Hivi kuna mtu bado anazipuuzia English medium schools?

Hivi kuna mtu bado anazipuuzia English medium schools?

Huwa mtu anaeponda lugha hususani English huwa namuona kama Fala. Gharama ya kushindwa kuzungumza lugha ya kimataifa nikubwa mno .
Watanzania wengi tunakosa fursa nyingi za kikazi kibiashara kwa sababu ya lugha sii kwamba sisi ni wajinga ila lugha.
 
EMS hazifundishi kiingereza. Ingekuwa wazazi wanajua kiingereza wangeshtuka kitambo.

Waalimu wenyewe wametoka kayumba ndo wafundishe kiingereza?

Tanzania hatuna utamaduni wa kuizungumza hiyo lugha.
Hiki ndicho kitu nilichomueleza huyu jamaa mtoa mada ila haelewi kwa vile tayari ameshamezeshwa na kuingiziwa hiyo imani kwenye kichwa chake kwamba kule English medium ni ngumu sana kumnasua mtu wa aina hiyo kutoka kwenye huo mtego
 
Nimepita huko mkuu najua ninachokisema. Hawajui na hawa-practice.

EMS zina faida ya miundombinu—Madarasa, madawati, chakula nk. ila elimu bora Tanzania wanapata watoto wachache mno.
Huu ni ukweli kabisa......
Mtoto wangu wa kwanza alisoma hizo EMS hakuna kitu ilikuwa ni jitihada zake tu binafsi!!!!
alivyomaliza la saba nikampeleka Benjamini Mkapa.
Hawa wengine sijafanya huo ujinga nimepeleka International school
 
Kaka muulize huyo mrusi akija Africa hapa ataongea na nani kama hajui kingereza? Ilihali wasomi wetu kiasi Fulani ndio lugha yao, muoneshe hii picha, na ajue madhara makubwa yaliyopo hapa,
Kuna tools za kufanya translation, kuna watu ndio kazi yao kutafsiri na wanalipwa. Kama lugha yako ina mashiko duniani wala sio issue siku hizi. Swali ni kwamba, kiswahili kinatosha kwenye taaluma?
 
Kuna tools za kufanya translation, kuna watu ndio kazi yao kutafsiri na wanalipwa. Kama lugha yako ina mashiko duniani wala sio issue siku hizi. Swali ni kwamba, kiswahili kinatosha kwenye taaluma?
Kaka inshu ya kuajiri mkalimani sio poa Kuna private issues sio mpaka mwingine ajue mnacho zungumza, lakini pia Kwa lugha ya urusi ni ngumu hata MIKOANI kumpata mkalimani kaka
 
Kaka inshu ya kuajiri mkalimani sio poa Kuna private issues sio mpaka mwingine ajue mnacho zungumza, lakini pia Kwa lugha ya urusi ni ngumu hata MIKOANI kumpata mkalimani kaka
Mtu akija kwa issues za kibiashara hakuna chochote private, utatafuta mkalimani mfanye biashara. Kama ni issue private hata msipoelewana mnaweza kuelendelea tu😃.
 
Tundu lissu Alisha wahi kulalamika, mawakili Fulani kingereza chao hakikua vizuri, mwingine akaenda mbali kumbe zile international case zinatubwaga huenda lugha, ukiona mzazi anatoa mamilioni fedha ana maana yake


Mtu anataaluma ya habari, lakini hawezi kuhoji Kwa kingereza lakin huyu mtu ana taaluma yake? Kumbuka kipindi kile Rick Ross kaja, wakamsusia vmoney na hawa wa Jana changamoto tupu
Kimombo ni muhimu Sana, sie tuliopita kayumba tunajua mziki wa kushindwa,
Kujieleza mbele ya watu, mwaka wa mwisho nipo mbele ya jopo la msprofesa wa UD pale DIT, nafsnya presentation ya project, kupitia prototype yangu! Acha kabisa,
Kizungu ni muhimu,
Hata kama hutaenda huo mkondo,kwani kuna ubaya gani kujua lugha ya kigeni vzr!
Kitaa watu huwa wanashindwa kujua mi kabila gani,
Naongea kimakua, kichags, kisukuma, kigogo,
 
Mkuu, kujifunza Kiingereza na kukimudu ni juhudi zako binafsi sio lazima ukasome hizo shule.Tena kwenye huu ulimwengu wa teknolojia, unaweza kujifunza na kumudu kabisa lugha yoyote unayoitaka sio Kiingereza tu. Mimi nilisoma kidumu na mfagio ila nimemaliza la saba Kiingereza nakimudu kabisa hadi kujielezea maana nilikuwa napenda kusoma vitabu na movie pia zilinisaidia. Kwahiyo mimi mtu akinambia hawezi Kiingereza kisa kasoma shule za Kayumba nakuwa simuelewi yaani.
 
Back
Top Bottom