Hivi kuna mradi mkubwa wa umwagiliaji kuliko wa Hombolo bwawani uliopo Dodoma?

Hivi kuna mradi mkubwa wa umwagiliaji kuliko wa Hombolo bwawani uliopo Dodoma?

Wilaya ya mbarali,
kata ya igawa,kwa kilimo cha vitunguu,nyanya,na mbogamboga nyinginezo kuna heka 2000 (igomelo scheme)

Kata ya Chimala,kuna heka 30,000 za kumwagilia ila mpunga (kapunga estates).

Mbarali estates kuna heka 15,000
Za kumwagilia

Madibira estates kuna heka 10,000 za kumwagilia mpunga

Miundombinu iko imara sana
Mkuu hii igomelo scheme nayo ni kwa ajili ya mpunga peke yake au?
 
Serikali Yatelekeza Mradi wa Milioni 750

Na Dotto Kwilasa, Dodoma

DIWANI wa kata ya Hombolo Bwawani Ased Ndajilo ameilalamikia serikali kwa kuutelekeza mradi wa umwagiliaji ambao uligarimu takribani milioni 750,195.

Hayo yalibainishwa jana na Diwani huyo wakati akizungumza na wandishi wa habari alipotembelea mradi huo ambao hutumia Makanareta kusafirisha maji kwenye mashamba ya wakulima wa zabibu.

Ndajilo alisema kuwa inasikitisha sana kuona serikali imeusahau kabisa mradi huo ambao hapo awali ulikuwa ukiwasaidia kupata mazao mengi zai na kuwafanya waufurahie mradi huo kinyume na sasa.

Alisema kuwa Makanareta hayo yalitengenezwa na Waitaliano mnamo mwaka1991 ambapo waliambiwa kuwa yatadumu ndani ya miaka 15 tu na baada ya hapo yatahitajika kutengenezwa mengine mapya .

“Waitaliano wametusaidia sana mpaka kufikia hapa tulipo hivyo tunaiomba serikali itusaidie zaidi ilitusiweze kuingia kwenye kilimo cha umwagiliaji ambacho kita mdhoofisha mkulima kiafya kwa kuchukua maji mbali yakuweza kumwagilia mazao”alisema Ndajilo.

Diwani alisema kuwa mradi wa umwagiliaji unategemewa na mashamba takribani 464 ambayo ni sawa na hekta 600 na Makaraneta hayo yameanza kuvunjika kutokana na kutumika kwa muda mrefu hali ambayo imesababisha wakulima kuanza kukata tama.

Alibainisha kuwa mradi huo umekuwa kimbilio la wakulima wengi akiwemo yeye mwenye ambao maisha yao yote yamejikita kwenye kilimo hivyo makaranata hayo yanapo endelea kuvunjika kilimo cha umwagiliaji kitakufa.

“Mimi pia ni mkulima inaniuma sana kuona makaranata yanaendelea kuharibika huku hakuna hatua zozote zinazo chukuliwa na serikali hali ambayo itasababisha kilimo cha umwagiliaji kutoweka katika kata yetu” alisema Ndajilo.

Aidha Diwani huyo alisema wakulima hawana ujuzi wa kuyatengeneza makanareta hayo kwani yana hitaji ujuzi wa hali ya juu ili yaweze kudumu miaka mingi kama yaliyotengenezwa na Waitalianao.

Naye mmoja wa wakulima anayetumia mradi huo Willisoni Nyamwale alisema endapo serikali haita litilia maanani jambo hili maisha ya wananchi wa kata hiyo yataendelea kushuka zaidi.

Hata hivyo Nyamwale alisema wanaiomba serikali iwaangalie kwa jicho la tatu kwenye mradi huo kwani ndio unaowasababisha vijana wengi kuepuka kufanya matendo maovu ikiwemo uwizi,uzururaji na

Mwisho.

(2)

Share this on WhatsApp

Categories: MAISHA
 
Kuna story moja inadai kuwa watu wenye ulemavu wa macho siku moa walienda kutalii wakiwa na shauku ya kumjua tembo. Mmoja akapata bahati ya kumshika tumboni, katika kupapasa akawa hafiki mwisho, akaondoka akijua tembo ni kama ukuta, mwingine akapata bahati ya kupapasa sikio, akaondoka akijua tembo ni kama ungo.

Naifananisha story hii na baadhi ya wachangiaji wa mada hii akiwemo mleta mada.

Nadhani ingependeza mleta mada kueleza kwanza hilo eneo la hombolo hiyo skimu ina ukubwa gani, inahudumia wakulima wangapi? Chanzo chache cha maji na sustainability yake kwa mwaka mzima,

Wachangiaji wengine nao waje kwa fact za skimu wanazojua, MTU mwenyewe tu bila ushawishi atajua skimu IPI bora. Unless otherwise mleta mada anatafuta Wateja kwa aidha udalali au eneo lake, maana nilidhani anatafuta kujua ili kuongeza uelewa wa mambo. Maana huwezi sifia ubora wa kitu ukiwa huna fact za kukilinganisha na kingine!
Naunga mkono hoja. ..awake FACTS ZA HOMBOLO NA HASA UKUBWA WA SCHEME YAKE ....
 
Nimeuliza na kujibu kwa uelewa wa wengine walio pendekeza miradi wanayoijua

mimi siyo dalali na wala sijawahi kufanya udalali,,kwa kifupi tu maji yanapotoka mpaka mashambani ni umbali km8+

kuna mashamba zaidi ya 300 yaliyotumiwa,kikubwa nilikua nauliza na kuonyeshana fursa kwa ambao wanapenda kilimo cha umwagiliaj
 
Habari wanajamvi,kama kichwa kinavyojieleza,ukitoa ule mradi wa mto Nile,
kwa hapa Africa kuna mradi mkubwa na ulio bora kuliko uliopo Hombolo bwawani Dodoma?

karibuni hombolo kwaajili ya kilimo cha umwagiliaji (Irrigation)
siyo zabibu tu,hata nyanya,bamia,mihogo,mbogamboga nk.
Kwa Wabongo huo ni mradi wa kupigia dili.
 
Habari wanajamvi,kama kichwa kinavyojieleza,ukitoa ule mradi wa mto Nile,
kwa hapa Africa kuna mradi mkubwa na ulio bora kuliko uliopo Hombolo bwawani Dodoma?

karibuni hombolo kwaajili ya kilimo cha umwagiliaji (Irrigation)
siyo zabibu tu,hata nyanya,bamia,mihogo,mbogamboga nk.
Habari.. ndugu bado upo Hombolo?
 
Back
Top Bottom