Hivi kuna mtanzania amewahi kwenda kutafuta maisha nchini India akatoboa?

Hivi kuna mtanzania amewahi kwenda kutafuta maisha nchini India akatoboa?

watanzania wengi naowasikia leo kuwa wapo nchi za Ulaya na Asia kuanzia miaka ya Mwanzoni ya 70, maka ya 60 na Kabla, elewa kuwa safari yao ilianzia bandari ya Dar kuelekea India.

Enzi hizo usafiri pekee wa rahisi na urahisi wa kuchomoka Tanzania / Tanganyika ulikuwa kupitia Inda kwa meli mbili marufu ziizokuwa zikija Dar, nazo n MV Karanja na MV Haryana.

Mabaharia walioelekea Ugiriki enzi hizo hiyo ndiyo ilikuwa route yao kuu.

Licha ya hayo. India na Bandari za Tanzania zina maingiliano na uhusiano mkubwa Kihistoria wa kibiashara kabla sana ya ujio wa wakoloni wa kizungu.

una kabila la Kiafrika India na Pakistan ambalo kwa asilimia kubwa asili yao ni Afrika Mashariki.

Bila kutafuna maneno, kumbuka kuwa una wajomba na shangazi zako huko Kihistoria kuna mpaka tawala za Kiafrika, India.
 
Sijawahi kusikia nilokwenda kule kikazi mwaka jana sasa kwenye hoteli niliyofikia mlinzi wa pale hotelini akaniomba nimfanyie mpango wa yeye kuja Tanzania kufanya kazi ya Ulinzi, nilimjibu haiwezekani.
Nikamuuliza mshahara wake nakumbuka ilikuwa kama rupee elfu 80 kama laki 2 na nusu ya kibongo nikamjibu huku Tz mshahara ni kama huo ila kwa mhindi hawezi kukubaliwa kuwa mlinzi Tanzania labda kwa professionals.
Jamaa alisikitika sana kwa mimi kukataa kumsaidia kuja bongo kuwa mlinzi.
Kule maisha ni magumu sana kule kuna maskini huku bongo hakuna maskini kama wale .
Kule kuna watu ukoo mzima haumiliki hata kijipande cha ardhi hata vijijini.
Huku bongo unakutana na maskini ila ana miliki ardhi huko kijijini kwao ,kule hakuna .
Kuna siku nilitembelea ubalozini nikakutana na dada wa kibongo analia kwamba alidanganywa kuna kazi akapelekwa kule akaishia kwenye danguro akawa anafanyishwa kazi za sex halipwi chochote zaidi ya kupewa msosi.
Siku hiyo alibahatika kutoroka akakimbilia ubalozini passport hana walikuwa wamemnyang'anya ubalozi ndio ukawa unawasiliana napolisi waende kuchukua passport yake.
Kali kulipo yote hapo ubalozini siku hiyo nikakutana na mhindi mbongo .
Huyo mhindi mbongo alikwenda India kusalimia bibi yake alikuwa mgonjwa sasa akakaa hadi passport yake ya kibongo ikaexpire sasa akawa anataka atengenezewe passport nyingine na ile fomu kuna sehemu inatakiwa ijazwe na mdhamini ambaye lazima awe mbongo akawa ananiomba nimjazie nikawauliza wale maofisa wa ubalozini kwa nini wasimjazie wao wakanijibu wao hawaruhusiwi. Wale maofisa waliniomba sana nimsaidie eti ni mtanzania mwezangu nilimjazia kwa shingo uoande sana manake ninavyowachukia wahindi basi tu.
Ila jamaa alikuwa anaongea kiswahili fresh aliniambia anaishi mitaa ya kariakoo.
Jamaa anakwambia mishe zake zote ni bongo kule hapafai.
India asikwambie mtu ni nchi moja ya hovyo sana ila wanaigeria noma wale jamaa niliwakuta kule hadi wana maduka na vimgahawa wanakomaa na wahindi .
Siwezi kamwe kumshauri mtu aende India kutafuta maisha
Wanigeria ni World wide wameshindikana.

Wao wana long plan kwenye maisha, kama ukifika Brazil sasa hivi wanigeria ni kiwanja chao na wana biadhara zao.

Halafu wale usione vile anaweza kukaa nje ya kwao hata miaka 20.

Mimi kuna Mnigeria nilikutana naye Sao Paulo ananiambia pesa anatumiwa kutoka kwenye asset zake za real estate kwao Nigeria, kwahiyo yeye kuchukuwa appartment na kuishi peke yake siyo issue jibu la mwisho utasema ni drug dealer lakini siyo Wanaigeria wote wanadeal na unga, wapo kwenye sanaa nyingi tofauti.
 
Tulikua kijiweni tunapoteza muda,jamaa mmoja akatuambia anataka ajilipue aende India kutafuta maisha.
Nikawaza,then nikaingia youtube kucheck maisha ya wahindi wenyewe tu huko India ni mara mia ya hapa kwetu.
Hivi kuna mtanzania aliwahi kwenda kujitafuta India akatoboa?
Tupo
 
Tulikua kijiweni tunapoteza muda,jamaa mmoja akatuambia anataka ajilipue aende India kutafuta maisha.
Nikawaza,then nikaingia youtube kucheck maisha ya wahindi wenyewe tu huko India ni mara mia ya hapa kwetu.
Hivi kuna mtanzania aliwahi kwenda kujitafuta India akatoboa?
Wenyewe wamejazana bongo wanatafuta maisha.. Labda ukatafute umaskini
 
Back
Top Bottom