Majini ni malaika waasi kwa Mungu. Ni roho, kwa mujibu wa Biblia majini ni wawakilishi wa shetani, shetani hana lolote jema kwa mwanadamu, shetani akikupa kitu na mkono wa kulia anachukua kitu ndani yako kwa mkono wake wa kushoto. Anaweza kukupa pesa na vitu vingine unavyo tamani lakini hawezi kukupa amani, amani ni kila kitu kwa mwanadamu, Bora ukose vyote lkn uwe na amani kwakua hata pesa tunazitafuta ili tuwe na amani. Mwisho wa uhusiano wowote na majini ni mauti na moto wa milele jehanamu. Mpokee Yesu awe Bwana na mwokozi wa maisha yako, naye atakupumzisha mizigo yako