Hivi kuna mradi mkubwa wa umwagiliaji kuliko wa Hombolo bwawani uliopo Dodoma?

Hivi kuna mradi mkubwa wa umwagiliaji kuliko wa Hombolo bwawani uliopo Dodoma?

Wakuu hivi ni maeneo gani ndani ya mkoa wa Mbeya wanafanya kilimo cha umwagiliaji
 
Natarajia kwenda mwez wa tano katkat khs namba hapana sina nilipoteza simu
 
Uje dakawa Moro... Nikupeleke utasema mm nalima au nacheza????? Hataliiii

mkuu miundombinu ya Hombolo huwezi fananisha na miundombinu yoyote Africa mashariki na kati,,,Muitaliano hatari sana
 
kabla ya kuongea fanya utafiti. Umefika lower Moshi irrigation scheme au Madibira Mbeya?


Sijafika ila kuna ndugu yangu yupo huku anaitwa Tarimo,katokea huko Moshi,amekiri kuwa huko kuna irrigation,ila hii aliyoikuta ni kubwa kuliko
 
Mleta mada mi naona ungeweka, vitu muhimu zaidi ya kutaka kujua tu kama kuna mradi mkubwa zaidi ya huu ulioueleza, tuwekee bei ya kukodi shamba na gharama nyingine pamoja na mategemeo baada ya mavuno, itasaidia kwa ataependa kuwekeza huko"


Mashamba yamegawanywa kimradi yani kuna A,B&C, hii ni kutokana na kuwa na urahisi wa kumwagia
shamba kukodi inategemeana na usafi au uchafu wa shamba
ila mara nyingi huwa haizidi 200,000

pata mda uje huku,then uwape mrejesho wenzako,kamwe hautojutia
 
Wakuu kama kuna yeyote humu anaepafahamu vizuri tafadhali atupe maelezo kwa kina ama kama kuna yeyote anaeweza kuwa mwenyeji wangu aje PM tuyajenge aliyeleta mada inaonesha kuna kitu hataki tukipate


Mkuu ni pm kama kweli una nia,mimi nitakuwa mwenyeji wako,then utawaletea mrejesho wenye wasiwasi
 
Ndugu ndani ya wiki hili nitafuatilia huu mradi kwa kina na nitaanika kila kitu ha jukwaani maana ni mradi nilioufikiria kwa muda

ukianza kuja ni pm mkuu kama utajali niwe mwenyeji wako
 
Ahsante ndugu...vp unaishi Mbeya pia
au unaweza niunganisha na mtu yyte anaetokea Ubaruku?
Kilimo cha umwagiliaji Ubaruku, Madibira na Kapunga zote ni za mpunga tu. Kilimo cha umwagiliaji ambacho si cha mpunga kinachofanyika Mbarali Mbeya unapoulizia ni cha bustani za mbogamboga ambacho kipo Igawa.
 
Mkuu nikitaka kulima mahindi yanakubali vzr hko?? Je nature ya umwagiliaji ikoje ni lazima niwe na water pump na mipira?
 
Wakuu hivi ni maeneo gani ndani ya mkoa wa Mbeya wanafanya kilimo cha umwagiliaji
Wilaya ya mbarali,
kata ya igawa,kwa kilimo cha vitunguu,nyanya,na mbogamboga nyinginezo kuna heka 2000 (igomelo scheme)

Kata ya Chimala,kuna heka 30,000 za kumwagilia ila mpunga (kapunga estates).

Mbarali estates kuna heka 15,000
Za kumwagilia

Madibira estates kuna heka 10,000 za kumwagilia mpunga

Miundombinu iko imara sana
 
Mkuu nikitaka kulima mahindi yanakubali vzr hko?? Je nature ya umwagiliaji ikoje ni lazima niwe na water pump na mipira?


Mahindi yanakubali tu vizuri,kuhusu kumwagia ukiwa na mpira wa Meter2 tu unatosha kaka,
 
Kuna story moja inadai kuwa watu wenye ulemavu wa macho siku moa walienda kutalii wakiwa na shauku ya kumjua tembo. Mmoja akapata bahati ya kumshika tumboni, katika kupapasa akawa hafiki mwisho, akaondoka akijua tembo ni kama ukuta, mwingine akapata bahati ya kupapasa sikio, akaondoka akijua tembo ni kama ungo.

Naifananisha story hii na baadhi ya wachangiaji wa mada hii akiwemo mleta mada.

Nadhani ingependeza mleta mada kueleza kwanza hilo eneo la hombolo hiyo skimu ina ukubwa gani, inahudumia wakulima wangapi? Chanzo chache cha maji na sustainability yake kwa mwaka mzima,

Wachangiaji wengine nao waje kwa fact za skimu wanazojua, MTU mwenyewe tu bila ushawishi atajua skimu IPI bora. Unless otherwise mleta mada anatafuta Wateja kwa aidha udalali au eneo lake, maana nilidhani anatafuta kujua ili kuongeza uelewa wa mambo. Maana huwezi sifia ubora wa kitu ukiwa huna fact za kukilinganisha na kingine!
 
Back
Top Bottom