Hivi kuna ofisi ina urasimu na usumbufu kushinda ardhi?

Mungu wakati anamfukuza Adamu kwenye bustani ya Edeni aliilaani pia ardhi anayokwenda kukaa juu yake. So hayo masahibu ni sehemu tu ya ..........
 
Wakuu
Nimefanya maombi ya hati ya ardhi mwaka wa pili unakatika. Kutoka dawati moja kwenda lingine faili linaweza kutumia miezi mitatu!

Nyie experience zenu zikoje na hizi ofisi za ardhi?
Kiukweli urasimu ni mkubwa sana. Wanatumia loophole ya watu kutokujua utaratibu wa masuala ya ardhi kutengeneza mazingira ya kuchelewesha huduma ili utoe kitu kidogo.
 
"Ndio kwanza tunajidaiiii (mkeshe mkisema),

Kama afisa wa nida (mkeshe mkisema)..."
 
Hakuna watu pasua kichwa kama idara ya aridhi,tatizo kuna mikono ya wengi,takukuru sijui wako wapi kuwadhibiti hawa jamaa?,hadi jalada la kuiweka hiyo hati inatakiwa kulipia!!!,huwa nashangaa ati, wakati kwa mjibu wa utafiti,watu wote wakupewa hati serikali inaweza kuingiza mapato mengi sana kwa kukusanya kodi ya aridhi na nchi ikapiga hatua kubwa tu,kimaendeleo.
 
Hao TAKUKURU wenyewe inabidi waundiwe TAKUKURU yao. Alisikika hayati mmoja akisema
 
Hati Moja ya ardhi ati inahitaji baraka la Baraza la madiwani! Nani alitunga hii Sheria? Madiwani wakae wapitie Kila application Moja?!!!
 
Wangeweka Online application ili mtu amalize kwenye mtandao kama TRA wanavyofanya.
Wakose rushwa? Rais Kikwete aliwahi kusema kumaliza rushwa pale ardhi ni kazi.

Watumishi wa umma wasio waaminifu wanaichukia sana biashara ya online, wanatamani watu wajazane maofisini wawaweke ili kutengeneza mianya ya rushwa.
 
kuna mfumo wa online umeanza kufanya kazi mikoa ya Dodoma na Arusha, unaitwa E-Ardhi ambapo e-Ardhi inakupa uwezo wa kufuatilia huduma ulizoomba ikiwa ni pamoja na kujua imefikia hatua gani, imekaa Wizarani kwa muda gani, hatua ngapi zimebaki ili kukamilika.
 
Njia pekee ya kukomesha uzembe ni kuweka utaratibu kama huu wa online. Hii inampa nafasi kiongozi kupitia mfumo na kuona ni mambo mangapi hayajafanyiwa kazi na kwa muda gani ili awafinye watendaji wake.

Unatengenezwa mfumo ambao hata wale viongozi wakuu watatu pale juu wanaweza kuingia na kuangalia hali inakwenda vipi, hapo uzembe na rushwa vitapungua kidogo.

Huwezi kuwa na hoja ya kujitetea maombi yapo sawa yakae bila kufanyiwa kazi kwa miezi sita, labda kama watumishi hawaendi kazini.
 
Wakuu
Nimefanya maombi ya hati ya ardhi mwaka wa pili unakatika. Kutoka dawati moja kwenda lingine faili linaweza kutumia miezi mitatu!

Nyie experience zenu zikoje na hizi ofisi za ardhi?
yaani hii kitu imenikuta tunduru mwaka wa pili sasa naambiwa file ipo kwa msajili na bagamoyo urasimu wa watu wa ardhi ni mkubwa sana sana
 
Back
Top Bottom