Hivi kuna uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha?

Pole sana dada kwa yaliokukuta, umetumika bure maskini. Watu wa Ulaya wengi wao hawana kitu zaidi ya mbwembwe tu. Kwa kifupi Bongo wapo watu wengi sana wanatengeneza hela kuliko waliopo Europe. Maisha ya Europe na America sio mepesi kiivo.

Muuza chips goli likimchanganyia kidogo tu ni bora mara 100 kuliko hao jamaa wa Ulaya.
 
Kwa kweli napokea pole yako kwa Moyo mkunjufu,kuishi Ni kujifunza.Tangu nipate hicho kisanga Cha kwanza nikidhani nimepata bingo kumbe bungo basi nimekuwa mdadis Sana kwa Hawa wanaojiita global citizen...na wengi hamna kitu...Vijana mliopo Bongo mna heshima zangu nyingi Sana pamoja na changamoto za tozo Ila mnapambanaaa
 
Huko South mbona Kama ndio hatari sana mdau?
Nje kuna exposure ni akili tu ya mtu
Mimi nina mtu nilimpeleka Sauzi. Sasa ameoa, amepata uraia, ana biashara kubwa, mama yaje kamjengea jumba la kisasa huku Dar, anamsomeshea dada yake watoto waliotelekezwa. Na mimi wakati nampeleka kaenda hana anayemjua. Niliyekua namtazamia awe mwenyeji wake ilishindikana. Elimu yake ana diploma alitoka nayo Bongo

Wapo naowajua wamebutua Canada, na Ulaya vilvile. Ni jinsi mtu unavyochanga karata zako tu.
 
Kila siku mnakandia wabeba box afu mnakuja inbox kuuliza jinsi ya kuja kiwanja 😀

Hao wachache maisha yamewachapa mbona huongelei waliotoboa huko ughaibuni. Kila sehemu wapo wanaofanikiwa na wanaofeli.

Unataka kusema wote waliobaki bongo wametoboa? Mbona kila siku mnalia njaa. Tukidondoka wanyamwezi toka kiwanja ni kupigwa mizinga tu.

Wapo kibao waliotoboa nje sema wewe inaonekana circle yako ni ya waliosanda so unakutana na waliofulia wenzako, wengine tunadondoka bongo kila siku spending like there's no tomorrow na kurudi kiwanja. Tupo in the corporate world now tushapita kubeba box. Tunawekeza pia for our families ikibidi hata kuiba rasilimali maana bongo watu bado wamelala usingizi wa pono wanasubiri serikali iwafanyie kila kitu.

Nimerudi kiwanja last week toka kula vumbi bongo. Kama unataka kuja kiwanja usisite kuuliza 😜

Cc Nyani Ngabu
 
Uko sahihi...Kuna mpuuzi hapa amekaa South Africa miaka nane. Alichorudi nacho ni cheni ya Silver na simu na sasa anataka nimkopeshe nauli eti akifika Dizonga' atanitumia double ya kiasi nitakachompa.
Ukimtumia nauli umeliwa mkuu, huko nje ya nchi ukiwa mtaalamu hufi njaa ila ka wabangaiza kule kila sector imeshafanyiwa kazi na kutoboa ngumu sana, tofauti na bongoland
 
Wa UK Wana Hali gani?
Mmoja babmkwe ndo kampiga tafu vitu kadhaa ndio kasimama other wise hakuwa na mbele Wala nyuma.wengine maisha ya kuunga unga yaan walirudi tz ndio tuseme wameanza upya. Mimi naona walio marekani WENGI WAO sio wote wako better zaidi kuliko walioenda UK

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
cultural shock! Inapelekea mlengwa kupata post traumatic stress disorder! (PTSD) nafikiri ni jibu unalolitafuta.
 
Aiseee Bora kudanga Tanzania kuliko kupoteza muda huko Ulaya....rudini tu kwa kweli
Mimi Niko bongo hapahapa ila Mwanaume ambae anatafuta maisha kiasi Cha kuizunguka dunia hawezi kuitwa amefeli hata kama bado hajapata/hajafanikiwa huyo anaitwa mpambanaji, ndo maana askari anaefia vitani bado anazikwa kwa heshima hata kama hakushinda vita ila ujasiri wake wa kusimama katkat ya njia za risasi unatosha kupewa heshima.

Bali mwanamke asie na mapenzi ya dhati ambae anaingia kwenye mahusiano na mtu asiempenda ila anautoa mwili wake kingono kwa mategemeo na nia ya kupata hafadhali ya kimaisha kupitia mgongo wa mwanaume mtafutaji mwanamke huyo ndo amefeli maisha, maana utatumika sana na wanaume wanaoigiza maisha Hadi utachakaa
 
Inategemea mtu na mtu na pia nchi uliyoenda na malengo yako pia.

Hata bongo mbona Kuna waliofanikiwa na waliofeli.

Kuna bidada yuko zake US anabusti ndugu zake, ana viwanja na nyumba bongo na amenunua apartment huko huko US .

Kwahiyo haya mambo ya kufanikiwa au kutofanikiwa kwa mtu yanachangiwa na vitu vingi. So msipende ku- conclude kwa hao wachache mnaowafahamu au kuwaona au kuwasikia.

Kuna nchi nje ni bora kwenda kwaajili ya kupambana kuliko hata bongo. Vishughuli vya kufanya vya hapa na pale hukosi ,malengo Ni muhimu usijisahau na pia usisahau kuishi kuenjoy maisha yenyewe mafupi haya tena Yenye tabu nyingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…