Hivi kuna Mganga anayeweza kumuua Mchawi?

Uko vizuri. Ni wachache sana waliokuelewa. Wengine wanakurupuka tu.
 
Sijapayuka wewe ndo umepaniki. Hakuna kupayuka kwa maandishi, kupayuka inakuwa na sauti. Elewa matumizi ya maneno.
Kufanya kazi NIMR si kigezo. Wewe ndo ulikuja kwa maneno yasiyo na msingi. Hapa tukijitangaza tumefanya kazi wapi utashangaa.

Shetani ni shetani na jini ni jini. Kwanza uwezi mwona shetani, lakini waweza muona jini. Mara nyingi jini anaweza jibadili akawa kitu chochote. Lakini shetani ni roho chafu isiyoonekana.

Unaweza ukaishi na jini, ukamtuma kazi yoyote akafanya. Wapo majini wapole na wastaarabu, mpaka uwauzi ndo wanaweza kukutesa. Na ni marafiki. Na mara nyingi ili wawe rafiki na binadamu wanajibadili kuwa binadamu, mwaweza ongea vizuri tu. Nashukuru mara kadhaa nimeonana na majini. Ni rafiki wazuri.

Na ujue kuna watu baadhi ya maeneo wanafuga majini na kuishi nao.
Ila uwezi fuga mashetani.
Mashetani ni roho chafu zisizoonekana kwa macho ya nyama bali katika ulimwengu wa roho. Na masetani yapokuangamiza na kuharibu.

Narudia jini na mchawi hawapatani. Na jini hampendi kabisa mchawi.
So usilazimihe mambo usiyoyajua. Sema ufundishwe.

Kuna mizimu pia. Hii ni miungu. Ina nguvu za kimungu na uabudiwa. Zinauwezo wa kufanya lolote, kuangamiza au kubariki.
 
Mpaka hapo sina haja ya kuendelea na mjadala na wewe kwasababu unaonesha kujivunia ujinga wako hadharani.

Ngoja nikupe ilmu ndogo tu. Hayo maneno mawili Jini (jinni) na shetani (shaytwaan) asili yake ni kiarabu. Kwahiyo ili kuipata maana halisi ya hayo maneno ni lazima urudi kwenye lugha ya kiarabu ambayo nina uhakika kuwa huijui.

Jinni (jini) ni kiumbe aliyeumbwa na Mungu kabla ya mwanadamu na waliishi katika uso huu wa ardhi miaka mingi kabla ya kuumbwa kwa Adam. Asili ya maumbile yao ni moto wakati mwanadam asili yake ni udongo mweusi wa mfinyanzi.

Shetani (shaytwaan) ni sifa ya kiumbe muasi (mchochea maasi) , sifa hii anaweza kuwa nayo mwanadamu na vilevile anaweza kuwa nayo Jini.

Kwahiyo basi kuna mashetani wa kijini na mashetani wa kibinadamu vilevile. Majini wamegawanyika makundi mawili kuna waja wema na kuna mashetani (waovu), hawa mashetani kiongozi wao ni Iblis. Iblis anawatuma kuja ardhini kuchochea dhambi na uasi kwa wanadamu. Na pia mashetani wa kibinaadamu nao huwa ni mawakala wa iblis, anawatumia kuchochea maasi na uasi kwa wanadamu wengine.

Tukirudi katika point yako unayosema kuwa shetani haonekani na jini anaweza kuonekana, hapa sio kweli. Mashetani wa kibinadamu wanaonekana waziwazi ,wakati mashetani wa kijini wao hawaonekani.Mungu amemuwekea mwanadamu pazia katika macho yake asiweze kuyaona majini katika umbile lao ila mwanadamu anaweza kumuona jini pale tu jini atakapochukua umbile la mdudu au mnyama au mtu.

Jini anaweza kuchukua umbile la mbwa mweusi,ng'e,nyoka au hata umbile la mwanadam...hapa ndipo binadamu atakapoweza kumuona ila kwenye umbile lake halisi mwanadamu huwezi kumuona jini.

Ukimuacha Nabii Suleyman bin dawood hakuna mwanadamu mwingine aliyepewa kibali cha kuyamiliki majini na kuyatumikisha .Ukimuona mwanadamu anafuga majini na kuyatuma yamfanyie kazi jua kuwa huyo ni mshirikina na ni wakala wa Iblis. Majini hayakai kwa mtu ikiwa mtu huyo hayatumikii majini kwa kuyatolea sadaka ya vichinjwa n.k (kuyaabudu).
 
Hatuwezi kuelewana kwasababu ndani yako una imani ya kishirikina. Kitendo cha kusema kuwa mizimu ni miungu inaonesha kuwa hujui kitu na hujui hiyo mizimu ni nini! Pia tukirudi ktk suala unalodai kuwa jini na mchawi hawapatani ni uongo tu.

Majini wamegawanyika makundi mawilj , wapo waliomuamini Mungu na wapo waliomkataa Mungu.Kama ilivyo kwa wanadamu leo wapo wanaomuamini Mungu na wapo wanaomkataa Mungu.

Majini wasiomuamini Mungu ndio huitwa masheytwaan wa kijini na hawa ni marafiki kindakindaki na wanadamu wasiomuamini Mungu. Kama unavyoona mlevi rafiki yake ni mlevi mwenzie.

N wapo majini ambao ni wachamungu hawa nao ni marafiki na wanaadamu ambao ni Wachamungu na huwa hawaingilii maisha ya mwanadamu kama kumuingia mwilini na kumtumikisha. Wao wanaishi maisha yao kama wao ila hawa wasiomuamini Mungu ndio unaowaona wakiingilia maisha ya wanaadamu kwa kuwaingia kwenye miili yao na hata kuwadhuru. Pia huwatumikia wale wanaadamu ambao wamekubali kuwaabudu na kuwatii. Mfano humletea pesa na vito vya thamani mwanadamu ambae amekubali kuwatii,kuwaabudu na kuwanyenyekea.Pia huweza kutumwa kwenda kuwadhuru watu ambao wanatakiwa kudhuriwa na huyo mtu anayewafuga n.k

Mara nyingi majini yanayofugwa na mwanadamu huwa yamekimbia adhabu ujinini kutokana na makosa mbalimbali waliyoyafanya kama wizi,uuaji au ubakaji, so wanakuja nchi kavu kwa wanadamu na kuomba hifadhi kwa mwanadamu na mwanadamu huyo akikubali kuwapa hifadhi katika mwili wake na makazi yake ndio huahidi kumtumikia mwanadamu huyo kwa masuala nbalimbali.

Naongea haya nikiwa nishakaaa na watu wenye haya masheytwaan katika miili yao na hata kuongea na hayo majinj yenyewe.
 
nimemkumbuka dr manyaunyau na profesa maji maref
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…