pili unaufahamu
 
Mganga na mchawi wote wana maarifa sawa, wanaenda shule moja, mwalimu wao mmoja, kozi moja, darasa moja, mitihani yao ni sawa, tofauti ni kwamba mganga amechagua kuondoa nadhara wakati mchawi amechagua kuleta madhara
Nyongeza mkuu. Walosoma darasani waloishia njian yan miaka minne wao hujua kuharibu zaidi ila alomaliza miaka yote saba anajua kuleta madhara na kuagua.
Mganga yoyote ili ajue kuagua lazima ajue aina ya uchawi ulofanyika na ndo maana mganga anakuwa na vitu viwili vya ziada yani kuagua pia kuloga pindi akitaka

Mganga ni aliye na taaluma zote mbili yan kuagua na kuloga
Mchawi anataaluma moja tuu yani kuloga

Japo kunawaganga wakiwa na njaa ya hela huwa huwaloga baadhi ya watu ambao waliwahi kufika kwao ili warudi tena ili wawaague na wapate hela.
Kwenda kwa mganga ni kama kujiwekea maagano na kuweka bond na shetani

Kiufupi mganga hajawahi kuwa mzuri pia mchawi hajawahi kuwa mzuri.
 
Wote nguvu zao wanatoa kwenye chanzo kimoja
 
Fisi anaweza muua simba? Ukipata jibu umepata jibu la swali lako.
 
Hapa hatuongelei kuhusu tabibu wa hospitali au anaetumia miti shamba.

Anaezungumziwa hapa ni mganga atumiaye mashetani ktk tiba zake. Huyu na mchawi hawana tofauti yoyote. Wote wanatumia uchawi ktk kutibu ama kudhuru. Leo hii unaona matangazo kuwa mganga anaweza kufanya watu wakapendana ama kufarakanisha. Wangapi leo hii wanaenda kwa waganga kwa ajili ya kufarakanisha ndoa za watu ama familia ,mzazi na mwanae n.k

Mganga (atumiae mashetani wa kijini) ktk kutibu ni sawa na mchawi atumiae mashetani wa kijini ktk kudhuru. Wote wana same background na lengo lao ni wanadamu wakufuru na kuwa washirikina kama walivyo wao.
 
Hujui chochote. Nimeaza kwa uchambuzi, nadhani kunashida ya uelewa. Ukakurupuka kupinga.

Neno mganga limetumika kama key word. Na elewa tunawanganga wa asili ambao wamejenga hospitali zao na wanaendesha matibabu kwa mfumo wa kihospitali . Na serikali inawatambua.

Pia tembelea Muhimbili, kuna kitengo cha waganga wa asili na dawa asili zinazotambulika. Hata NIMR wanatambua waganga asili na kufanya nao kazi katika tafiti.

Elewa kuwa hata hizi dawa za hospitalini ni miti shamba. Hivyo hakuna tofauti kubwa. Umekaririshwa na mkoloni kuwa unganga wa asili ni mbaya na uchawi. Kwanini muhimbili wakubaliwe.
Ndo maana nikafanya uchambuzi kwa uzoefu nilionao.

Hakuna mchawi anaetumia majini. Na tofautisha mashetani na majini. Kama hujui jambo uliza usipende kukurupuka kupinga uonekane nawe umepinga.
Kwa asili nimeeleza uadui baina ya jini na mchawi. Hawa hawapatani.
Nakuona hujui chochote juu ya hii mada sipo hapa kushindana. Nimeeleza niliyoyaishi.
 
wapo wengi tu.anamfuta fasta ,Ila mpaka huyo mchawi ,awe amekuzingua .Ili mganga apate kibali/sababu ,bila kuwa na sababu hawezi!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona unapayuka na kupaniki mdogo wangu ...nimeshafanya kazi huko NIMR unapopaongelea na nadhani unachanganya mada hapa.

Sijakataa utabibu /uganga unaohusisha miti shamba, asili ya dawa karibu zote zinatokana na miti. Ninachopinga ni waganga waotumia mashetani wa kijini katika kuagua watu.

Mfano mdogo unaweza kunambia ni mti gani unaotumika na hawa waganga kupiga ramli?

Pia ukija kwenye mada kuhusu majini vilevile utakaa? Hakuna sehemu niliochanganya kuhusu mashetani ba majini.

Majini ni viumbe vilivyoumbwa kwa miale ya moto, na ushetani ni sifa ya kiumbe muasi aliyekengeuka kwa mola wake,shetani anaweza kuwa mwanadamu au jini!!! Nafahamu ninachokiongea kijana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…