Hivi kuna mtu bado anazipuuzia English medium schools?

Hapana sijui mkuu, naona tutakesha mana unaaminisha uko bright kumbe tayari una kisasi cha kusoma kayumba na si kuongea uhalisia
Waliopeleka watoto wao English medium huwa nawacheka kwa upeo mdogo wa kutochanganua mambo wamenaswa nakuingizwa kwenye mfumo wa marketing wa English medium na kuaminishwa kuwa ni shule bora wako mmojawapo ni wewe hapo uliyedanganywa kuwa English medium kuna elimu bora.
Wewe ulishawahi kuishi na watu wanaozungumza English kama lugha yao ya kwanza?Je English yao inafanana na ile ya English medium?
 
NIMEKUSHTUKIAAAAAAAAAAA HAHAHAHAAAAAAAA🀣🀣🀣🀣🀣 UNA HASIRA ZA WATOTO WAKO KUSOMA KAYUMBA HAHAHHAHAHAAAAπŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜† SINA CHA KIKU SHAURI TAFUTA HELA MKUUUUU KACHUMBALI SIO MBOGA HAHAHAAAAAAAAAAAAAA UNAJIZUNGUSHA KUMBE UNA HASIRAAA ZA WATOTO WAKO KUSOMA KAYUMBA. KAKA ANZA NA KILE ULICHO NACHO KAKA NDIO MAISHA USITUKANE NDIZI KISA HUNA UWEZO WA KUZIFIKIA, HAHAHAAAA UMASIKINI BHANA
 
Achana huyo mjinga mtandao kama Quora si wa wahindi mbona hawakitumii hicho kipindi?
 
Kwamba ada ya milioni 2 inanishinda ama?Hebu fanya hivi tafuta nauli utembelee hata Uganda tu hapo watoto wanaongea English pure hata kabla hawajaanza shule,mabibi wa mashambani huko wanaongea fluent English ili uondoe ushamba wa kudhani kujua kiingereza ni dili.
Nimegundua hapa napoteza muda wangu kubishana na mtu ambaye ana zero exposure.
Hapa ninapoongea na wewe niko na waganda kwenye meza moja wengine hawajaenda shule kabisa na wanaichapa hiyo lugha kama wamezaliwa nayo ingekuwa hapa JF kuna sehemu ya kurekodi sauti ningewahoji nikurekodie sauti zao.
 
Lakini kinachoongelewa hapa sio mtu kujua Kingereza maana hata mtoto anaweza kujua kuongea Kingereza hata bila kwenda shule.

Hapa tunaongelea mtu akiwa ana elimu ni vema akajua Kingereza maana ni lugha muhimu kwenye dunia ya sasa.

Wewe unakuja na arguments zako zisizo na kichwa wala miguu na kutaka kutiaminisha kwa vile ulikutana na Waganda wa kijijini aanaongea Kingereza basi hakina maana.

Nikutaarifu tu Kingereza ni lugha kuu ya Kibiashara na kielimu duniani na zingine ndo zinafuata wewe baki na unachokiamini.
 
Kaka unani chosha mbona kila kitu tusha zungumza huko nyuma, tumesema kuongea kingereza ni jambo lingine kuongea fact ni jambo lingine ukatolewa mfano hata Masai wa Zanzibar wanaongea kingereza lakini changamoto ni wao kutokua na ufahamu wa kile wanacho kiongea, nikakupa mfano unaweza enda Zanzibar Kwa wale Masai wanatamka water wakijua ni maji changamoto ina kuja pale unapo waambia waiandike hiyo water kasheshe huanzia hapo
 
Nashindwa kuwaelewa mpo busy kuzizungumzia Nchi zilizoendelea wakati ninyi ndio kwanza mnajengewa vyoo kwa msaada wa Germany..
Dunia ya leo unaponda Lugha aisee utakua na shida sio bure lugha yeyote inasaidia sana kwa mawasiliano au muingiliano na jamii ingine korahisi hasa kwa watu wanaotoka Nchi masikini.
 
Kujua Lugha ni exposure kubwa sana hao Waganda ndio walikua wanamiliki shule nyingi SA hata yule mke wa Diamond waliechana nae alikua na shule kibao baadae wakaanza kusumbuliwa kuhusu vyeti ndio ikawa shida lugha ni kigezo muhimu cha kujichanganya na watu popote pale kirahisi..
Ukimuona mtu anaponda Lugha iwe kiiingereza,Germany,Kichina na Kireno jua ana matatizo sio bure Arusha watu wanaishi kwa sababu ya Lugha tu kuwapeleka wageni porini na kuwaeleza kwa lugha yao harafu upo busy unaona haina maana aisee..
 
Kaka huyu jamaa simuelewi hata
 
Nimemwambia huyu jamaa kama ni msomi na yupo serikalini Kwa akili hizi kupiga HATUa ni ngumu sana ajiuuzulu hatufai
 
Haya sasa wakuu, kwa watu waliochelewa kuiongea kwa ufasaha hiyo lugha ya Kiingereza na wanauhitaji nao mkubwa, nini wafanye na kupata matokeo bora kwa muda mfupi.
 
Nafahamu matumizi ya lugha mkuu.
Ninachomaanisha mimi lugha si kitu cha kusema ukamie sana au utumie nguvu sana kama jamaa anavyozitukuza hizo English medium,kujua lugha mara nyingi hutegemea ujanja wa mtu au uwepesi wa kichwa chake na nchi aliyopo yaani kwa mfano umeenda English medium ukakaririshwa maneno baadae ukirudi mtaani unakutana na watu wanaoongea kiswahili tu haitakusaidia usipolijua hili utaliwa sana pesa na unaweza usifanikishe vilevile.
Nina uhakika na ninachokiongea nimejifunza lugha 3 mwenyewe bila kwenda kwa mwalimu yeyote.
 
Mtaalamu wangu hii mada ipotezee hauwezi kujua Lugha bila kwenda kwa mwalimu yeyote lugha iliyojaa wakati uliopita,uliopo na ujao sema unaelewa kuwasiliana tu na ukaeleweka Lugha ni ngumu sio kama unavyoongelea kirahisi rahisi tu.
 
Mtaalamu wangu hii mada ipotezee hauwezi kujua Lugha bila kwenda kwa mwalimu yeyote lugha iliyojaa wakati uliopita,uliopo na ujao sema unaelewa kuwasiliana tu na ukaeleweka Lugha ni ngumu sio kama unavyoongelea kirahisi rahisi tu.
Tena kama sasa hivi kuna tools nyingi za kujifunzia ikiwemo AI ukishindwa na hiyo ujue una kichwa kizito
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…