Kuna story moja inadai kuwa watu wenye ulemavu wa macho siku moa walienda kutalii wakiwa na shauku ya kumjua tembo. Mmoja akapata bahati ya kumshika tumboni, katika kupapasa akawa hafiki mwisho, akaondoka akijua tembo ni kama ukuta, mwingine akapata bahati ya kupapasa sikio, akaondoka akijua tembo ni kama ungo.
Naifananisha story hii na baadhi ya wachangiaji wa mada hii akiwemo mleta mada.
Nadhani ingependeza mleta mada kueleza kwanza hilo eneo la hombolo hiyo skimu ina ukubwa gani, inahudumia wakulima wangapi? Chanzo chache cha maji na sustainability yake kwa mwaka mzima,
Wachangiaji wengine nao waje kwa fact za skimu wanazojua, MTU mwenyewe tu bila ushawishi atajua skimu IPI bora. Unless otherwise mleta mada anatafuta Wateja kwa aidha udalali au eneo lake, maana nilidhani anatafuta kujua ili kuongeza uelewa wa mambo. Maana huwezi sifia ubora wa kitu ukiwa huna fact za kukilinganisha na kingine!